Ukali wa Nyerere, Upole wa Mwinyi, Ubabe wa Mkapa na...

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
"Rais Mwinyi ni mtu mwema na mpole, lakini ni kiongozi dhaifu; na upole wake na udhaifu wake unatumiwa na watu ambao wala si wema wala wapole kuhatarisha umoja na amani ya nchi yetu" - Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania, Uk. 50-51

"Wengi wanamfahamu Mkapa kama kiongozi aliyekuwa mbabe, asiyekuwa na subira, ilikuwa ni rahisi sana kwake kufoka, kukemea na hata kutumia lugha mbaya dhidi ya wale wenye msimamo tofauti na wa kwake" - Fikra Yakinifu, http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/10/24/makala8.php

"Sina kawaida ya kulizwa na mambo ya siasa, lakini katika kikao chicho nilishindwa kujizuia kulia. Sikupata maelezo ya maana ya kuwafanya watu wazima wafanye walivyofanya ... Huu ni uongozi wa ajabu kabisa!" - Mwalimu Nyerere, Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania, Uk. 20
 
Nawakumbuka katika hotuba hizi...

Rais Nyerere: Hawa ni wahuni tu hawafai kuongoza nchi... (akimaanisha Kolimba Malecela...na Genge la Wabunge 55 )

Rais Mwinyi: Ukitaka kula panya rhuksa... (baada ya vurugu za kuvunjwa kwa maduka yanayouza nyama ya nguruwe!

Rais Mkapa: Mimi sijali rangi ya paka najali kama anakamata panya au la...! (Mei Mosi akinukuu methali ya kichina akitetea Network Solution na alipokataa kulinda ajira za wazalendo dhidi ya waajiriwa kutoka nje)

Rais Kikwete: Isijekuwa tukalaumina mbele ya safari... (Hutoba yake ya kwanza kama Rais akionya mafisadi) Ni kwa kiwango gani anatimiza hili?
 
Nawakumbuka katika hotuba hizi...

Rais Nyerere: Hawa ni wahuni tu hawafai kuongoza nchi... (akimaanisha Kolimba Malecela...na Genge la Wabunge 55 )

Rais Mwinyi: Ukitakula panya rhuksa... (baada ya vurugu za kuvunjwa maduka ya wanaouza nyama ya nguruwe!

Rais Mkapa: Mimi sijali rangi ya paka najali kama anakamata panya au la...! (Mei Mosi akinukuu methali ya kichina alipokataa kulinda ajira za wazalendo dhidi ya waajiriwa kutoka nje)

Rais Kikwete: Isijekuwa tukalaumina mbele ya safari... (Hutoba yake ya kwanza kama Rais akionya mafisadi) Ni kwa kiwango gani anatimiza hili?
hapa alikuwa akiwatahadharisha wadanganyiika kuwa wasije kumlaumu manake washkaji wake ndio wameshika mpini na hawezi kuwasaliti
 
Ukali wa Nyerere, Upole wa Mwinyi, Ubabe wa Mkapa na... UCHESHI WA JK na ........wa watanzania
 
Ni kweli twaweza kumuelezea Nyerere kama kiongozi aliyekuwa mkali, thabiti/serious, aliyemaanisha alichokisema na pia mcheshi.

Mwinyi ...mpole, mtu wa watu.

Mkapa...mbabe, asiyeshaulika, muumini wa wazungu na mdharau wa watu weusi

Kikwete...Kiogozi dhaifu, asiye na vision, mcheshi, nonserious, mtu wa watu, asiye na uwezo wa kufanya mamuuzi mazito, mtafutaji wa simple popularity kutoka kwa wananchi wake.
 
Back
Top Bottom