Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Dua, sijaangalia ni nani aliyesema, nimeangalia hoja alizotoa. Hakuna ushahidi aliotoa ambao unaondoa maelezo mengine na kubakia ukabila tu. Je ni undugu unaoendelea, je ni urafiki, je ni rushwa? Kuona majina ya watu wa kabila moja na kudai huo ni ukabila ni hitimisho la kihisia (emotional conclusion). We have to eliminate all the other factors before we conclude with authority that there is tribalism in TRA and other institutions. As long as the other factors are at work, madai ya ukabila have no basis in reality or fact and they remain to be just that, madai!!
Endapo itatokea kuwa kwenye mtaa fulani majambazi wamekuwa wakivunja mara nyingi na kuiba, na tukagundua baadaye kuwa wengi wanaoibiwa ni watu wa kipato cha chini, je tunaweza kuhitimisha kuwa wezi wanawalenga masikini? Kabla hatujasema hivyo, tukagundua kuwa kuna nyumba za masikini wengi ambao hazizunjwi mtaa huo huo na tulipofutilia tukadungua kuwa wenye nyumba hizo wameweka vitasa na makomeo ya uhakika na wanahakikisha kuwa kuna mtu nyumbani, je hilo halielezei kwanini nyumba zile nyingine huvunjwa? Sasa wale masikini wanovunjiwa nyumba kila siku watadai wanafanyiwa hivyo kwa sababu ni masikini au kwa sababu nyumba zao hazina ulinzi wa kutosha? Anayeta kuona ukabila anaweza kufanya hivyo, lakini ili aweze kutushawishi sisi wengin ni lazima aoneshe kisayansi kuwa hakuna maelezo mengine yanayoelezea hali hiyo.