Ukimwaga ugari tutamwaga mboga

Kitomai

JF-Expert Member
May 21, 2009
1,060
281
Hiyo sauti imesikika ikisemwa na moja ya mafahari wagombanao. Jaribu uone! Thubutu ukione alichokiona mtema kuni! Huyo mwenye pembe ndefu akawaambia'' hakika nitakufukuzeni humu peponi maana nisipofanya hivyo kiama yangu imewadia.Mumechafua hali ya hewa lazima muondoke maana pepo nzima sasa inanuka harufu mbaya.
Na nikisha kuwafukuza nimeandaa mpango maalumu lazima mfikishwe kwa kadhi mkuu mkajieleze ni kwa nini msihukumiwe kwenda Jehanamu kwa kosa la kuchafua hewa peponi.

Mafahari hao wakasema tena: ukitufikisha kwa kadhi tutakuchongea kwake kwani wewe ndiyo uliyotupatia hiyo mikunde.

Fahari mkuu sasa yupo njiapanda anawauliza washauri wake niwafukuze hama nisiwafukuze?
Shinikizo linazidi kutoka kwa raia wa peponi wafukuzwe hao mulika mwizi!
Mkuu wa mafahari kachanganyikiwa ajui cha kufanya saa nyingine anajiuliza sijue nikimbilie ughaibuni?
Msaada wako unahitajika sana maana hivi vita vya mafahari vitaumiza nyasi nyingi sana.
Maana sasa nasikia harufu ya moshi wa gesi moshi wa baruti ninajiuliza maana yake nini hii? Harufu hizo tumezoe kusikia huko katika pepo za ughaibuni. Leo hii hawa mafahari wako mbio kuzileta katika pepo hii washindwe na walegee.
Tunataka amani katika pepo yetu. Hawa mafahari waondoke wenyewe nasema wote wanaotaka kumwaga mboga na hao wanaotaka kumwaga ugari wajivue magamba.
La hawako tayari iwekwe tiba mbadala kama hiyo ilityofanyika katika hizo pepo nyingine kwa migomo na maandamano wakafa mamia pasina hivyo wangekufa ma kumi elfu. Nawasilisha.
 
Utaelewa taratibu jaribu kutakari hiyo ni habari nzito ingewekwa katika lugha ya wazi ingepoteza radha
 
fafanua , ugari ninini? au sawa na kusema upikipiki, ubasi, utrekta?
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Wewe ugari ndo lugha gani?Halafu angalia hii, radha ndo nini wewe?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom