Ukigundua Mke ama Mume wa rafiki yako anacheat utafanyaje?

Ndugu wana jamvi, hii tabia imekuwa ikinikera hata sijui cha kufanya "is kind off" niko kwenye "dilemma". Nina rafiki yangu mpenzi ambaye hivi siku za karibuni nimegundua kuwa wife wake anacheat na sehemu anayofanyia huo mchezo naifahamu. Rohoni najiuliza kumwambia mme wake ndoa yao inaweza vunjika, na itakuwa mm ndiye niliyesababisha kuvunjika kwa kutoa siri hiyo. Lakini naumia sana rohoni maana, utakuta rafiki yangu anakwama kufanya shughuli zake zingine akidhani wife wake yuko kazini na gari kumbe amebana sehemu na jamaa yake. Wakati mwingine ananiomba niende kumpeleka sehemu anayotaka kwenda. of course kwa kuwa ni rafiki yangu naenda huku rohoni naumia nikiwaza kama hivi ingekuwa mm rafiki yangu ananiambia wife wako anacheat sehemu furani ninge react namna gani. Kinachosikitisha huyo mama kila wakati ananilalamikia jinsi mume wake anavyocheat. Najiuliza hivi huwa haoni aibu kulalamika na yeye ndiyo mchezo wake? Naomba ushauri wenu nimwambie????

Je best yako nae katulia (au anecheat vilevile)? Kama nae anecheat kama alivyokulalamikia mke basi piga kimya mazee.
 
Inabidi umkanye mhusika anayefanya cheating aachane na hiyo tabia na si kwenda kuharibu mahusiano kati yake kwa mke/mme wake

FL1, ushauri wako ni mzuri lakini kwa ninavyojua wanawake wa mjini, ukitaka kumkanya kwa issue kama hiyo, atakugeuka na kumwambia mumewe kuwa unamsumbua sana kumtongoza. Je itakuwaje?

Mimi still ambacho ningefanya ni kumpa jamaa ushauri nasaha wa jinsi ya ku handle issue kama hiyo kwa minajili ya kuweza kuendeleza hiyo ndoa, then ningempeleka akaone mwenyewe na uamuzi achukue yeye!!!
 
Ndugu wana jamvi, hii tabia imekuwa ikinikera hata sijui cha kufanya "is kind off" niko kwenye "dilemma". Nina rafiki yangu mpenzi ambaye hivi siku za karibuni nimegundua kuwa wife wake anacheat na sehemu anayofanyia huo mchezo naifahamu.

Mshauri huyu wife wa rafiki yako abadilishe kiwanja na "cheater" wake hili usiwe unawaona ....

BTW: Inaonekana kama na wewe una-spy nyendo za wife wa rafiki yako? Au na wewe ulitaka kugonga shemejiyo akakutolea nje?

Ni maoni yangu tu..

Obuntu
 
mimi nimeshawahi kumwambia jamaa halafu akamwambia mkewe nikaonekana mbea. kumsaidia mchukue mume mpeleke hapo wanapokutana bila kumwambia unafuata nini afumanie mwenyewe
 
mi watu wengine hata siwaelewi......yaani nyie mnaona kuficha madhambi ya uzinzi ni kuokoa ndoa???

poa, mi nikiona wake zenu na wanaume zenu wanagongana huko wala sitawaambia.....lakini mi napenda niambiwe bana. kwa nini niishi kwenye ndoa ya uongo iliyochakachuliwa?
 
mimi nafikiri anfwate huyo cheator wa kiume amwambie ukweli kuhusu kutoka na mke wa rafiki yake,hii ikiwa pamoja na kumtaka aacha mara moja hiyo tabia ama la atamwambia mume wake/rafiki yake.
 
mambo ya ndoa ni magumu,mume ana cheat na mke ana cheat,kwa hiyo wote wana matatizo,hapo wa kusuluhisha ni wao wenyewe,hili suala la ukimwi nina uhakika wao wenyewe wanalijua.kifupi mfahamishe huyo shoga,halafu basi muachie mwenyewe na kisanga chake
 
Hali hiyo haijawakuta. Ngoja itokee then tuone haya majibu kama yata apply. Kumbuka ni mke wa mtu na unapofungua mdomo, huadhiri tu watu 2 bali familia 2, koo 2, etc. Tafuta wanapo sali/swali cheki na padri/shehe wao anayeaminika, mwambie vizuri yeye atawajibika kuweka mambo sawa. We jikaushe kama sio ww vile. You have to take trouble if you really want to help ya friend.
 
Ndugu wana jamvi, hii tabia imekuwa ikinikera hata sijui cha kufanya "is kind off" niko kwenye "dilemma". Nina rafiki yangu mpenzi ambaye hivi siku za karibuni nimegundua kuwa wife wake anacheat na sehemu anayofanyia huo mchezo naifahamu. Rohoni najiuliza kumwambia mme wake ndoa yao inaweza vunjika, na itakuwa mm ndiye niliyesababisha kuvunjika kwa kutoa siri hiyo. Lakini naumia sana rohoni maana, utakuta rafiki yangu anakwama kufanya shughuli zake zingine akidhani wife wake yuko kazini na gari kumbe amebana sehemu na jamaa yake. Wakati mwingine ananiomba niende kumpeleka sehemu anayotaka kwenda. of course kwa kuwa ni rafiki yangu naenda huku rohoni naumia nikiwaza kama hivi ingekuwa mm rafiki yangu ananiambia wife wako anacheat sehemu furani ninge react namna gani. Kinachosikitisha huyo mama kila wakati ananilalamikia jinsi mume wake anavyocheat. Najiuliza hivi huwa haoni aibu kulalamika na yeye ndiyo mchezo wake? Naomba ushauri wenu nimwambie????

Mweleze live. Kama unashindwa, basi tafuta jinsi ya kum-set up ili aende hiyo sehemu mke wake anapochakachuliwa ili akajionee mwenyewe. Ni vema ajue kwani kuna maradhi siku hizi. Na kama kweli unampenda rafiki yako ni bora umjulishe ama fanya vile utaweza ili ajue, then decisio itabaki kwake kama aendelee na mkewe ama abwage manyanga
 
Back
Top Bottom