UK yaichambua Tanzania, yaishangaa na kuibeza, tunaongoza kuombaomba kama nchi zilizokuwa vitani

Inasikitisha kusome na hasa ukutazama mbele hakuna matumaini.

Inasikitisha kwa vile tumeporwa raslimali zetu kwa misingi hii hii ya kupewa misaada. Wananchi wetu wamefukuzwa kwenye maeneo yao, wachache wamefanywa manamba wa kitumwa katiaka migodi hii. Serikali yetu inapewa huo msaada ili kuwafunza na kuwawezesha mapolisi wetu kuwalenda wao na makuwadi wao ili watuibie zaidi. Sasa wamemaliza sehemu kaeribu zote nyeti kwa mikataba ya kilaghai ambayo wanaona itawalinda mpaka hapo watakaotuachia mashimo, magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingara, umaskini uliokithiri na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mkapa ni mla watu ni baba wa mabo haya yote, na fisadi mwenzake Kikwete. Taifa hili halitakaa kuwasamehe kwa haya mliotufanyia.

Ninakosa matumaini kwa vile serikali yetu ni ya kifisadi na mihimili yake yote, sisiemu imekuwa chama cha mafisadi, italinda na kudumisha hulka hiyo kwa njia yoyote ile ikiwa kama wanavyofanya sasa kwa kuchukua madaraka kwa nguvu nje ya matakwa ya wananchi na itazidi kutugawa kwa misingi ya imani, makabila, ukanda nk. Katiba tunayotaka hatutaipata, kama tutapata basi itakuwa mbaya mara 100 kuliko tuliyonayo.. Jk atazidi kuendelea kuuza rasilimali zote zilizosalia katiaka kipindi hiki kwa sababu baada ya kusema hajui sababu ya umaskini wetu akiona fahari bila aibu kuomba omba sasa amekuja na jibu kuwa ni ukosefu wa wawekezaji na uwekezaji wake ni huu wa kifisadi kama alivyofanya mtangulizi wake. Na kama katiba yake mpya haitampa kuendelea kututawala basi watahakikisha fisadi mwingine na hasa Lowasa atashika madaraka.

Kweli tutaendleea kulia na kusaga meno mpaka lini? Kuna mtu alisema humu tuingie msituni. Je tuna haki ya kulalamika tu bila kujua la kufanya? Si misahafu inasema jisaidie nami nitakusaidia! Je babu zetu hawajasema suluhu haiji ila kwa ncha ya mapanga! Basi kwa vile kuna njia za amani kama mijadala nk, basi ziiwe agenda kuu kwa vyama na yale ya kisomi nk

Nani atakaeyeturudishia matumaini Tanzania? Dr Slaa! Nasema NDIYO.
 
One day it wil be...........nad yes we will..............

It is better to be poor but free rather than being rich but a slave
 
Ndugu yangu nimeupenda uchambuzi wako kwa kina.Hakika umekaa vyema,ila hiyo sasa ndugu yangu ndiyo Tanzania eti twaitwa masikini,twatumia mabilioni ya shilingi kuelezea mafanikio yetu tuliyopata wmbayo hayakutakiwa watu watangaziwe si wanayaona wenyewe,Hivi ulishajiuliza tangu tuanze kuukimbiza mwenge hadi leo hii umeleta ninin?kwani hizo hela si zingeelekezwa kufanya kazi hata ya kujenga shule kama hii uliyotuonyesha kwenye picha,yapo mengine ni vigumu kuamini kama yanatokea nchini kwetu,ila ninatamani kuiona Tanzania mpya ninayoifikiria siku moja kwa msaada wa Mungu yatakuwa,kwani naamini waliopo nao watatoka tu katika nafasi walizonazo sasa ambazo wapo kwa maslahi yao binafsi na ndugu zao,marafiki zao,na watoto wao,na dini zao.kazi njema wandugu
 
Kuna haja ya maksudi kwa Ccm na Serikali yake kuondoka madarakani mwaka 2015 au kabla ya hapo.
Tutajitahidi kuchangia kiufundi kuhakikisha wameondoka, na hiyo inawezekana.
 
Sina haja hata ya kusoma zaidi mkuu, inatosha sana kwa maumivu ya kufukuzwa tu ma dakitari huku viongozi wa serikali wakiugua kidogo wanapelekwa apollo india.
 
Hii sentence ni muhimu sana!!

The director of the International Centre for Tax and Development Research, Professor Odd-Helge Fjeldstad, observes that Tanzania is good at chasing donor money and argues that if efforts chasing donor funds were reduced by one per cent and redirected to increase local revenue collections, the treasury coffers could have increased.

Hapo kwenye red inanikumbusha wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka juzi wakati JK alipoahirisha kampeni kwa muda wa nusu saa akidai anaongea na balozi wa Tanzania huko USA. Baada ya simu alida kuwa Obama kawahakikishia misaada hivyo wananchi wampe kura!!!!
 
Hii sentence ni muhimu sana!!

Hapo kwenye red inanikumbusha wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka juzi wakati JK alipoahirisha kampeni kwa muda wa nusu saa akidai anaongea na balozi wa Tanzania huko USA. Baada ya simu alida kuwa Obama kawahakikishia misaada hivyo wananchi wampe kura!!!!
Zero siyo hilo tu. Nakumbuka wakati wanazindua ujenzi wa barabara za East Africa, JK alitamka kitu kimoja juu ya ufuatiliaji wa ahadi nilishangaa sana, alisema ni muhimu kuwakumbusha waliotoa ahadi, tena alienda mbele zaidi na kusema wakati mwingine hata kuwatembelea na kuwaambia mzee unakumbuka ahadi yako? sasa kwa mtindo huo Mzee Dr JK ni zaidi ya Mhasibu.
 
To hell with uk ambao waliturudisha nyuma kimaendeleo kwa kukalia nchi yetu kimabavu na kutunyanyasa waafrika huku wakiiba mali asili yetu!
Leo hawa wezi hawana sura ya kuja kutufundisha au kutoa ripoti za uongo na za kinafiki! Bado machungu ya kutawaliwa na kudhalilishwa ktk nchi zetu zipo vichwani mwetu na katu hatutawasamehe wakoloni hawa!
 
Matusi kwa Serikali yetu ombaomba kutoka kwa wahisani.

Tanzania depends annually on foreign aid by 45 per cent, receiving US$453 million for its 2011/12 aid budget under the umbrella of General Budget Support (GBS)

"African governments (particularly Tanzania) consider foreign aid as a permanent, reliable and consistent source of income providing no reason to adopt an alternative policy to foster and finance the economic development of their countries. If the only thing you have to do is to collect your aid cheques, why should you elaborate an economic-financial policy or planning in the long term?"

"It is said, Tanzania is good at chasing donor money and argues that if efforts chasing donor funds were reduced by one per cent and redirected to increase local revenue collections, the treasury coffers could have increased. He highlights the negative relationship between aid funds and revenue collection i.e the more we get aid, the less we make local revenue collections and vice versa”.

Wahenga walisema mazoea hujenga tabia, suala la Serikali yetu kuombaomba sasa limekuwa ni tabia, yaani hata pasipofaa/kisichofaa/asiyefaa kuomba/kuombwa Serikali yetu inajikuta imeomba.

Kwa kweli ukisoma hiyo directed article, utaona jinsi nchi yetu inavyotia aibu na jinsi ilivyochokwa kwa uombaomba wake na mbaya zaidi kuwa ombaomba wakati una uwezo wa kujitegemea. Hawakuishia hapo wanasikitishwa sana na kitendo cha kuombwa fedha kwa ajili ya maendeleo na wakishapewa fedha hizo haziwafikii walengwa kutokana na Rushwa iliyokithiri na lack of commitment ya hao ombaomba katika kuwakwamua watu wanaowaombea hizo hela. Itoshe tu kusemwa kuwa hapa tumetukanishwa na viongozi wetu wasio wabunifu na wasio na dhamira ya dhati ya kututoa hapa tulipo. Nchi yetu haina kasoro hata kidogo ya kutufanya tushindwe kujitafutia na kuwa na bajeti isiyo tegemezi.

Nini sasa kifanyike??????

Hawa jamaa wametukumbusha jinsi sekta ya madin peke yake inavyoweza kututoa hapa tulipo. Kweli tume ya Jaji Boman ilikaa na iliandaa Report ambayo kama ingetekelezwa ingeleta ahueni. Wananchi inatupaswa sote kwa pamoja tuishinikize Serikali kuitekeleza. Waingereza ni wawekezaji pia ila nao wanashangaa ni uwekezaji wa aina gani uliopo Barrick Gold Mine na migodi mingine iliyopo Tanzania, ambapo mwenye mali anapata chini ya 5%, huu ni wizi ingawa watawala wetu wanaona sawa, Hawa watawala wanakuwaga na percent zao mule hivyo tukiwasubiria wao wafanye maamuzi magumu tutakuwa tumeamua kuliwa

Sehemu nyingine waliotukumbusha ni kwenye kukusanya pato la ndani. What TRA is doing Rright now kwa kweli ni TRADITIONAL way of collecting revenue where mlipa kodi anajisalimisha mwenyewe. Huu ni upumbavu kabisa kwa maana inafahamika vzr tu kuwa tabia ya mlipa kodi ni kukwepa kodi! Kwa Tanzania Kodi ambayo inakusanywa kwa asilimia kubwa ni kodi ya PAYE/ Mishahara, ukusanyaji wa kodi nyingine zote ni ubabaishaji mtupu. Nini kinashindikana katika kukusanya kodi???Viongozi wetu kutwa mnashinda Ulaya na marekani kwann hamtaki kujifunza walichofanya wenzetu huko kwao??Inawezekana uzembe huu wa kutokuziba mianya ya ukusanyaji wa kodi unafaidisha wafanyamaamuzi na ndio maana wamefumbia macho suala hili. Ili kuepukana na matusi haya kwa kweli kuna haja sasa suala la kuziba mianya ya ukwepaji kodi kupewa kipaumbele, sisi ni wakushindwa hata na COMORO??
 
watz tunatakiwa tufundishwe kuvua samaki na si kupewa samaki. Kwanini serikali isiombe misaada ya ujuzi zaidi kuliko ya kifedha!!!
 
Matusi kwa Serikali yetu ombaomba kutoka kwa wahisani.

Tanzania depends annually on foreign aid by 45 per cent, receiving US$453 million for its 2011/12 aid budget under the umbrella of General Budget Support (GBS)

"African governments (particularly Tanzania) consider foreign aid as a permanent, reliable and consistent source of income providing no reason to adopt an alternative policy to foster and finance the economic development of their countries. If the only thing you have to do is to collect your aid cheques, why should you elaborate an economic-financial policy or planning in the long term?"

"It is said, Tanzania is good at chasing donor money and argues that if efforts chasing donor funds were reduced by one per cent and redirected to increase local revenue collections, the treasury coffers could have increased. He highlights the negative relationship between aid funds and revenue collection i.e the more we get aid, the less we make local revenue collections and vice versa".

Wahenga walisema mazoea hujenga tabia, suala la Serikali yetu kuombaomba sasa limekuwa ni tabia, yaani hata pasipofaa/kisichofaa/asiyefaa kuomba/kuombwa Serikali yetu inajikuta imeomba.

Kwa kweli ukisoma hiyo directed article, utaona jinsi nchi yetu inavyotia aibu na jinsi ilivyochokwa kwa uombaomba wake na mbaya zaidi kuwa ombaomba wakati una uwezo wa kujitegemea. Hawakuishia hapo wanasikitishwa sana na kitendo cha kuombwa fedha kwa ajili ya maendeleo na wakishapewa fedha hizo haziwafikii walengwa kutokana na Rushwa iliyokithiri na lack of commitment ya hao ombaomba katika kuwakwamua watu wanaowaombea hizo hela. Itoshe tu kusemwa kuwa hapa tumetukanishwa na viongozi wetu wasio wabunifu na wasio na dhamira ya dhati ya kututoa hapa tulipo. Nchi yetu haina kasoro hata kidogo ya kutufanya tushindwe kujitafutia na kuwa na bajeti isiyo tegemezi.

Nini sasa kifanyike??????

Hawa jamaa wametukumbusha jinsi sekta ya madin peke yake inavyoweza kututoa hapa tulipo. Kweli tume ya Jaji Boman ilikaa na iliandaa Report ambayo kama ingetekelezwa ingeleta ahueni. Wananchi inatupaswa sote kwa pamoja tuishinikize Serikali kuitekeleza. Waingereza ni wawekezaji pia ila nao wanashangaa ni uwekezaji wa aina gani uliopo Barrick Gold Mine na migodi mingine iliyopo Tanzania, ambapo mwenye mali anapata chini ya 5%, huu ni wizi ingawa watawala wetu wanaona sawa, Hawa watawala wanakuwaga na percent zao mule hivyo tukiwasubiria wao wafanye maamuzi magumu tutakuwa tumeamua kuliwa

Sehemu nyingine waliotukumbusha ni kwenye kukusanya pato la ndani. What TRA is doing Rright now kwa kweli ni TRADITIONAL way of collecting revenue where mlipa kodi anajisalimisha mwenyewe. Huu ni upumbavu kabisa kwa maana inafahamika vzr tu kuwa tabia ya mlipa kodi ni kukwepa kodi! Kwa Tanzania Kodi ambayo inakusanywa kwa asilimia kubwa ni kodi ya PAYE/ Mishahara, ukusanyaji wa kodi nyingine zote ni ubabaishaji mtupu. Nini kinashindikana katika kukusanya kodi???Viongozi wetu kutwa mnashinda Ulaya na marekani kwann hamtaki kujifunza walichofanya wenzetu huko kwao??Inawezekana uzembe huu wa kutokuziba mianya ya ukusanyaji wa kodi unafaidisha wafanyamaamuzi na ndio maana wamefumbia macho suala hili. Ili kuepukana na matusi haya kwa kweli kuna haja sasa suala la kuziba mianya ya ukwepaji kodi kupewa kipaumbele, sisi ni wakushindwa hata na COMORO??

Mkuu mie kabla ya kuipost hapa nimeisomaaaa nikashuikwa na uchungu lakini nikasema ngoja nione watanzania wenzangu wanasemaje. Na hii kweli imenisikitisha Mtu anakwambia japokuwa nakusaidia wewe ni Lipumbavu.
 
To hell with uk ambao waliturudisha nyuma kimaendeleo kwa kukalia nchi yetu kimabavu na kutunyanyasa waafrika huku wakiiba mali asili yetu!
Leo hawa wezi hawana sura ya kuja kutufundisha au kutoa ripoti za uongo na za kinafiki! Bado machungu ya kutawaliwa na kudhalilishwa ktk nchi zetu zipo vichwani mwetu na katu hatutawasamehe wakoloni hawa!

Wewe naona umeamua kupingana na uhalisia wa mambo kwa sababu unazozijua wewe. Nadhani umesahau historia, nchi zilizotawaliwa na Waingereza haikuwa Tanganyika peke yake. Tulikuwa wengi sana tulionyonywa, kuteswa na kukandamizwa, bad enough Waingereza hawakuwa wacoloni per se! walikuwa our Protectorate. Anyway ninachotaka kusema hapa ni kwamba sababu uliyoitoa haijustify uzembe wetu, ufisadi wetu, ubabaishaji wetu na uombaomba wetu kama nchi. Hizo sifa zote tunazo cha msingi tujadiliane nini kifanyike na sio kuwarudishia lawama waingereza ambao nao kimsingi wamechoka biashara ya kubeba watu wasiobebeka kwa sababu ya kuendekeza wizi, ufisadi na kutokuwajibika
 
Maumivu ya kichwa huanza taratibuuuuu...... There is a long way to go..... but with this speed!!!! I can't see the way out..... ohooo Gosh.... "Msituni"...
 
To hell with uk ambao waliturudisha nyuma kimaendeleo kwa kukalia nchi yetu kimabavu na kutunyanyasa waafrika huku wakiiba mali asili yetu!
Leo hawa wezi hawana sura ya kuja kutufundisha au kutoa ripoti za uongo na za kinafiki! Bado machungu ya kutawaliwa na kudhalilishwa ktk nchi zetu zipo vichwani mwetu na katu hatutawasamehe wakoloni hawa!

wakati tanzania inapata uhuru ilikuwa masikini sawa na singerpore.....kwa kifupi misaada inayotolewa na nchi wahisani inaliwana viongozi wetu wa nchi
 
Ninakumbuka pia wakati wa kampeni Kikwete aliulizwa kwenye TBC kama sikosei kwamba anataka watanzania wamkumbuke kwa lipi baada ya urais wake (legacy)....na jibu lake lilikuwa fupi lakini bibafsi nililielewa; alisema na namnukuu.."ninataka watanzania wafikie mahali waseme kwamba tulikuwa mahali hapa kabla ya kikwete, na sasa tupo hapa mara tu baada ya kikwete".

Mnaona? Jibu lake kuhusu legacy yake linatufundisha nini? Linatufundisha kwamba next time watanzania tuwe makini kuchunguza sana uwezo wa akili wa mgombea urais kabla ya kumpa kibarua cha Ikulu. Sasa hilo jibu linaeleza nini kama siyo kushindwa kujibu swali? Mimi nilimwelewa kwamba hapo bosi wangu ndo mwisho wa kufikiri kwake. Miiaka kibao ya ubunge, miaka kibao ya uwaziri, miaka mitano ya urais, unashindwa hata kuelezea legacy yako kwa ufasaha unasema utawahamisha watanzania? Na kweli katuhamisha. Katuhamisha kutoka kwenye trajectory nzuri ya uchumi imara iliyoachwa na Mkapa (pamoja na mapungufu yake) kuelekea kwenye uchumi mbovu na maisha magumu ombaomba yasiyoelezeka ikiwemo kudharauliwa na Wayahudi (Ehud Barak) na sasa ona hata Waingereza!!!
 
Mkuu mie kabla ya kuipost hapa nimeisomaaaa nikashuikwa na uchungu lakini nikasema ngoja nione watanzania wenzangu wanasemaje. Na hii kweli imenisikitisha Mtu anakwambia japokuwa nakusaidia wewe ni Lipumbavu.

Kiongoz tunashida sana na hii serikali yetu ya kipumbavu. Sasa cjui kwanini wanang'ang'ania kuwahi Ikulu ilihali hawana uwezo wa kuongoza na kuleta mabadiliko. Katika KATIBA mpya WANANCHI na sio WABUNGE tupewe uwezo wa kupiga kura ya VOTE OF NO CONFIDENCE kwa viongozi WABABAISHAJI pale mazingira yanaporuhusu.
 
Back
Top Bottom