Ukikutwa huna Kondom kwenye First Aid box ya basi faini shs. 20,000

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
Nimeshtushwa na matraffic wa Mbeya leo hii mchana nikiwa safarini kwenda boarder kuwahi usafiri wa Lusaka. Nikiwa katika kiti cha mbele karibu na dereva, basi lilisimamishwa eneo la Tazara Iyunga, na baada ya kukaguliwa mambo yote dereva aliambiwa afungue first aid kit na alipofungua aliulizwa askari wa kike ni kwanini hakuna kondom ndani ya kit hiyo. Ndipo alipoambiwa alipe faini ya sh. 20,000. Alipojitetea sana alikata buku tatu akaachiwa. Nilipomuuliza akasema ni lazima wawe na kondom kwa kila basi, hata zile ziendazo boarder ya Malawi. Hivi hii ni sheria mpya ya usalama barabarani au ni bylaws za huku Mbeya au hawa nyangenyange ndo design ya mlo wao??
 
naunga mkono traffic police ..matumizi y kondomu yanaenda kinyume na maagizo ya muumba wetu kuujaza ulimwengu...
 
Back
Top Bottom