Ukimwi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
Huu ni ugonjwa wa zinaa ulio hatari zaidi kwa binadamu. Unasababishwa na kirusi kinacho sambazwa kwa urahisi wakati unapofanya mapenzi. Pia huambukiza watoto ambao hawajazaliwa wakati wa kuzaliwa na

wanaponyonyeshwa. Hakuna tiba ya HIV na hivi sasa zaidi ya watu milioni 30 wameambukizwa kote ulimwenguni. Wengi wa watu walioambukizwa huishi katika nchi za Afrika zilizoko chini ya jangwa la Sahara na Wakenya 500 hufariki kila siku kutokana na Ukimwi.

Virusi huingia mwilini na kuharibu seli za ulinzi katika mwilini
(kinga ya mwili). Pindi tu kinga ya mwili imedhoofika, mwili huathirika na maambukizo mengine mengi ambayo husababisha kuharisha, kutapika, kuumwa na kichwa, homa ya uti wa mgongo (menengitis), maambukizi ya ngozi na nimonia na hatimaye mtu asipotibiwa hufariki kutokana na moja ya maambukizi hayo.

Kuna madawa yajulikanayo kama ARV yanayopatikana katika hospitali za wilaya ambazo hupunguza kiwango cha ukuaji wa virusi katika mwili. Madawa haya kwa hivyo yataendeleza afya ya mtu na kurefusha maisha yake. Hata hivyo hii sio tiba na virusi vitabakia mwilini. Mtu aliyeathirika anaweza kumuambukiza mtu mwengine na mbaya zaidi anaweza kujiambukiza tena mara tena. Na kwa kila ambukizo, kinga ya mwili hudhoofika na afya ya mtu hudhoofika.

Unaweza kufanya nini?

Tanguliza kwa kujikinga unapofanya ngono

Ngono za Usalama.

Ngono salama: Fanya jambo la sawa
Ngono ni sehemu muhimu kwa maisha ya mtu mzima, lakini usipojikinga waweza kupata mambo usio tarajia, au magonjwa ya zinaa ambayo ni hatari kama ukimwi. Mnaposhiriki ngono na mpenzi wako tumieni mipira ya kondomu, mnapofanya mapenzi bila kondomu, hatari ya kuambukizana magonjwa ipo.

Jinsi gani ya kushiriki ngono kwa usalama?

Unapomfahamu mpenzi wako ndio bora na salama. Ngono ya usalama ni hatua yoyote unayochukuwa kupunguza magonjwa ya zinaa. Magonjwa mengi ya zinaa husababisha ugumba/tasa, ulemavu wa watoto na maumivu. Kujikinga, kuwa muaminifu kwa mpenzi mmoja na fanya maamuzi ya busara.

Ni zipi njia bora za kuzuia maambukizi?
  • Tumia kondomu
  • Usiguse vidonda vitokanavyo na magonjwa ya zinaa
  • Msishiriki ngono ikiwa mpenzi wako ana vidonda sehemu nyeti au maambukizi yoyote.
  • Nenda kwa uchunguzi kwa daktari kila mara
  • Ukiwa umeambukizwa pata matibabu mara moja.
Nenda ukapimwe iwapo unakuwa na Virusi vya ukimwi

Je unajua hali yako ya HIV?

large_musa_in_studio_pic_by_joyce.jpg
Jina langu ni Musa Harun. Mimi ni mwanafunzi katika Chuo cha Teknologia na pia ni kijana anayefunza vijana wenzake kuhusu afya. Kuwa kijana anayewafunza vijana wenzake kunahitaji mtu kuwa mfano mwema na aweze kutoa mwelekeo. Hii ndio sababu nilienda katika kituo cha VCT ili kupimwa ikiwa nina virusi vya HIV.


Kituo kinachotoa huduma za ushauri na upimaji wa hiari (VCT)


Maono yetu ni kukuza ufahamu wa hali ya HIV kupitia uvumbuzi wa mikakati ya kutoa ushauri na upimaji.
Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa katika sehemu ya mapokezi katika kituo cha VCT nilichokitembelea huko Kericho. Kama kijana aliye katika miaka ishirini ya mwanzoni, nilikaa pale, huku nikiwa nakerwa. Ilikuwa kama kwenda katika majaribio ya mambo

uliyofanya maishani huku ukiwa hauna dhana yoyote kuhusu matokeo ya uamuzi na jambo hili linaweza kuwa la kuogofya. Nilikuwa hapa kupimwa HIV.


Niliitwa na kuingizwa katika chumba kidogo.Kina meza moja pekee,viti vitatu na vifaa vinavyotumiwa katika upimaji.Mwanadada aliyenikaribisha alinionyesha urafiki na alinisemeza kwa upole. Alikuwa kijana kama mimi na alipoanza kutoa maelezo kuhusu kile kitafanyika, nilihisi naanza kupumzika.


Kabla ya upimaji

‘Kabla ya upimaji, ningependa tuzungumze kidogo kukuhusu na HIV na UKIMWI'. Nilitikisa kichwa na aliendelea kunielezea mambo muhimu kuhusu usambazaji wa HIV na jinsi hukua hadi kufikia UKIMWI. Pia alinieleza jinsi upimaji utafanyika. Alimalizia, `kumbuka ya kwamba mistari miwili inaashiria ya kwamba una VVU, mstari mmoja unaashiria ya kwamba hauna HIV.'

Kisha ikafika sehemu iliyokuwa ngumu; '‘Ushawahi kushiriki ngono?''aliniuliza. Niliona aibu. Nilitaka kudanganya lakini nilifahamu hiki kilikuwa kilele cha majaribu. Nilikuwa hapa kujua ukweli kwa hivyo nilihitajika kuwa mkweli. Nilijibu ndiyo, nikiwa na matumaini ya kwamba hataniuliza nilishiriki ngono na nani na mara ngapi. Kwa bahati nzuri kile kilichofuatia hakikuguzia ujinsia wangu. Alinihakakishia ya kwamba kufanyiwa upimaji lilikuwa jambo bora kwani licha ya matokeo; itanisaadia kuchukua hatamu ya maisha yangu.

Upimaji


Kufikia hivi sasa nilijihisi mtulivu.Kisha akaniuliza ikiwa nikuwa tayari kwa upimaji. Nilisema ‘ndiyo'. Alivaa glavu zake na kisha akasafisha kidole changu cha pete na antiseptiki. Kwa kuwa na utambuzi kuwa ni haki na wa kufanya jambo kutokana na miaka 2 ya utendaji kazi, mshauri alidukua kidole changu na kutoa tone la damu na kuliweka kwenye kifaa kinachotumiwa kupimia.


Huku nikiwa nimekodoa macho, nilitazama jinsi vidole vyake viliruka kutoka kwa kitu kimoja hadi kingine katika onyesho ambalo limefanyika zaidi ya mara mia moja kabla yangu. Ilinibidi ningoje dakika 15 ili matokeo yawe tayari. Hizi dakika 15 zilinikulia kama kwamba ni milele na niliteswa kiakili vibaya.


Katika akili yangu, nilianza kujiuliza. Kweli nilikuwa tayari kujua hali yangu? Kwani ilikuwa lazima? Je ikiwa nina HIV? Ndiyo nilikuwa nimepitia ushauri lakini ni kawaida kwa binadamu kuogopa. Nilijaribu kujipa moyo. Maelfu ya watu wamepimwa tangu vituo vya VCT vianzishwe. Baada ya kupiwa watu wengi wameishi na matumaini na na virusi hivi. Nilifahamu ya kwamba mimi niko katika kikundi kinachoshiriki ngono na ambacho kinakisiwa kuwa katika hatari kubwa ya kupata HIV. Kwa hivyo nilisubiri. Mshauri alisubiri nami huku tukiongea polepole. Alikuwa akinipoza.


Matokeo

'‘Nafikiri matokeo yako yako tayari na unaweza kuyatazama.Kumbuka ya kwamba mistari miwilli inaashiria ya kwamba una HIV, mstari mmoja unaashiria ya kwamba hauna HIV,'' mshauri wa VCT alinieleza. Katika hatua hii miguu yangu ilikuwa
ikitetemeka na sikuwa naona vizuri. Mahali ninapotoka sisi husema mtu anapaswa kujitayarisha kufa mara mia moja. Wakati ulikuwa umewadia. Nilipiga moyo konde na nikatupia jicho kifaa kinacho onyesha matokeo ya upimaji - mstari ulikuwa tu mmoja. Ungehisi kushusha pumzi kwangu kwa faraja hata ikiwa ungekuwa nje! Nilikuwa na furaha isiyo na kifani.


Baada ya upimaji


Mshauri alinishauri jinsi ya kubakia bila ya HIV kwa kuzingatia kanuni ama ABC za kuzuia uambukizaji wa HIV na UKIMWI ambazo ni kutoshiriki ngono, kuwa mwaminifu ama kutumia mpira wa kondomu kila unapofanya mapenzi. Lakini bado nilikuwa na swali moja la mwisho, ‘Je ikiwa ningepatikana nina HIV?' Mshauri alinijibu, ningekupa ushauri wa jinsi ya kusimamia hali

yako ya HIV. "Ningekutuma kwa mtu anayetoa huduma ya matibabu ili uanze usimamizi wa HIV".

Nilitoka kwenye chumba hicho nikiwa na furaha, lakini pia nikiwa na jukumu kubwa la kuwashauri marafiki zangu, huku nikiwa na ufahamu ya kwamba kujua hali yako ya HIV kunakupa usimamizi wa maisha yako.


 
Magonjwa tegemezi yanayosababishwa na kuwa na virusi vya Ukimwi

Maambukizi tegemezi au Opportunistic infections (OI) kwa Kiingereza ni maambukizi yanayojitokeza na kuvamia mwili wakati kinga yako iko chini sana. Unayapata unapoanza kuwa na Ukimwi. Mengi ya maambukizi haya yanaweza kuathiri watu

ambao hawana virusi vya Ukimwi. Lakini huwa ni hatari sana kwa watu ambao tayari wana Ukimwi.

Iwapo una Ukimwi na upate dalili zozote za magonjwa yaliyotajwa hapa chini, ni lazima upate matibabu mara

moja. Vituo vya afya vya kiserikali hutoa huduma za afya kwa maambukizi tegemezi yanayo sababishwa na Ukimwi. Pia wao huwapa bure dawa za kupunguza makali dalili za haya maambukizi (OIs) huwa haimaanishi kuwa una Ukimwi lakini ni muhimu ufanyiwe uchunguzi ili upate matibabu yanayofaa haraka iwezekanavyo.


Dalili za kawaida za haya maambukizi
  • Vipele – hasa vya kiunoni
  • Ugonjwa wa kifua kikuu
  • Kuvimba ulimi na ufizi
  • Ugonjwa wa mapafu unaomfanya mgonjwa ashindwe kupumua vizuri wa aina ya PCP – Penumocystis Causini Pneumonia
Matibabu Hospitalini

Kuna mambo machache ambayo unatakikana kuyafanya na machache ambayo hutakikani kuyafanya.
  • Nenda kwa kituo cha afya cha umma ama umwone daktari wa kibinafsi aliye mjuzi wa mambo yanayohusiana na ukimwi. Ukishahakikisha kuwa, una muuguzi au daktari unayeweza kumwamini na una uhusiano bora naye, nenda mara kwa mara wakuangalie ili waone vile unavyoendelea kudhibiti maambukizi ya ukimwi.
  • Utahitaji ufanyiwe hesabu ya chembechembe zako za CD4 na wingi wa maambukizi yaliyo mwilini mwako mara mbili kwa mwaka
  • Karibu kila mtu aliye na virusi vya Ukimwi (asili mia 97%) baadaye atapata ugonjwa wa Ukimwi au
  • magonjwa mengine yanayohusishwa na ugonjwa huu. Haya huitwa, magonjwa yanayotumia nafasi hii ya hali iliyoko mwilini kukuangamiza. Karibu magonjwa yote ya aina hii yanaweza kutibika kwa kutumia dawa zilizodhibitishwa.
  • Kwa watu wengi, Ukimwi ni ugonjwa ambao hauwezi kutibiwa hata hivyo, ni hali inayoweza
  • kudhibitiwa kama magonjwa mengine yoyote ya kudumu ambayo hayana tiba. Watabibu wanajua kuna dawa za kudhibiti haya maradhi, (antiretrovirals - ARVs) ya kusaidia watu kuishi maisha ya
  • kawaida na kwa mda mrefu wakiwa na virusi vya ugonjwa huu. Hata hivyo unachohitaji kujua ni
  • kuwa ni muhimu uanze kutumia hizi dawa za ARV za kudhibiti ugonjwa hasa unapo ambukizwa na maambukizi yanayoambatana na magonjwa haya (yanayojulikana kama magonjwa yanayotumia
  • nafasi au hali ya mwili wako ya kuwa umeambukizwa). Ama wakati ambao chembechembe zako za CD4 ni chini 350. Kwa watu wengi walio na virusi vya ukimwi, haya hutokea kwa kati ya miaka 8 – 10
  • baada ya maambukizi. Hata hivyo kuna hali fulani ambazo hazifuati hali hii.
  • Kuna ushahidi wa kuaminika kuwa ukitumia tembe badala ya vitamini kila siku kidogo unapunguza
  • makali ya ukimwi na haukuporomoshi haraka. Jaribu utumie tembe badala zilizo na vitamini B, C na
  • E. Vituo vya afya vya umma vinafaa kuwapa wagonjwa bure, bila malipo, hizi tembe. Tambua kuwa
  • kuna madai mengi ya uongo kuhusu hizi tembe badala ya vitamini. Haya madai huwa yametiwa chumvi na poroja kali. Haijathibitishwa bado iwapo, mtu anakula virutubishi vyote vya mwili kwa chakula anastahili pia kutumia tembe hizi ili ziwe za manufaa kwake.

 
Jua haki zako kama mgonjwa anayeugua ugonjwa wa Ukimwi

Jihusishe na vita dhidi ya Ukimwi

Ukimwi umeua watu mengi sana. Kuna njia nyingi za kukabiliana na ugonjwa huu. Kabla ya kujifunga utepe mwekundu, jua ukweli ufuatao kuhusu ugonjwa huu!​
  • Watu watano hufariki kila dakika ulimwenguni kutokana na ugonjwa na ukimwi
  • Watu elfu arobaini huishi wakiwa na virusi vinavyosababisha ukimwi
  • Kutojihusisha na ngono kabisa ndiyo kinga kamili ya kuzuia na kujikinga kutokana na ugonjwa huu.
  • Kuna jinsi nne tu za kukuambukiza ugonjwa huu.
  1. Kupitia kwa damu iliyo na virusi
  2. Shahawa/manii
  3. Unyevunyevu wa sehemu za siri za mwanamke
  4. Maziwa – wakati ambapo mama aliye na virusi humnyonyesha mwanawe
Wanawake wana nafasi kubwa sana ya kupata virusi vya ukimwi.

Hata kama huna virusi vya Ukimwi, unaweza kuwasaidia mamilioni ya watu ambao wameambukizwa kwa kujishughulisha na mambo yafuatayo.

Jihusishe na ngono salama

Kuvalia kipira cha kondomu wakati wa kufanya mapenzi ndiyo njia nzuri zaidi ya kuzuia kupata virusi vya Ukimwi. Iwapo utajihusisha na ngono, jikinge wewe pamoja na mpenzi wako.

Enenda ukapimwe uone kama una virusi vya Ukimwi

Hata kama unaona kwamba hakuna vile unaweza kuwa umeambukiwa ugonjwa
huu, fikiria kuhusu kupimwa ili ujue hali yako. Heshimu afya yako na
ya mpenzi wako kwa kujua hali zenu.

Valia utepe mwekundu

Kuvalia utepe mwekundu ni ishara ya kuonyesha kuwa unawaunga mkono walio na virusi vya Ukimwi. Ukiwa nyumbani, valia utepe huu. Waulize marafiki zako wafanye vivyo hivyo. Pia unaweza kutoa kwa tarakilishi yako utepe na utumie watu kwa barua pepe.

Tuma ujumbe wa ‘Siku ya Ukimwi Duniani’ kama Agano (Promise)

Siku hii huadhimisha agano kutoka kote ulimwenguni kuhusu yale ambayo watu wamepanga kuzuia ugonjwa Ukimwi. Unaweza kuandika ujumbe kwenye mtandao wako wa kibinafsi akiapa ahadi hii. Huu ujumbe utatumwa kwa wanasiasa na viongozi wote kote duniani.

Zungumzia watu shuleni na mahali pako pa kazi.

Fanyeni mazungumzo na wote walio karibu nawe. Wafunze yote unayojua kuhusu Ukimwi nawe pia ukajifunze kutoka kwao yote wayoyajua.

Changisha pesa kusaidia mradi wowote wa Ukimwi

Kama unajua kupika, tengeneza mandazi au chochote. Kiuze na upate pesa za mradi huu. Unaweza kutuma pesa utakazopata kwa mfadhili yeyote utakayemchagua.
 
Kuishi vyema na HIV na UKIMWI

Ikiwa umetoka kupimwa na umepatikana na VVU, tukio hili linaweza kuwa la kuogofya. Hata hivyo, ni muhimu kufahamu ya kwamba kuwa na HIV hakumaanishi ya kwamba utakuwa mgonjwa mara moja na utafariki hivi karibuni.

Virusi vya HIV vinaweza kudhibitiwa kwa utunzi mwafaka, tiba na kuwa na mafikira mema, mtu anaweza kuishi maisha ya kawaida kama mtu yeyote.
Ni nini kwanza unachofaa kufikiria ama kufanya ikiwa una HIV?

HAUKO PEKEE YAKO


Hii ni kwa sababu:-
  • Kuna watu wengi wenye virusi vya HIV
  • Kuna watu wengi wenye UKIMWI
  • Watu wengi wanasumbuliwa na VVU na UKIMWI
ONGEA NA MTU

Watu wenye HIV na UKIMWI wanahitaji kuongea na mtu kuhusu hali yao ama mafikiria yao. Ni jambo la kuogofya kuwa na HIV ama UKIMWI. Unaweza pata ya kwamba utapunguzia mzigo ikiwa utaongea na mtu anayeelewa.

ISHI KAMA KAWAIDA

Ikiwa una VVU na UKIMWI usikate tamaa.
  • Kuwa msafi na vaa nguo nadhifu
  • Jishughulishe.
  • Fanya kitu kitakachowasaidia watu. Jihusishe na familia na marafiki zako – usijitenge nao – bado wanakuhitaji.
TANGAZA HALI YAKO IJULIKANE
Ikiwa una VVU ama UKIMWI usijifiche. Mwanzoni watu watakuzungumzia lakini usife moyo.
  • Jishughulishe katika jamii. Kwa njia hii, wengine wataanza kukuona kama mwanajamii wa kawaida na mwenye manufaaa katika jamii na wataanza kukuthamini. Inaweza pia kuwapa hima wangine kama wewe na pia inaweza kuwa njia kwako na kwao kujenga kikundi cha kujisaidia.

KUWA NA TAFAKARI NJEMA KUJIHUSU

  • Jivunie. Usiwache kile mtu anasema kikuvunje moyo.
  • Wewe bado ni muhimu. Wewe bado ni wewe. Tembea wima.
Katika sehemu hii, unaweza kupata habari jinsi watu wenye HIV na UKIMWI wanaweza kujilinda na kujitunza na kuwatunza wale walio karibu nao.
 
mkuu, hizo ulizoweka hapo chini ndio haki za mgonjwa anayeugua UKIMWI?
Jua haki zako kama mgonjwa anayeugua ugonjwa wa Ukimwi

Jihusishe na vita dhidi ya Ukimwi

Ukimwi umeua watu mengi sana. Kuna njia nyingi za kukabiliana na ugonjwa huu. Kabla ya kujifunga utepe mwekundu, jua ukweli ufuatao kuhusu ugonjwa huu!​
  • Watu watano hufariki kila dakika ulimwenguni kutokana na ugonjwa na ukimwi
  • Watu elfu arobaini huishi wakiwa na virusi vinavyosababisha ukimwi
  • Kutojihusisha na ngono kabisa ndiyo kinga kamili ya kuzuia na kujikinga kutokana na ugonjwa huu.
  • Kuna jinsi nne tu za kukuambukiza ugonjwa huu.
  1. Kupitia kwa damu iliyo na virusi
  2. Shahawa/manii
  3. Unyevunyevu wa sehemu za siri za mwanamke
  4. Maziwa – wakati ambapo mama aliye na virusi humnyonyesha mwanawe
Wanawake wana nafasi kubwa sana ya kupata virusi vya ukimwi.

Hata kama huna virusi vya Ukimwi, unaweza kuwasaidia mamilioni ya watu ambao wameambukizwa kwa kujishughulisha na mambo yafuatayo.

Jihusishe na ngono salama

Kuvalia kipira cha kondomu wakati wa kufanya mapenzi ndiyo njia nzuri zaidi ya kuzuia kupata virusi vya Ukimwi. Iwapo utajihusisha na ngono, jikinge wewe pamoja na mpenzi wako.

Enenda ukapimwe uone kama una virusi vya Ukimwi

Hata kama unaona kwamba hakuna vile unaweza kuwa umeambukiwa ugonjwa
huu, fikiria kuhusu kupimwa ili ujue hali yako. Heshimu afya yako na
ya mpenzi wako kwa kujua hali zenu.

Valia utepe mwekundu

Kuvalia utepe mwekundu ni ishara ya kuonyesha kuwa unawaunga mkono walio na virusi vya Ukimwi. Ukiwa nyumbani, valia utepe huu. Waulize marafiki zako wafanye vivyo hivyo. Pia unaweza kutoa kwa tarakilishi yako utepe na utumie watu kwa barua pepe.

Tuma ujumbe wa ‘Siku ya Ukimwi Duniani' kama Agano (Promise)

Siku hii huadhimisha agano kutoka kote ulimwenguni kuhusu yale ambayo watu wamepanga kuzuia ugonjwa Ukimwi. Unaweza kuandika ujumbe kwenye mtandao wako wa kibinafsi akiapa ahadi hii. Huu ujumbe utatumwa kwa wanasiasa na viongozi wote kote duniani.

Zungumzia watu shuleni na mahali pako pa kazi.

Fanyeni mazungumzo na wote walio karibu nawe. Wafunze yote unayojua kuhusu Ukimwi nawe pia ukajifunze kutoka kwao yote wayoyajua.

Changisha pesa kusaidia mradi wowote wa Ukimwi

Kama unajua kupika, tengeneza mandazi au chochote. Kiuze na upate pesa za mradi huu. Unaweza kutuma pesa utakazopata kwa mfadhili yeyote utakayemchagua.
 
MARPs ni kina nani?

inject_drug_0.jpg


Neno MARPs linasimamia Most At Risk Populations - Watu waliomo katika hatari kubwa. Hutumiwa kwa kikundi cha watu ambao wako katika hatari kubwa zaidi ya kupata na kusambaza HIV. Hii ni kwa sababu wao hujihusisha na mienendo inayojulikana
Kuwaweka katika hatari ya kupata HIV.

Tabia hizi ni:-
  • Kuwa na wapenzi wengi.
  • Kubadilisha wapenzi kila mara.
  • Kufanya mapenzi kwa uke na Tigo bila kutumia kinga.
  • Kutumia sindano moja.

Makundi ya hawa watu ni:-

  • Makahaba na wapenzi wao
  • Wanaume wanaoshiriki ngono na wanaume wenzao
  • Wafungwa
  • Watu ambao hutumia dawa za kulevya kwa kujidunga sindano
  • Madereva wa malori yanaoenda masafa marefu.

Ni kwa nini tufadhaike kuhusu MARPs?


Kando na dhana wanajihusisha na ngono inayowaweka katika hatari kubwa, pia kuna mambo mengine ya kusikitisha:
  • Ukosefu wa upatikanaji wa huduma za Ukimwi. Mienendo yao hufanywa hatia na wao hushutumiwa na hivyo kutengwa na kufanya iwe vigumu kuwafikia.
  • Watu hawa huwakilisha theluthi moja ya maambukizi mapya ya HIV nchini Kenya ambayo inakisiwa kuwa watu 100,000 kila mwaka.

Ni nini kinachofanywa ili kuwafikia MARPs

  • Serikali imewahusisha MARPs katika mkakati na mpango wa kitaifa wa HIV/AIDS.
  • Utoaji wa huduma za kuzuia, kutunza na kutibu HIV na magonjwa ya zinaa na habari mahsusi kwa ajili yao.
Njia 3 za kuingilia kati ili kutoa huduma kwa MARPs na wapenzi wao zimepangwa:-
  • Mienendo na tabia
  • Huduma za ukaguzi na matibabu
  • Huduma za kijamii
Hivi karibuni tutatoa ni wapi huduma zilizotajwa hapo juu zinaweza kupatikana kwa watu walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa HIV.
 
Kuvimba Ulimi na Ufizi (Thrush/Candidiasis)

Ugonjwa na kuvimba ulimi na ufizi husababishwa na viini vya ukungu (candida fungus). Watu wengi huwa na hali hii miliini mwao na huwa si hali ya kutia wasi wasi. Wakati mwingine hizi bacteria zikizaana sana bila kudhibitiwa, huweza kumsababishia mtu maradhi. Watu wengi hupata haya maambukizi kwa sababu tofauti tofauti lakini kwa watu walio na Ukimwi, hutokea mara kwa mara. Wakati mwinigine mgonjwa huhisi vibaya kidogo au kujisikia tu akiwa mgonjwa sana.

Dalili na matibabu

Kuvimba vipele kwenye ulimi na ufizi
– Huwepo na mabaka mabaka meupe ndani ya mdomo. Kama uchafu mweupe kikatoka na hapo mahali hubaki pekundu sana. Pia kwenye kona za mdomo wako, kunaweza kutokea uvimbe na kukauka. Pia unaweza kutoka vipele vya mayai mdomoni mwako. Hutibiwa kwa dawa ya kuosha mdomo ya kuzuia hizo bacteria kuenea or antifungal systemic medication.

Kuvimba kwa vipele kwa koromeo – Uvimbe ukitokea kooni mwako hukufanya ushindwe kumeza chochote au ukimeza unahisi uchungu. Hutibiwa kwa dawa ya Traconazole ama Fluconazole antifungal systemic medication.

Uvimbe wa vipele kwa ngozi – Ngozi hugeuka na kuwa nyekundunyekundu na huwa na mabaka ya uvimbe ndani ambayo huwasha na huna machungu. Ngozi ya kazi ya vidole huweza kubambuka na pia sehemu ya kona kwenye makucha huwa chungu sana. Hutibiwa kwa dawa ya kupaka ya kumaliza hizi bacteria. Hizi sehemu ni lazima ziwekwe safi na kavu.

Uvimbe wa vipele kwenye mlango wa uzazi. Humfanya mtu ajikune. Pia hizo sehemu huvimba kukatokea harufu mbaya kwenye uzazi pamoja na usaha mzito mweupe unaosababisha hiyo harufu. Unaweza kuhisi uchungu na kukawa kujikuna kwenye sehemu zako za siri. Hutibiwa kwa dawa ya kujipaka ya kuzuia huo uchungu wa bacteria kuenea maambukizi yakitokea tena na teana, unaweza kupewa dawa ya kumeza ya kusafisha kila sehemu mwilini.

Uvimbe na upele unaotokea kwa nche ya sehemu ya mwanaume na kwenye hiyo ngozi ya mbele (Balanitis). Balanitis hufanya ncha ya sehemu ya siri ya mwanamume kuwa nyekundu na kuwa mabaka mabaka na sugamba kwenye ngozi ya mbele ya mboo. Mtu huhisi kujikuna na kuchomeka sehemu za siri. Hutibiwa kwa kupaka dawa ya kupaka ya kuzuia hivi vipele. Ni muhimu hizi sehemu zisafishwe vizuri. Maambukizi yakitokea tena na tena, daktari anaweza kumtaka mtu mzima atahiri.

Maambukizi kwenye damu (Systematic Thrush) Viini vya ukungu zikisambaa mwilini mwako, zinaweza kufanya viungo kushindwa kufanya kazi kabisa. Hutibiwa tu hospitalini kupitia kwa sindano inayodungwa kwenye mishipa ya damu.
 
Nimonia (Pneumonia)

Kinachosababisha ugonjwa sana sana kwa wale wa wanaougua Ukimwi ni viini vya aina ya ukungu vinavyovamia mapafu (Pneoumycitis carinii). Walio katika hatua ya kwanza ya kuugua Ukimwi ndio sana sana hupata ugonjwa huu. Huwa ndio ugonjwa wa kwanza kwa yale maambukizi humvamia mtu aliye na Ukimwi. Aina hii ya ugonjwa wa mapafu huitwa PCP.

Nitajuaje kuwa nina PCP

Huwa unajihisi ukiwa mchovu sana, unakuwa na homa kali, unapumua haraka haraka na huwa una kikohozi kisicho na makohozi. Muone daktari mara moja. Atakahikisha kuwa mapafu yako yamepigwa picha kuangalia iwapo pana dalili za PCP. Dalili hizi pia hujitokeza mtu awapo na magonjwa mengine kama vile T.B. (Kifua kikuu). Itambidi daktari wako afanye uchunguzi ndipo atambue hali inayokusumbua.

Matibabu
Mtu hupewa madawa ya kunywa mwanzoni. Iwapo ameugua sana, hudungwa dawa kupitia kwa mishipa. Pia anaweza kupewa dawa za kupunguza uvimbe na uchungu kwenye mapafu. Unaweza kuhitaji hewa zaidi ya oksigeni. Ni muhimu ufuate maagizo ya daktari wako kujitunza vilivyo.

Baada ya kupata matibabu ya PCP, huenda ukahitajika kumeza dawa zako za kila siku kwa maisha yangu yote ili uzuie mambukizi ya baadaye. Hakuna uwezekano mkubwa wa mtu kumuambukiza mwingine PCP.

Vipele

Vipele ni ukurutu mchungu unaosababishwa na ugonjwa wa tetemaji/tetewanga (Varicella – zoster virus or VZV) Pia huitwa, ugonjwa wa ngozi wa vilengelenge. Yeyote ambaye amewahi kuugua ugonjwa huu akiwa mtoto au hata mtu mzima huwa

amebelea VZV kadika seli zake za mishipa kwa maisha yake yote. Kwa wakati wowoteule kataka maisha yako VZV `uweza kechochewa tena na kujitokeza kama kipele kikubwa chekundu kinachofanana na sagamba ndogo kwenye ngozi. Madaktari

hawana hakika kuhusu kinachofanya VZV kutoke mara ya pili na wanajua kwa hakika kuwa, hakijitokezi kwa watu ambao kinga yao imehujumiwa, kama vile wale wanaougua Ukimwi.

Ingawa hali hii haihatapishi maisha yako, huwa inadhooficha mwili wako. Watu walio katika hatua ya mwisho ya kuugua ugonjwa wa ukimwi wanaweza kushikwa tena na tena na vipele hivi ambavyo huwa haiponi na vinaweza kuwa vijidudu vimelea. Iwapo

unaugua ugonjwa wa ukimwi, epukana na watu walio na vipele kwani vitadhoofisha kabisa afya yako. Pia epukana na wale walio na tetewanga. VZV huweza kuambukizwa kupitia kwa sugamba zilizo wazi.

Nitajuaje kuwa nina vipele?

Mara nyingi dalili za kwana huwa mwasho mchungu kwenye ngozi yako. Huu mwasho hutokea kwenye shingo, nyuma au kwenye kiwiliwili au hata mahali popote tu mwilini. Baada ya siku 2 au 3 ngozi itakuw nyekundu na vipele vidogo kutokea. Kwa

muda wa siku 10 – 14 hizo sagamba hubadilika na kw mavundevunde, hupasuka na kukauka kasha hupotea. Hata hivyo, iwapo unaugua ukimwi, zitachukua majuma manne kabla upone. Unaweza kuhisi uchungu mwingi au la. Tezi zako za maji ya mwilini kama damu nyeupe zinaweza kufura na kuwa chungu ukishika. Mahali ambapo hicho kipele kimetokea panaweza kubaki na baka baada ya kupona.

Wakati mwingine, mtu huweza kuhisi uchungu mahali lakini kipele kisitokee. Kikitokea hivi, huwa vigumu kutambua kuwa ni kipele na kukitibu. Hata hivyo, daktari anaweza kukufanyia uchunguzi wa damu au ngozi iwapo, anashuku kuwa huenda ikawa una vipele.

Matibabu

Hakuna tiba maalum inayojulikana. Hata hivyo unaweza kupunguza muda wa kusambaa na hiyo wapi isiyotuliza, unayokuwa nayo kabla hujativiwa. Ni muhimu utibiwe kwa muda wa siku tatu baada ya dalili kutokea. Mtu hupewa dawa za kuzuia maumivu na ya kuzui kusambaa kwa hivyo vipele.
 
Matibabu Hospitalini

Kuna mambo machache ambayo unatakikana kuyafanya na machache ambayo hutakikani kuyafanya.

  • Nenda kwa kituo cha afya cha umma ama umwone daktari wa kibinafsi aliye mjuzi wa mambo yanayohusiana na ukimwi. Ukishahakikisha kuwa, una muuguzi au daktari unayeweza kumwamini na una uhusiano bora naye, nenda mara kwa mara wakuangalie ili waone vile unavyoendelea kudhibiti maambukizi ya ukimwi.
  • Utahitaji ufanyiwe hesabu ya chembechembe zako za CD4 na wingi wa maambukizi yaliyo mwilini mwako mara mbili kwa mwaka
  • Karibu kila mtu aliye na virusi vya Ukimwi (asili mia 97%) baadaye atapata ugonjwa wa Ukimwi au magonjwa mengine yanayohusishwa na ugonjwa huu. Haya huitwa, magonjwa yanayotumia nafasi hii ya hali iliyoko mwilini kukuangamiza. Karibu magonjwa yote ya aina hii yanaweza kutibika kwa kutumia dawa zilizodhibitishwa.
  • Kwa watu wengi, Ukimwi ni ugonjwa ambao hauwezi kutibiwa hata hivyo, ni hali inayoweza kudhibitiwa kama
  • magonjwa mengine yoyote ya kudumu ambayo hayana tiba. Watabibu wanajua kuna dawa za kudhibiti haya maradhi, (antiretrovirals - ARVs) ya kusaidia watu kuishi maisha ya kawaida na kwa mda mrefu wakiwa na virusi vya ugonjwa huu. Hata hivyo unachohitaji kujua ni kuwa ni muhimu uanze kutumia hizi dawa za ARV za kudhibiti
  • ugonjwa hasa unapo ambukizwa na maambukizi yanayoambatana na magonjwa haya (yanayojulikana kama magonjwa yanayotumia nafasi au hali ya mwili wako ya kuwa umeambukizwa). Ama wakati ambao chembechembe zako za CD4 ni chini 350. Kwa watu wengi walio na virusi vya ukimwi, haya hutokea kwa kati ya miaka 8 – 10 baada ya maambukizi. Hata hivyo kuna hali fulani ambazo hazifuati hali hii.
  • Kuna ushahidi wa kuaminika kuwa ukitumia tembe badala ya vitamini kila siku kidogo unapunguza makali ya ukimwi na haukuporomoshi haraka. Jaribu utumie tembe badala zilizo na vitamini B, C na E. Vituo vya afya vya umma
  • vinafaa kuwapa wagonjwa bure, bila malipo, hizi tembe. Tambua kuwa kuna madai mengi ya uongo kuhusu hizi tembe badala ya vitamini. Haya madai huwa yametiwa chumvi na poroja kali. Haijathibitishwa bado iwapo, mtu anakula virutubishi vyote vya mwili kwa chakula anastahili pia kutumia tembe hizi ili ziwe za manufaa kwake.
 
Back
Top Bottom