Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,268
- 33,040
Idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi nchini Tanzania imeshuka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha mwaka 2008-2009 kwa kulinganisha na mwaka 2007-2008. Wednesday, December 02, 2009 4:49 AM
Idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi nchini Tanzania imeshuka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha mwaka 2008-2009 kulinganisha na kipindi cha mwaka 2007-2008. Kigoma ndio mkoa wenye wagonjwa wachache sana wa ukimwi kuliko mikoa mingine. Imeelezwa kuwa idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi nchini Tanzania imeshuka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha mwaka 2008-2009 kwa kulinganisha na mwaka 2007-2008.
Hayo yamebainishwa katika hotuba mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo nchini Tanzania yalifanyika kitaifa katika mkoa wa Tanga.
Katika taarifa za kitaifa, kiwango cha ukimwi kinatajwa kushuka kutoka asilimia 7.2 mwaka 2008 hadi kufikia asilimia 5.5 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa za kitaifa mkoa wa kigoma ndio unaotajwa kuwa na maambukizi madogo kuliko mikoa mingine nchini Tanzania na kwamba ni asilimia 2.2 ya maambukizi ukilinganishana mikoa ya Iringa, Dar es salaam na Mbeya inayotajwa kuwa na kiwango cha juu cha kati ya asilimia 7 na 12.
Aidha takwimu za mkoa wa Kigoma zinaonesha kuwa wilaya ya Kasulu ambayo ina idadi ya watu wapatao laki saba pamoja na wakimbizi wa DRC na Burundi, ndiyo yenye maambukizi ya chini.
Kwa mujibu wa hotuba ya mkuu wa wilaya ya Kasulu Bi. Zainab Kwikwega aliyoitoa jana katika kijiji cha Kanazi katika maadhimisho ya kiwilaya amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2008, jumla ya wananchi 30,352 wakiwemo wanaume 11,111 na wanawake 19,241 walijitokeza kwa hiari kupimwa Afya zao ambapo Kati ya yao wananchi 413, wakiwemo wanaume 162 na wanawake 251 waligundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi sawa na asilimia 1.3 ya wote waliopimwa.
Akichambua juu ya sababu za kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi, mkuu wa wilaya ya Kasulu Zainab Kwikwega amebainisha kuwa, tabia ya vijana kufanya ngono zisizo salama kabla na baada ya kuoa au kuoelewa ni moja ya vyanzo vikubwa vya kuendelea kuwepo kwa UKIMWI hapa nchini.
Amebainisha kuwa, juhudi zaidi za kutoa elimu zinaendelea kufanyika ili hatimaye kiwango cha maambukizi kiweze kushuka zaidi au kutokomea kabisa na kwamba kila Mtanzania anawajibika kujilinda ili asiambukizwe na aliyeambukizwa asiwaambukize wengine.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3664166&&Cat=1