Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
dua fungu la ule msaada wa barabara za kili ,ulikuwa ni msaada wa mfadhili ambaye alielekeza specifically pesa ziende wapi,..hata wafadhili wana priority zao..kwa mfano hizo pesa zili cover pia kuboresha barabara kuelekea hifadhi ya kilimanjaro kupitia njia ya machame na marangu...pia kipindi hicho hicho barabara ya arusha to ngoro ngoro ikajengwa kwa kiwango cha lami....nafikiri kama sikosei hata ile ya kupita serengeti imefanyiwa ENVIRONMENTAL IMPACT ASSESSMENT...unajua wazungu wako very sensitive kusaidia maeneo ambayo pia na wao wanayatumia ,sasa kwenye vivutio vya utalii ni kati ya sehemu hizo...na hata siku moja huwezi kukata pesa ya kupeleka maji nzega kutuka lake victoria upeleke masaini...hiyo ilikuwa zamani na ikatuletea sifa mbaya ,,sasa hivi project management zinashirikisha wafadhili kuanzia hazina....
NIKUPE MFANO WA MILLENIUM GOAL mfuko wa wamarekani kwa nchi masikini ,juzi tu wamekuja hapa na wanafungua ofisi pale hazina ili kusimamia pesa zao zitumike kwa malengo waliyoweka.
PH
Mjomba mimi naweza kukusahihisha mambo mengi tu uliyosema hapo juu na yote ni katika kuweka FACTS sawa
Ninafanya kazi na organisation ambayo inatoamikopo katika nchi nyingi zinazoendelea na naweza kukuhakikishia kuwa huwa tuna tatizo kubwa sana katika baadhi ya nchi na hususwa za Africa kama kenya, Zimbabwe,Nigeria,Ghana,Zabaia,Uganda,Sudan na bila kuisahau Tanzania katika suala zima la kupunguza umasikini kuna UKABILA wa hali ya juuu katika proposals zao na hii inatokana na hao wanaowakilisha reports zao kuhusu miradi gani ifanyiwe kazi. Nitakupa mfano mdogo back in 90's Kenya kulikuwa na malalamiko makubwa kuhusu miradi mingi kwenda Rift Valley na Western Kenya kama Nyanza na Kakamega ili hali watu wanakufa na njaa Trukana na Marsabit vile vile mikoa ya Pwani iliachwa na ikapelekea movement ya jamaa wa COAST kutaka kujitenga na ikaundwa tume....kumbe baada ya uchunguzi kufanyika ikaja gundulika kuwa kulikuwa na Wakikuyu wanawapiga bao wajaluo ambako wao nao waliona isiwe tabu kwani wanao vigogo wao ambako walitaka investments ziende na kwao...
Si kweli kuwa wazungu ndio wenye kuweka priority bali ni nchi mwanachama kama Tanzania ambayo huwa tunahitaji tupate mikakati yao ya kupunguza umasikini na hapo ndipo jamaa wa Mipango wanawasilisha miyo Poverty Reduction Strategy Papers (PRSPs) na kusema ukweli ni kuwa mikoa mingi inayopewa kipaumbele mfano wa kurekebisha infrastructure Tanzania ni mikoa ya Kaskazini LAKINI SIYO KUTOKANA NA PRESHA ZA WAZUNGU kama ulivyosema bali
Vile vile umekosea kusema kuwa MILLENIUM DEVELOPMENT GOALS ni mfuko wa Wamerekani. Huuu ulikuwa ni mfuko ulioanzishwa na UNITED NATIONS kushirikisha member states zote za UN na kulikuwa na GOALS 8 ambazo walipeana kama njia za kumaliza umasikini na ofisi iliyofunguliwa DAR japo unaweza kufikiri iko independent lakini wako chini ya Country office ya UNDP
nimeona bora nikuweke sawa na hizo facts hapo juu