Nimekuwa nikifuatilia harakati za Chadema kwa muda mrefu sasa, linapokuwa linatokea jambo gumu linalohusu Taifa Chama hiki maarufu kimekuwa nyuma sasa kutoa msimamo wao. Mfano tukio la Mbagala na Zanzibar, haya kila mtu anayajua jinsi yalivyotokea lakini Chama makini bado wao hawajasikia hayo matukio labda wapo mbali na vyombo vya habari kama walivyosema. Mimi nafikiri kama kunakuwepo na mkutano sehemu ni bora wanachama tukawajulisha kabla hawapanda jukwaani ili jambo la kwanza kiongozi apandapo jukwaani aonyeshe basi kuguswa hata kama haguswi. Wananchi wanaotarajiwa kuongozwa ndo hao hao wanaopatwa na majanga kama hayo tuwaliwaze hata kwa kauli ambazo tunajua ni danganya kubwa, kwa haya viongozi wa Chadema siwatofautishi na Rais Kikwete.
Kinga ni bora kuliko tiba
Mbona cdm hawatoi tamko kuhusu ndoa ya katibu wao mkuu