Ukabila UDSM?

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,526
19,381
Nimesoma kwa masikitiko sana pale Dr. Lwaitama alipoelezea msimamo wa UDASA kuhusu mgogoro wa kisiasa uliopo Kenya hivi sasa na kugusia wasiwasi wake kuhusu kuanza kwa vyama vyenye mlengo wa ukabila pale UDSM.

"Katika hili, sisi pia tunasikitishwa na tabia za ukabila hasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia vyama vya wanafunzi vya kikabila, tunawashauri wanafunzi kuanzisha vyama vyenye sura ya kitaifa na kizalendo, vyuo vikuu vinatakiwa kuwa vituo mkakati vya mapambano dhidi ya ukabila, ubeberu na ufisadi, visiwe makambi ya maovu hayo," alisisitiza Dk Lwaitama

Kwa maoni yangu, nadhani kuwa tabia hii ya ukabila ilianza wakati wa utawala wa awamu ya pili ambapo mikutano ilikuwa inaitishwa na watu wa kutoka eneo fulani la nchi ili kuchangia maendeleo ya eneo lao. Juzi juzi kulikuwa na mkutano wa aina hiyo uliofanywa na watu wa Kagera. Inawezekana tatizo la Ukabila likatukumba na sisi baada ya muda si mrefu endapo hatutakuwa makini. Mwanzo wa Ngoma ni lele
 
Nimesoma kwa masikitiko sana pale Dr. Lwaitama alipoelezea msimamo wa UDASA kuhusu mgogoro wa kisiasa uliopo Kenya hivi sasa na kugusia wasiwasi wake kuhusu kuanza kwa vyama vyenye mlengo wa ukabila pale UDSM.



Kwa maoni yangu, nadhani kuwa tabia hii ya ukabila ilianza wakati wa utawala wa awamu ya pili ambapo mikutano ilikuwa inaitishwa na watu wa kutoka eneo fulani la nchi ili kuchangia maendeleo ya eneo lao. Juzi juzi kulikuwa na mkutano wa aina hiyo uliofanywa na watu wa Kagera. Inawezekana tatizo la Ukabila likatukumba na sisi baada ya muda si mrefu endapo hatutakuwa makini. Mwanzo wa Ngoma ni lele

Kichuguu:

Usiwe na wasiwasi mkubwa wa kikabila Tanzania. Dawa ya ukabila sio kuufuta au kufanya jitihada za kikabila zisiwepo.

Sera kubwa katika awamu ya pili ilikuwa ni kuruhusu watu kufanya jitihada za maendeleo katika maeneo ya bila kutegemea sana serikali.

Maeneo mengi ya Kagera ni ya wahaya. Na hawa watu wakitaka kufanya shughuli zao wenyewe ni lazima uhaya utaonekana. Lakini uhaya wao sio wa nia mbaya. Ni wa kutaka kushughulikia maeneo yao.

Chama cha kwanza cha ushirika barani Afrika kilianzishwa Kilimanjaro. Na sehemu kubwa ya waanzilishi walikuwa ni wachagga. Na ulikuwa ni mfano kwa watu wa mikoa mingine. Na tulipoviunganisha shughuli za vyama hivi katika mamlaka za mazao. Matokeo yake yalikuwa mabaya kwa taifa zima.

Niliishi Mwanza kwa muda mrefu. Watu wa mkoa wa Mwanza kwa kuona kuwa serikali haijengi shule za sekondari walihamua kujenga shule zao (Shule za sekondari za wakulima). Na shule ya kwanza ilikuwa mjini Geita na walikuwa wanataka kila wilaya kuwa shule. Lakini kwa kuwa serikali ya awamu ya kwanza ilikuwa na mikakati ya shule serikali ambazo hazikuwa za kikabila au kimikoa ilichelewesha kutoa kibali cha shule za wakulima. Matokeo yake ilikuwa ni kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

Kwa maoni yangu. Watanzania mna makabila yenu. Hamkuchagua kuzaliwa na makabila haya na hamna sababu ya kutojivunia makabila yenu au kusaidia sehemu mlizotoka. Cha muhimu kukumbuka ni kuwa mtu wa kabila jingine ana haki sawa na wa kabila lako na mpe heshima zake.
 
Shilingi haikosi pande mbili, na majambo yote vivyo. Katika makala nyingine nilizokwisha andika katika ukumbi wetu huu maarufu, nimezungumzia sana mustakabali wa umuhimu wa kabila na ukabila na kwa muhtasari athari za ukabila. Naomba hapa nipewe nafasi ya kulirejea somo hili.

Kabila ni kikundi cha watu wachache ndani ya Taifa letu. Kabila, nilisema, ni kikundi cha watu wenye koo zinazohusiana, mara nyingi kwa damu au ujirani mwema wa karne nyingi. haivi ni vikundi ndani ya Taifa kama vikundi vingine. Kwa mfano, CCM ni kikundi ndani ya Taifa, hali kadhalika Young Africans au Simba Sports Club ni vikundi ndani ya Taifa. Vikundi vyote vinawajibu wa kushirikiana na vikundi vingine ndani ya Taifa, ili kudumisha amani na mshikamano. Kama vile pia vikundi vya UTAIFA vinavyohitaji kushirikiana kudumisha amani na mshikamano duniani.

Kusema tu ukabila utatuletea mashaka nchini, hakutoshi. Kwa sababu, hata uccm au uyanga na usimba unaweza kuleta mashaka. Sawa na utanga au umorogoro na udaressalaam.

Ukabila, unaweza kutumiwa vizuri ukawa na manufaa ya kujiendeleza wenyewe kwa kushirikiana ama na serikali kujiletea maendeleo katika mkoa wao au hata katika tarafa yao. Kama vile usimba na uyanga unaweza kutuletea maendeleo katika eneo la michezo.

Kama mtu anavyoipendelea familia yake, ndivyo hivyo hivyo anavyoupendelea, ukoo ukabila, uchama au utaifa wake. Wacha ukabila hata utaifa au uccm ukitumiwa vibaya unaweza kusababisha madhara kwa namna ile ile ya ukabila. Hakuna ubaya wowote kama ukabila unatumika kwa manufaa ya ummah. Ukabila hauwezi kuondoka au kuondolewa. Huu ni uhusiano wa watu kwa damu.

Kabila kwa watu wengi ni ya upande wa baba na ikiwa mama ni wa kabila jingine, huko ni ujombani. Mara nyingi huwezi kumwambia mtoto akawadhuru wajomba wake. Hii nayo ni njia nzuri ya kuleta uhusiano mzuri kati ya makabila. Ndio maana pia unapatikana utani kati ya makabila. Utani nao mara nyingine hutumika katika makabila kusaidiana na kuleta maendeleo katika mizizi ya Taifa.
 
Mikutano na vyama vya kikabila huwa inajenga kuta pale ambapo serikali kuu haina ajenda inayoeleweka kwa wananchi wake. Binafsi nadhani vyama hivyo ni sehemu tu ya tatizo. Tatizo lenyewe ni kukosekana kwa mwelekeo wa pamoja ambao unajengwa na ajenda za kitaifa zinazoongozwa na utaifa. Kukosekana huko kwa ajenda ndiko kunakopelekea kila mtu au kikundi cha watu kujikusanya na kuanza 'kujisaidia'. Si dalili nzuri, kwani aanzaye kwa uruzi mwisho huimba.
 
Kichuguu, hili alilosema Lwaitama tumelipigia kelele miaka mingi sana. Mimi pia siamini kwamba tunahitaji mikutano ya aina ile. Mle ndo kunapikwa kasumba ya nepotism. Fikiria mtu aliyepata kazi kwa kuunganishwa na mkubwa fulani waliyemwalika kwenye kamkutano kao kaukabila, akienda kwenye shirika huko yeye atatumia kigezo gani zaidi ya jicho hilo hilo la mtu wa kwao kama ndiyo njia aliyepitia. Ndiyo maana basi siku hizi imekuwa ni kawaida kusikia vijana wakisema kwamba huwezi kupata kazi mpaka uwe na mtu unayemfahamu sehemu fulani. Yaani watu wanahangaika kutafuta watu wa kuwaunganishia wapate kazi badala ya kunoa CV zao sawasawa
 
Labda sasa malengo yamebadilika lakini nakumbuka wengine tulivyokuwa tunasoma pia kulikuwa na mikutano ya kimkoa au kikanda ambayo lengo lake hasa lilikuwa kutafuta njia za kusaidia huko tulikokuwa tunatoka.

Kwa mfano kuna kipindi kulikuwa na uhaba mkubwa walimu kwa baadhi ya shule za secondary. Wanafunzi ambao walikuwa hawaendi practical, walikuwa wanaombwa wakajitolee kufundisha hizo shule kwa malipo kidogo.

Binafsi sioni tatizo kabisa kama lengo ni kujadili mambo ya huko wanakotoka.
 
Ukiangalia kwa jujuu, inaonekana mikutano/vyama hivyo vina nia njema, lakini vikiendelea muda mrefu na kuzidi kusimika mizizi, vina elekeza huko huko katika ukabila na kusaidia mtu wa kwenu kwanza kuliko mwingine ama kujitenga kwa njia moja ama nyingine katika kufanya urafiki na shughuli nyinginezo!!

Kinacho tusaidiia sana watanzania, ni kuoleana, na pia dini hutuweka pamoja watu wa makabila tofauti na kutufanya tuonane wote ndugu katika allah!
 
Kichuguu,

Mimi binafsi bado sijaona tatizo kwenye hiyo mikutano. Wakati nikiwa mlimani Tena nilikua Katibu wa mojawapo ya chama kimojawapo malengo yake yalikua kama ifuatavyo.
1. Kusaidiana wakati shida na Raha
2. Kusaidia kule tulikotoka: hapa tulikua na legho mahususi. kuongeza idadi ya wataojiunga chuo kikuu kwa kufanya yafuatayo
a. kutoa madesa(vitabu, pamphlets.n.k) kwa shule za sekondari zilizopo maeneo husika.

b. Wote wanaosomea ualimu kuzipa priority shule zilipo maeneo husika na tulitoa motisha kwa wote wataoenda kufundisha regardless kule anatoka yaani sio lazima anayetaka kufundisha awe ametoka morogoro ndio afundishe shule za morogoro bali yeyote atakaenda kufundisha shule za morogoro basi tulimpatia motish sawa na wale waliotoka morogoro japo ulikua kidogo.

c. Kutoa seminara za Ukimwi mashuleni na kuwapa vijana Moyo na mbinu mbali mbali za kusoma ili kufaulu.


Hayo ndio malengo makuu tuliyokuwa nayo wakati huo. sasa sijui kama yamebadilika na Tulipofanya seminar kwenye shule za sekondari pamoja na kupeleka baadhi ya madesa. Najua vyama 6 vilivyoiga huo utamaduni.

Ndugu Kichuguu, pia kuna mkoa fulani ulikua na vyama zaidi 5 na walisema sababu ni kwamba wako wengi hata Nkurumah haitoshi kama wakikaa pamoja so wakagawanyika kutokana na sehemu walizotoka (wilaya na tarafa)ingawa hawa wote ni kibila Moja.

Kuna mikoa mingine walikua wachache so walikua wanakutaka kama mkoa na ujue mkoa una kabila zaidi ya moja. Ssasa huo ukabila unatoka wapi?
 
Bowbow - hao walijigawa vikundi vitano ni hatari!

Ufahamu wangu ni kwamba hakuna mkoa (Tanzania Bara)ulio na kabila moja. Ukienda Kagera; na hasa Bukoba mjini utawakuta hata watu kutoka Mtwara wapo, na siajabu kuna watoto wao pia walioko Chuo Kikuu Dar. Kama hii mikutano sio ya watu wa kabila fulani, na kama misingi yake ni ya kuleta maendeleo kwa jamii yote iliyopo katika mkoa huo, hapo itakuwa vigumu kuilalamikia mikutano/mikusanyiko ya namna hii, na hata lugha inayotumika ikiwa ni lugha yetu ya taifa, bila ya kumbagua mtu.

Hatari kubwa ni hapo vyama hivi vinapoanza kuwabagua watu kwa misingi ya makabila yao; hata kule kwa kuendesha mikutano katika lugha za kikabila.

Kupeana kazi kwa kujuana kikabila, mmmmmh, ni hatari; lakini ni nani asiyejua hata huko majuu, anayeanza kupata connection ni mwenye contacts? Njia bora ya kupunguza upendeleo wa namna hii ni kuwa na utaratibu mahsusi wa sifa zinazotakiwa kwa kazi inayotaka kujazwa, na pawepo uwazi wa kuitangaza ili kila anayetafuta awe na nafasi ya kujua kuwa kazi inatangazwa.
 
Kalam suala la kazi
ni kitu kingine. Nikuulize najua haupo Tanzania kwa sasa, Je nani aliyekupa mchongo wa hapo Ulipo?

inawezekana ni rafiki yako uliyekutana nae shule(chuo, secondari n.k), Inawezekana ni ndugu yako alipata mchongo mahali kaukrushia ama employer wako

Je kama hukufahamiana nae leo ungekuwa hapo? Ninaochotaka sema ni kwamba kufahamiana na kupeana kazi, michongo yeyote haina uhusiano na hivi vyama zaidi ya social networking.

Wachaga waliokua mlimani walikua na vyama vingi warombo, marangu, Same, wauru, wakibosho, wasiha, waoldmoshi n.k Je hawa wote sio wachaga?

Nilikua na rafiki yangu wa kichaga na niliwahi kwenda kwenye kikao chao siku moja sikuwahi kusikia wanaongea kilugha (anyway siwezi kuwasemea)lakini kama ndio lugha wanaweza kuwasiliana kwa karibu mimi sioni taabu as long as kama hawadharau vyama vingine kwa misingi ya kabila ama kule watokako.

Vyama hivi vyote viko registred chini ya ofisi ya Dean of Student na katiba zao nakumbuka zilikuwa lazima zipelekwe kwake, hivyo kama vilikua na malengo tofauti nadhani vingekuwa vimefutwa.

So social networking inafanyika popote, kwa njia nyingi na kwa maoni yangu Vyama hivi ni moja wapo ya social networkng, ikiwa ni pamoja na kutafuta wachumba sio kazi tu.
Ndio maana kila association ilikuwa inafanya party na kualika general public ili kwa wale wanaotaka kuongeza sample size yao ya kuchagua mchumba wapate nafasi.

Usifikirie ukabilaaaa tuuuuuuuuuu, kutafutiana kazi tuuuuuuu, yapo mengi mazuri kwenye vyama hivi

Naomba kunyamaza na wengine wachangie
 
Bowbow:
Katika jambo hili tunakubaliana kwa sehemu kubwa. Nisipokubaliana na wewe ni kama hivyo vyama vitano (5) vya hao wanafunzi waliotokea katika mkoa mmoja vilikuwa katika misingi ya ukabila au (kama ulivyoainisha hapo juu, urombo, umachame, umarangu n.k., na kuwatenga wengineo wasiokuwa wa u....huo. Social networking ni jambo la kawaida na wala halihusiani kabisa na ukabila; in fact ninadiriki kusema ni kinyume kabisa na ukabila. Mtu kama unaconnect na watu vizuri unataka ukabila wa nini.

Mimi nipo hapa hapa Bongo yetu ninadunda bila wasiwasi na washikaji wenzangu wote waTanzania. Sina nafasi ya uvumilivu kabisa na mambo ya ukabila.
 
Bowbow - hao walijigawa vikundi vitano ni hatari!

Ufahamu wangu ni kwamba hakuna mkoa (Tanzania Bara)ulio na kabila moja. Ukienda Kagera; na hasa Bukoba mjini utawakuta hata watu kutoka Mtwara wapo, na siajabu kuna watoto wao pia walioko Chuo Kikuu Dar. Kama hii mikutano sio ya watu wa kabila fulani, na kama misingi yake ni ya kuleta maendeleo kwa jamii yote iliyopo katika mkoa huo, hapo itakuwa vigumu kuilalamikia mikutano/mikusanyiko ya namna hii, na hata lugha inayotumika ikiwa ni lugha yetu ya taifa, bila ya kumbagua mtu.

Hatari kubwa ni hapo vyama hivi vinapoanza kuwabagua watu kwa misingi ya makabila yao; hata kule kwa kuendesha mikutano katika lugha za kikabila.

Kupeana kazi kwa kujuana kikabila, mmmmmh, ni hatari; lakini ni nani asiyejua hata huko majuu, anayeanza kupata connection ni mwenye contacts? Njia bora ya kupunguza upendeleo wa namna hii ni kuwa na utaratibu mahsusi wa sifa zinazotakiwa kwa kazi inayotaka kujazwa, na pawepo uwazi wa kuitangaza ili kila anayetafuta awe na nafasi ya kujua kuwa kazi inatangazwa.

Kalamu, heshima mbele.
Naunga mkono maoni yako kwamba kwa Tanzania ya sasa hakuna mkoa wowote wenye kabila moja, kwani tumechanganyikana sana, tumeoleana sana, nk. Na hii inatokana na sera za taifa tangu zamanai, kwamba mtu anaweza kufanya kazi popote katika jamhuri hii bila mipaka ya kikabila. Matokeo yake ndio hayo unakuta mtu kwa kabila ni Mgogo (wazazi wake), lakini alizaliwa Mtwara na wala hata kigogo hajui kabisa. Mtu anazaliwa Tukuyu, lakini wazazi wake ni Waha, hata Kiha hajui, anajua Kinyakyusa tu. Nakumbuka pia nikiwa Udsm, tulikuwa tunaitisha na kuwezesha mikutano hii ambayo Dk Lwaitama anasema ni ya 'Kikabila'. Hatukuwa tunasema watu wa kabila fulani tutakuwa na mkutano mahali fulani, hapana! Tulikuwa tunasema kwamba, watu kutoka eneo fulani, iwe wilaya ama mkoa, tukutane siku fulani kwa ajili ya kujadili maendeleo ya eneo letu (kwani Tanzania hailingani kimaendeleo). Hapa tulikuwa tunapata watu kutoka makabila mbali mbali ambao wanatokea eneo husika na mikutano yote ilifanyika kwa Kiswahili. Sasa hapa ukabila uko wapi? Unakuta mtu kwa kabila ni Mhaya, lakini kakulia Rufiji, sasa ukisema uite mkutano wa Wahaya sidhani kama jamaa yangu huyu atahudhuria.
Labda pointi murua hapa ya kujadili ni 'ujimbo' ama 'Ueneo'. Napinga ukabila katika suala hili, haupo!
 
Nadhani hoja ya Lwaitama ni ya msingi kabisa. Maana nakumbuka zamani pale UDSM vyama vilikuwa mainly vya kimkoa mfano TAUSA, UWAMBE, DUSA, KAUSA n.k lakini miaka ilivyozidi mambo yalibadilika kabisa maana vikaanza kuwa vya kiwilaya, mara vya tarafa. Utasikia Vunjo juu uni students association, sijui Karagwe south uni std assoc. na huko siriaz ni ukabila tu maana huyo wa vunjo chini akionekana kwenye kikao cha vunjo juu, japo hakataliwi lakini anakuwa haaminiki na si rahisi akawa recognised katika same level. Nakumbuka those days nadhani ilikuwa 97 (enzi za ujana) tulialikwa kwenye sherehe ya jamaa wa karagwe na rafiki yetu wa huko mambo yalikuwa ni vioja maana hata kiswahili kilikuwa hakitumiki, halafu bia ni mpaka ujulikane huko karagwe ni kjj gani unatoka.

Kwa kifupi ni kwamba vyama vile vingi vinalenga kusaidiana lakini within boundaries ambazo ni za kikabila. Mimi binafsi nadhani vyama vilke vya kitaaluma ni muhimu zaidi na vinaweza kuleta changes accross the republic kuliko hivi vya KIKABILA
 
Nadhani hoja ya Lwaitama ni ya msingi kabisa. Maana nakumbuka zamani pale UDSM vyama vilikuwa mainly vya kimkoa mfano TAUSA, UWAMBE, DUSA, KAUSA n.k lakini miaka ilivyozidi mambo yalibadilika kabisa maana vikaanza kuwa vya kiwilaya, mara vya tarafa. Utasikia Vunjo juu uni students association, sijui Karagwe south uni std assoc. na huko siriaz ni ukabila tu maana huyo wa vunjo chini akionekana kwenye kikao cha vunjo juu, japo hakataliwi lakini anakuwa haaminiki na si rahisi akawa recognised katika same level. Nakumbuka those days nadhani ilikuwa 97 (enzi za ujana) tulialikwa kwenye sherehe ya jamaa wa karagwe na rafiki yetu wa huko mambo yalikuwa ni vioja maana hata kiswahili kilikuwa hakitumiki, halafu bia ni mpaka ujulikane huko karagwe ni kjj gani unatoka.

Kwa kifupi ni kwamba vyama vile vingi vinalenga kusaidiana lakini within boundaries ambazo ni za kikabila. Mimi binafsi nadhani vyama vilke vya kitaaluma ni muhimu zaidi na vinaweza kuleta changes accross the republic kuliko hivi vya KIKABILA


Sula la kugawanyika kutoka mikao tu wilaya au tarafa ni kama nilivyosema kuna baadhi ya mikoa imekuwa na wanachuo wengi so wakagawana kiwilaya then tarafa(kwa mikoa yenye watu wengi)
ila nakumbuka Mkoa wa pwani haukuwa na hicho chama sijui kwa nini.

So kama vyama hivi vimeadilika na kuwa kwa basis ya kabila kuna sababu ya kuvipigia kelele ila kama bado ni social networking na kusaidia maendeleo ya maeneo yao walikotoka Dr. Lyaitama must be wrong.

Lakini bado naamini
 
Ukabila ni nini basi? Je ukienda Mtwara na ukaona katika ofisi mojawapo kuna wamakonde au wamakua wengi wameajiriwa tunaweza kusema kuna ukabila hapo? Vipi ukienda Kagera na kwenye ofisi za serikali ukakuta wahaya wengi wameajiriwa hapo tunaweza kusema kuna ukabila? Je ukienda Mbeya au mkoa mwingine wowote ule na ukakuta watu wa makabila ya huko wameajiriwa wengi zaidi kuliko watu wa mikoa mingine tunaweza kusema kuna ukabila?

Binafsi kama nilivyochangia kwenye ila mada ya "Ukabila" bado naamini kuwa kuna vipimo vya ukabila na wingi wa watu wa kabila moja mahali fulani siyo ukabila. Na hapa nina maana hata ukiwakuta wangoni wamerungikana mtaa mmoja kule Magomeni Tanga, au ukiwakuta wachagga wamenunua maduka karibu karibu kuzunguka soko la ngamiani haina maana kuna ukabila.

Binafsi naamini kuwa ukabila ni hisia na mwelekeo wa mtu au kikundi cha watu kutukuza ukuu wa kabila lao huku wakiyaona na kuyafanya duni makabila mengine. Ni hisia ya kutaka watu wa kabila la mhusika kufanikiwa na wengine "lwao". Hisia hii ya kikabila hujionesha hasa pale ambapo mtu yuko tayari kufanya jitihada za kuangamiza makabila mengine ili kabila lake lifanikiwe. Hisia hii iko sawa na hisia ya watu wanaotukuza nasaba za rangi, utaifa, n.k Ni hisia ya kibaguzi na msingi wake ni kujiona bora zaidi kuliko watu wengine kwa sababu ya mtu kuwa ndani ya kabila lile.

Sasa utaona kuwa kuna watu wanazo hisia hizo. Nimewahi kukutana na mtu ambaye aliyeniambia kuwa "kabila letu ndio wasomi zaidi Tanzania kwa sababu mungu ametujalia akili zaidi". Sasa utaona kuwa sehemu ya kwanza ya kauli hiyo inaweza kuwa kweli, lakini sababu ya ukweli huo (Mungu ametupendelea) ina hisia za kibaguzi!

Sasa nirudi kwenye jumuiya kukutana na kuhamasishana kwenye mambo mbalimbali. Binafsi ningependa kuona watu wa mahali fulani (wananchi wa mkoa wa Kagera kwa mfano) wanakutana na kutaka kusaidia eneo fulani badala ya kukutana kwa minajili ya kabila. Kwa mfano, kuna wachagga wengi ambao ni wazaliwa wa Dar, na kuna wangoni ambao hawajawahi kukanyaga Songea lakini wamekulia Tanga n.k Hivyo kimsingi kama jumuiya ni wananchi wa mkoa fulani au wilaya fulani wanakutana kusiwe na kutaja kabila bali wananchi wa sehemu ile wote regardless of their tribal affiliations.

Ila inapotokea kuwa wananchi hao wanapokutana na wanajikuta kuwa ni watu wa kabila moja na kuna watu wawili ambao wanatoka mikoa ile lakini siyo wa makabila ya kule na watu hao wakaambiwa hawakaribishwi, basi huo ni ukabila!

Je hayo ndiyo yanayotokea Mlimani na kwenye vyama hivi vya watu wa mahali pamoja?
 
Mwanakijiji,

..huu ukabila unakuwa exaggerated.

..hivi vyama vya makabila/wilaya vimechipuka baada ya serikali kushindwa kupeleka maendeleo mpaka ngazi ya wilaya.

..wananchi walielekezwa wavivunje kwa ahadi kwamba serikali itakuwa makini, na hakutakuwa na haja ya wananchi kuhamasishana/kuchangishana kupeleka maendeleo wilaya wanazotoka. serikali imeshindwa, vyama vimerudi.

..kuna sehemu wananchi wamerudi kwa waganga wa kienyeji kwasababu hudumu za afya za kisasa hazipatikani.

..wakulaumiwa ktk hili ni SERIKALI, siyo wananchi.
 
Hii mada wakuu ni ngumu, ni ngumu hasa kwakuwa kila mtu hapa ana kabila na kwa kweli kwa njia moja au nyingine kama amepita chuo kikuu anaweza kuwa ameshiriki kwa njia moja au nyingine. Kwa maoni yangu mimi, nadhani tatizo hapa sio ukabila,tatizo hapa ni azma zilizojificha za haya makundi(kama zipo) Hivi vyama wanafunzi wamevirithi toka naweza kusema awamu ya kwanza. Kibaya hapa nachokiona ni kugeuka kwa mwelekeo wa hivyo vyama na kuanza kuwa vyama vya kutafuta ajira serikalini na kwingineko kwa kutumia God fathers walioko huko,kutafuta upendeleo,kushiriki katika kampeni za kisiasa, na kuanza kusema sisi ni bora kuliko wale. Lakini kama malengo ni hayo aliyoyasema mtanzania(1. Kusaidiana wakati shida na Raha
2. Kusaidia kule tulikotoka: hapa tulikua na legho mahususi. kuongeza idadi ya wataojiunga chuo kikuu kwa kufanya yafuatayo
a. kutoa madesa(vitabu, pamphlets.n.k) kwa shule za sekondari zilizopo maeneo husika.

b. Wote wanaosomea ualimu kuzipa priority shule zilipo maeneo husika na tulitoa motisha kwa wote wataoenda kufundisha regardless kule anatoka yaani sio lazima anayetaka kufundisha awe ametoka morogoro ndio afundishe shule za morogoro bali yeyote atakaenda kufundisha shule za morogoro basi tulimpatia motish sawa na wale waliotoka morogoro japo ulikua kidogo.

c. Kutoa seminara za Ukimwi mashuleni na kuwapa vijana Moyo na mbinu mbali mbali za kusoma ili kufaulu.
) nadhani hakuna ubaya. Kinachotakiwa zaidi ni usimamizi na ufuatiliaji wa karibu kuona shughuli za hivi vyama,haitoshi tu kuvisajili na kuvipa namba ya usajili,je vinawajibika vipi kwa Dean of students?je,uwepo wake umewahi kufanyiwa tathmini ili kuona namna gani vinaathiri chuo hasi au chanya na je,vina mchango gani katika kutekeleza hayo malengo ya katiba zao. Hayo malengo ni vivuli tu? au ndio malengo halisi yanayotekelezwa? Nadhani kuanzia hapa ndio hatua nyingine inabidi ifuate
 
all in all au kwa ufupi nijuacho mie ni kuwa everything has got its benefits and harms!!

so we have to be macho navyo so as to ensure we enjoy benefit zake na twazuia harms zoote from all possible angles tusije fika walikofika majirani zetu
 
Nilipokuwa chuoni wote tulikuwa kama Watanzania. Pamoja na kuwa tulikuwa na umoja wa wanafunzi, lakini umoja huu uliwaunganisha Watanzania wote bila kujali wanatoka wapi Tanzania. Sasa hivi vyama vya kutengana chama cha wahaya, wasagara, wanyiha, wanyakyusa, wangoni kama vikiendezwa vitaleta ukabila Tanzania na matokeo ya ukabila tumeyaona katika uchaguzi uliofanyika Kenya hivi karibuni. Vyama hivi vipigwe marufuku katika vyuo vyote vya elimu ya juu Tanzania.
 
Back
Top Bottom