Ukienda bila kutumia akili unaweza kusema umependwa

fazaa

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,984
1,026
Leo asubuhi nilienda mpeleka mtoto wangu hospital alikuwa na ki homa homa, na dr mmoja wakike kila wakati ananichekea afu anamsifu mtoto wangu wa kume anasema huyu ni handsome kama baba yake.

Cha kushangaza time natoka kwake akawa ananisindikiza mpaa pale kwenye pharmacy anajidai kumsemesha mtoto wangu, lakini pale pale ananisemesha mara sijui nimefanana na mjomba wake, mara sijui namkumbusha sijui cousin yake yuko marekani, ni vutuko vingi tu nyie wacheni.

Afu akawa ana niuliza na watoto wangapi, nikamtajia akasema anatamani watoto hasa kama huyo mtoto wangu.

Nikamuliza umeolewa? akasema bado nikasema ooo very soon utaolewa mungu akipenda, akafurahi sana na huku akisema isije kuwa wewe tu ndo unakuja nioa, afu akacheka.

Nikachukua dawa zangu, afu na yeye akaniaga akasema it was nice to see you, afu akaendelea kusema; I just hope we will meet some other time...nikasema sure.

Sasa cha ksuhangaza mpaa mdaa huu najiuliza hivi itakuwaje mtu mkutana naye siku moja tu avutiwe na wewe namna hio, je nyie wanawake ndo zenu hizo mnapenda kwa kasi au ndo alikuwa anachemsha tu huyo babe.

Sasa swali nalo jiuliza, hivi wanagapi wanaume wanaweza kusema wameisha pendwa hapo? na wanagapi wanawake wanaweza kusema yule dr wakike kisha nipenda, na wangapi wanaweza kusema kama mimi; Ukienda bila kutumia akili, unaweza kusema umependwa.
 
Upendo wa siku moja? Tena kwa mtu mwenye familia? Mhhh, sina jibu. Labda alikufanyia usanii au alitaka kupima uaminifu wako na familia yako! Au anafahamina na mkeo na alijaribu walishawahi kudiscuss kukutega! Kwa kweli ni ngumu kujua ...
 
Labda damu yake ilikupenda...! Usikute ajawahi kumshobokea mwanaume hata siku moja, labda siku hiyo ndio akajaribu labda bahati inaweza kuwa yake.! sio kila ukitokewa basi ujue ndio tabia ya mtu siku zote.
Labda katika fikra zake alikuwa anapenda mwanaume wa jinsi ulivyo ww.
 
Upendo wa siku moja? Tena kwa mtu mwenye familia? Mhhh, sina jibu. Labda alikufanyia usanii au alitaka kupima uaminifu wako na familia yako! Au anafahamina na mkeo na alijaribu walishawahi kudiscuss kukutega! Kwa kweli ni ngumu kujua ...
Aisay inawezekana kabisa.
 
Huwa inatokea waswahili husema damu kumatch!
Ila usikute alikuwa na minyege kiloba!
Vip ulimpa namba yako ya simu?Maana usikute aliomba
 
umeshindwaje kumfanyia kazi huyo mdada bwana ? bahati haiji mara mbili fazaa.
 
Hayo ni masihara 2 mkuu, mi ninavyofahamu iwapo mwanamke amevutiwa/kumpenda mwanaume hawezi kumshobokea ki-hivo ataishia kuwasimulia wenzie sifa zako 2.

Hiyo ni sehemu ya huduma kwa wateja(customer care).
 
Hujawahi penda at first sight? Kama hujawahi, you won't understand.
Haina cha unajiheshimu kama mama paroko au kicheche cha makaburini.

Tunachotofautiana ni uwezo wa kusema hisia kwa muda huo huo kwa mtu usiyemfahamu kabisa.
Na kana hauko smart unaweza jikuta umefanya kituko bila hata kujua umefanya nini.

Simaanishi huyo dada alikupenda kiukweli maana kila fani ina mamluki, inawezekana ulikuwa unatikisa funguo za gari.
Si unajua gari ni sumaki kwa baadhi ya akina dada.
 
Watu wengine mna mambo. . .
Mtu akikuchekea ananitaka, akikutania basi anakupenda.

Huwezi ichukulia hiyo hali kama ilivyokua?Kwamba kakuchangamkia na kukutania tu basi bila ya kuanza kutafsiri mambo vile unavyoona inakupendeza/kupa sifa zaidi?
 
Huwa inatokea waswahili husema damu kumatch!
Ila usikute alikuwa na minyege kiloba!
Vip ulimpa namba yako ya simu?Maana usikute aliomba
Hakuomba wala hatujaongelea mambo ya simu kabisa :cool2:
 
Leo asubuhi nilienda mpeleka mtoto wangu hospital alikuwa na ki homa homa, na dr mmoja wakike kila wakati ananichekea afu anamsifu mtoto wangu wa kume anasema huyu ni handsome kama baba yake.

Cha kushangaza time natoka kwake akawa ananisindikiza mpaa pale kwenye pharmacy anajidai kumsemesha mtoto wangu, lakini pale pale ananisemesha mara sijui nimefanana na mjomba wake, mara sijui namkumbusha sijui cousin yake yuko marekani, ni vutuko vingi tu nyie wacheni.

Afu akawa ana niuliza na watoto wangapi, nikamtajia akasema anatamani watoto hasa kama huyo mtoto wangu.

Nikamuliza umeolewa? akasema bado nikasema ooo very soon utaolewa mungu akipenda, akafurahi sana na huku akisema isije kuwa wewe tu ndo unakuja nioa, afu akacheka.

Nikachukua dawa zangu, afu na yeye akaniaga akasema it was nice to see you, afu akaendelea kusema; I just hope we will meet some other time...nikasema sure.

Sasa cha ksuhangaza mpaa mdaa huu najiuliza hivi itakuwaje mtu mkutana naye siku moja tu avutiwe na wewe namna hio, je nyie wanawake ndo zenu hizo mnapenda kwa kasi au ndo alikuwa anachemsha tu huyo babe.

Sasa swali nalo jiuliza, hivi wanagapi wanaume wanaweza kusema wameisha pendwa hapo? na wanagapi wanawake wanaweza kusema yule dr wakike kisha nipenda, na wangapi wanaweza kusema kama mimi; Ukienda bila kutumia akili, unaweza kusema umependwa.

A fiction story!
 
Hayo ni masihara 2 mkuu, mi ninavyofahamu iwapo mwanamke amevutiwa/kumpenda mwanaume hawezi kumshobokea ki-hivo ataishia kuwasimulia wenzie sifa zako 2.

Hiyo ni sehemu ya huduma kwa wateja(customer care).
Nice point, ndo siku zote huwa naogopa kudhania kabla kuhakikisha :cool2:
 
Hakuna cha ajabu hapo,huyo daktari ni ana mazoea ya kuchangamkia watu tu,usije ukajipa bichwa eti umeshobokewa wala nin.Mbona mie inanitokea sana hyo na nnawapotezea tu!
 
mkuu hilo duka la dawa uliloenda kununua dawa ambapo na yeye alikusindikiza halikuwa lake kweli? isije bashasha zake ilikuwa ni katika mipango ya kukuvuta ukanunue dawa kwenye duka lake tu.... si unajua tena biashara??? lazima uwe mchangamfu... maana mteja ni mfalme
 
Sasa kama nachekewa mara moja baada ya miongo 2, si lazima nijidai japo kidogo?
Kuna mambo magumu kuyapata jamani, hasa umri ukiienda.

Back
Top Bottom