Ujumbe wa Mh Kingwangala kwa Umma!

@Kituku, mimi siyo mtawala, mimi ni muwakilishi wa wananchi kwenye Bunge, sihofii chochote kutokana na maandamano ya CHADEMA na hata yale ya kule Kaskazini mwa Africa. Na mimi mtazamo na msimamo wangu kwenye masuala ya vurugu uko wazi kabisa, ni kitu nisichokitaka na nitakipinga siku zote. Naomba ifahamike hapa wazi kabisa kuwa 'sipingi maandamano' - hata mimi nimeishatoa mwaliko wa maandamano ya amani kupinga uwepo wa mgodi Nzega, na wewe nakukaribisha ushiriki. Sema nasikitishwa sana na kauli ya kiuchochezi iliyotolewa na mmoja wa viongozi wa CHADEMA kuwa Tanzania 'haitotawalika' na pili nasikitishwa sana na tafsiri potofu ya watanzania wenzangu, tena wengi wasomi wazuri kabisa, wanaojaribu kufananisha hali yetu kisiasa na kiuongozi na ya kule kaskazini na pia kufananisha maandamano safi kabisa ya CHADEMA na maandamano ya watu wenye hasira kali wa kule. Tatu, nasikitishwa na tafsiri potofu ya 'nguvu umma' - kwa kawaida nguvu ya umma haitegemewi ihamasishwe na chama cha siasa, maana yenyewe huibuka ghafla pale wananchi wanapochoshwa na mfumo wa kisiasa na kiuongozi unaotawala nchi au ukandamizaji unapozidi. Sasa hapa watu wanaongelea nguvu ya umma inayohamasishwa na chama cha siasa...kwa vyovyote vile hawatofanikiwa kuungwa mkono na watanzania walio wengi badala yake watabaki wao wachache na wanachama wao.

@SMZ, kama kuna mtu anahitaji gari kubwa aina ya 4WD basi ni Mbunge...mimi kabla sijawa Mbunge nilidhani kwamba kumpa gari
Mbunge ni anasa na matumizi mabaya ya pesa za umma, lakini baada ya kugombea tu nikaanza kuuona umuhimu wa uamuzi huu (wengine watasema kuwa nasema haya kwa kuwa mimi kwa sasa ni beneficiary! lakini mimi hupenda kusema ukweli na huu hapa ni ukweli tupu). Hebu jiulize Mbunge anafikaje kwa wananchi wa jimboni kwake? Barabara mbovu, huwezi kwenda na gari ndogo, wananchi wanataka Mbunge ufike kuwasikiliza kero zao, ushiriki kwenye kazi za maendeleo na matatizo na majanga ya kijamii, ukague miradi, n.k. Hivi utafikaje bila kuwa na gari? Sijui kwa nini walifikia maamuzi ya kutoa mikopo ya pesa hizi badala ya kuwapa wabunge magari, lakini naamini katika umuhimu wa kuwa na gari kwa kweli.

Nawasilisha,
Kigwangalla.
We kigwangala ulitakiwa ukemee kwanza dowans, epa, kagoda na ufisadi mwingine ndan ya ccm yenu
maana amani yetu inaharibikia hapo na si cdm kama mnavotaka 2amin. Tatizo ni kwamba tukionacho kuwa ni ttzo ccm wanaiona ni opportunity. Wakati sisi tunalilia miguu ninyi mwalilia viatu! Mmechakachua kila sehem. Aman ilishatoweka kakabaki kau2livu nako mmeanza kukaandama,..
 
Back
Top Bottom