Ukata wageuza walimu kuwa wakulima

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
UPUNGUFU wa mishahara na maslahi madogo kwa walimu, vimeelezwa kuwa ndio chanzo cha walimu hao kujihusisha na kilimo katika maeneo yao ya kazi na kuitelekeza taaluma yao.

Hayo yalisemwa juzi na Katibu wa Chama cha Walimu (CWT), Mkoa wa Shinyaga, Martini Samara, wakati wa uchaguzi mkuu wa chama hicho katika ngazi ya Wilaya ya Bukombe.

Samara alisema maslahi madogo wanayopata walimu yamechangia kushuka kwa elimu kila mwaka hali ambayo inahatarisha nchi kukosa wasomi.

Alisema kwa sasa baadhi ya walimu wamekuwa wakijihusisha na kilimo katika maeneo yao ya kazi, badala ya kufundisha na kusababisha wanafunzi wengi kufeli katika mitihani yao ya mwisho.

“Kama unamlipa mwalimu mshahara mdogo, unafikiri anaweza kufundisha darasani? Hata ukimsimamia, ukiwa na Ofisa Elimu na Mkurugenzi, anaweza kufundisha masomo ambayo yamekwishapita,” alisema Katibu huyo.

Alisema mwalimu akigoma, askari hawezi kufanya kazi ya kufundisha darasani tofauti na madaktari ambao wanaweza kugoma, na wakachukuliwa wengine kwenda kufanya kazi hiyo.

Alidai kuwa walimu wamekuwa wakidharaulika hadi kinapofikia kipindi cha uchaguzi ndipo Serikali inapowakumbuka na kuwalipa malimbikizo ya madai yao ya nyuma.
 
Ukata si unawageuza walimu wakulima tu ila hata walevi na watoro kazini. Mshahara wa mwalimu wa ni mdogo kushinda hata wa kibarua anayebangaiza mchana tu usiku analala. Bora hata hao wenye maeneo ya kulima watakuwa wamejipatia kipato halali kupitia njia halali. Je kwa wale ambao hawana maeneo ya kulima watajiongezea kipato kwa njia gani? Kwa nini asichanganyikiwe akalewa gongo baada ya kuona mahitaji yake ya nyumbani hayatimii kwa kuwa kamshahara ni kadogo kuliko kazi anayofanya?

Waalimu wanatakiwa kuwa wa kwanza kuunga mkono mgomo wa wafanyakazi unaoandaliwa mwezi Mei ili kuishtua serikali kufikiria upya maslahi yao. Tatizo la waalimu ni nidhamu ya woga katika kudai maslahi. Woga ni tatizo kubwa kwa kuwa wanatishiwa nyau nao wanaogapa. MAdaktari waligoma wakatishiwa kufukuzwa kazi, serikali ikaasumbua kidogo ila baada ya kuona mambo ni magumu ilisalimu amri na mshahra wa kuanzia kwa daktari wa shahada si chini ya laki sita wkati mwalimu mwenye digrii ni chini ya laki nne. Walimu jipangeni kudai maslahi bora kwani ninyi ni chanzo cha maarifa na mwongozo wa viongozi wanaowanyima haki zenu sasa. Walimu waache woga hii ni vita na katika vita ni lazima kuna kujitoa muhanga
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom