Ujumbe wa wazi kwa idara ya maji - mwanza (mtatuua wanafunzi wa saut - malimbe)

Kilangi Maliseli

New Member
Dec 9, 2011
2
0
:shock:Waheshimiwa wa idara ya maji Mwanza Hamjambo? Sasa yapata wiki nzima sisi wateja wenu wa maeneo ya Nganza na Malimbe - Nyegezi hatuna maji. Nashindwa kuelewa nini hasa tatizo na nikubwa kiasi gani hata lichukue muda mrefu namna hiyo. Kumbukeni kuwa sisi ni wanadamu tunaohitaji maji katika shughuli zetu za kila siku, isitoshe wengine ni wanafunzi kwani mazingira haya ni maarufu kwa kuishi wanachuo (SAUT). Hali ni mbovu achilia mbali kuoga na matumizi mengine lakini kubwa zaidi ni OFISI KUU (VYOO), kwa kweli hali si nzuri ama mnataka mpaka tuugue magonjwa ya mlipuko kama KIPINDUPINDU ndo mturejeshee maji? Mbona gharama za bili tunalipa? Nawaomba mfanye hima mturejeshee huduma hii muhimu kwa maendeleo ya afya zetu.

Vyombo vya habari na viongozi wa jamii tafadhalini, nawaomba muingilie kati suala hili kabla halijaleta madhara makubwa sisi ndo vijana ambao ni warithi wa Taifa hili. Ni aibu na dhambi kubwa sana kupoteza masomo, maisha na mambo mengine ya msingi kwa sababu ya MAJI mbona hivyo?

NB: Miaka 50 ya uhuru Mwanza maji tatizo na ziwa lipo vipi sehemu kama Shinyanga.
Tumepiga hatua majengo si huduma za kijamii kama AFYA.

Mheshimiwa Wenje, Tutazame wananchi wako wa Maeneo ya Nganza na Malimbe TUNAADHILIKA..!
 
Back
Top Bottom