UJUMBE WA MBUNGE: Shukrani, Twende Kazi!

Hongera sana Mnyika.
Wengi wana imani kubwa sana na wewe. Wewe ni kielelezo kizuri sana kwa vijana.
Keep it up.
Ushauri wangu wa haraka kwa ajili ya mafanikio yako ya kisiasa. NAJUA MENGI NINAYOSEMA HAPA UNAYAJUA NA PENGINE UNAYATEKELEZA HATA KWA ZAIDI LAKINI KUYASIKIA TENA KUTAKUPA KUYAIMARISHA.
1. Endelea na moyo wa kweli wa kutumikia watu - usirihusu uheshimiwa uingie moyoni. Jiite mtumishi moyoni na usikubali kulewa uheshimiwa.
2. Jilinde na suala la umaarufu. Umaarufu utatokea kwa wale wasioutafuta.Tafuta daima maslahi ya wengi.
3. Uwe mwangalifu na wanaokuzunguka tafuta wakweli wachache wakupe maoni na mtazamo wa kweli hata kama ni kukuonya uwe na watu hao, hao ni wazuri kuliko watakaokusifia kwa kila kitu huku pembeni wakikulaumu.
4. Pata nafasi kila wiki angalao mara moja ya kusoma kila kinachowezekana kwa habari za kimataifa.
5. Hakikisha kuwa unashiriki ibada kila wiki popote ulipo licha ya shughuli nyingi ulizo nazo ( kama ni Mkristo usiende kwenye nyumba moja tu au dini moja tu.) Nenda kwenye nyumba tofauti za ibada kila inapowezekana na sio lazima iwe ya dhehebu lako. Utajifunza mengi sana.
Wabunge wengi huanza kwenda kwenye nyumba za ibada wakati wa kampeni.
6. Anzisha sanduku lako la maoni jimboni mwako na hakikisha una mtu anayeyasoma na wananchi wako wajue kuwa kuna sanduku la maoni.
Utatukanwa katika maoni hayo, utalaumiwa, Usijali wala kuacha, kwani pia utaupata uwekli mwingi kuhusu hali halisi. Wape watu uhuru wa kutokuandika majina yao.
ASANTE SANA. HAYO TU. HAYA NINGEWEZA KUKUTUMIA BILA KUYAWEKA HAPA KAMA KUNGEKUWEPO NA EMAIL YAKO.
 
Hongera JJ,

Mwanzo mzuri kwa kweli. Mimi ni mkazi wa Goba mtarajiwa na kinachonichelewa kuhamia huko ni hiyo barabara inayounganisha barabara za Bagamoyo na Morogoro. Maadam iko kwenye vipaumbele vyako natumaini nitakuwa mpiga kura wako 2015 kama Mola anatujalia kufika.
Binafsi naamini maendeleo yataletwa na wananchi wenyewe na si mbunge isipokuwa kazi yako iwe kuainisha mipango, kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wake.
Ombi langu kwako ni moja tu. Ainisha katika mipango yako ipi inahitaji nguvu ya wananchi na ipi itahitaji msukumo kutoka serikalini (Kuu na Halimashauri).
Inayotuhitaji sisi tushirikishe. Mh JJ kinachofanya tuchangie harusi ni kwa vile tunaona pesa yetu imetumikaje sasa tumia nia njema hiyo ili Ubungo iwe ya kupigia mfano.
 
Nashukuru Mbunge wangu lile tuta la Stop over vp ulilifanyia kazi mwenyewe?

Fidel80,

Sio mwenyewe, ni wadau kadhaa wakiwemo baadhi wanaohusika na miundombinu. Lakini nashukuru kwamba hiyo ni kati ya ahadi za kwanza kutimia kadi ya ahadi nilizotoa kwenye kampeni. Niliahidi ndani ya mwezi mmoja tuta la stop over litakuwa limeondolewa. LIMEONDOLEWA


Tuendelee kufanya kazi

JJ
 
Unaonaje ukianzisha mtandao wa chama hadi mitaani .....hatuko united,CCM wana watu makini huku chini wanahitaji watu wa kuwachunga hawa ndio wanaogawa tshrt ....na wala si ya kudharau
 
Hongera sana JJ! Nimefuatilia mdahalo wakati wa kampeni za uchaguzi, sikuwa na shaka ya ushindi wako wako na kweli umeshinda! Sina shaka pia utatekeleza ahadi zako ulizoahidi!
 
Mkuu hongera sana, mimi nataka tu kujua action plan yako ni ipi katika kufikia hayo malengo na vipaumbele. Wananchi kushiriki watahitaji mwongozo mkubwa toka kwako. Hii action plan ni muhimu sana mheshimiwa. Amini usiamini kati ya wabunge wananchi wenye matumaini naye sana ni wewe mkuu.

Wewe tamka tunaanzia wapi, basi kazi itafanyika kwa ufanisi. Pia ninashauri uwe na timu ambayo ni ya kuaminika itakayokuwa inasaidia kutekeleza action plan hiyo wakati wewe ukiwa kwenye vikao ili kusiwe na gap ya continuation.

Hongera
 
Naona aibu ya kukusifia sana na kukupongeza kwa kuwa muda wa kupongezana na kusifiana umeisha. Hapa JF pamegeuka kuwa sehemu ya kupongezana tuu, wakati si mahali pake. Hapa ni kutoa changamoto na kuwabana nyie wawakilishi wetu. Tunataka kazi uliyotumwa uifanye inavyotakiwa. Naomba ili suala la katiba mpya mlifanyie kazi kweli, hata kama lisipopita, tunataka kuona mmejitahidi kulifikisha bungeni. Mwaka 1995, tulitegemea wabunge wa upinzani wangelifanikisha ili, ila matokeo yao, wakaingia bungeni wakabadilika na kuwa kuwa wabaya kuliko hata CCM na kuanza kugombea rudhuku. Tuna imani na nyie, kama kizazi kipya, vijana na wapambanaji.
 
Mheshimiwa John Mnyika, lngawa inapendeza kama mkitumia "Ndugu" kuliko Mheshimiwa!
Hongera sana kwa kuchaguliwa na nguvu ya Umma na nakutakia kazi njema kwa kibarua kigumu kilichopo mbele yako-ingawa tutakuwa bega kwa bega kuwasupport wabunge wote wa CHADEMA! Umma umewachagua na ku-risk maisha yao kwa kulinda kura na kushinikiza matokeo ya haki yatolewe kwa wakati, Hinyo umma UNAMATARAJIO MAKUBWA SANA kwa CHADEMA. Najua mna mikakati yenu mizuri mlio jiwekea katika kutekeleza malengo na ilani ya chama. Lakini ushauri wangu kwenu ni huu:-

1: Wapigeni msasa baadhi ya wabunge wa CHADEMA ili wawe tayari kusimamia, kutetea na kutekeleza msimamo wa pamoja wa maamuzi ya vikao vya chama. Hata kama walikuwa na mtazamo tofauti juu ya jambo husika ili kuwe na team moja yenye nguvu tofauti na hivi sasa baadhi yao wanajiona wao zaidi utafikiri wamekaa humo mguu upande! Kwa ujumla imarisheni NIDHAMU YA CHAMA.

2: Wabunge wa CHADEMA mjipambanue kimavazi, kimaono na kimkakati tofauti na chama tawala. Ninyi ni wana mapinduzi mnao hitajika zaidi na UMMA katika kipindi hiki kilicho jaa ufedhuli na ufisadi wa kila aina katika Taifa, endelezeni vazi lenu la khaki mpaka kitakapo eleweka. Kila jimbo lina kipaumbele chake, anzieni vipaumbele vya msingi ambavyo viachochea utekelezwaji wa malengo mengine, hakikisheni mnatekeleza yale yote yaliyo ndani ya uwezo wenu mliyoahidi na kuaminiwa na umma katika kipindi cha kampeni.

3: Kumbukeni haki haiombwi bali inapiganiwa! Chama tawala kinatatumia kila mbinu safi na chafu kuwa vuruga, lakini piganieni Tume Huru ya Uchaguzi, Mgombea Binafsi na Katiba Mpya. Tumeona Serikali inavunja katiba kwa kutumia polisi kupiga marufuku mikutano ya CHADEMA!

4: CHADEMA kipinge kauli na mbegu mbaya inayopandikizwa nchini kuwa Taifa lina UDINI! HAKUNA UDINI NCHINI bali kuna watu waliofilisika kisiasa wanataka wajifiche kwenye agenda hiyo baada ya kushindwa uchaguzi.

5: Mpiganie kupunguzwa kwa kodi za mishahara, kuanzishwa vyanzo vya uhakika vya umeme na upunguzwaji wa gharama za kuuganishiwa umeme, upatikanaji wa maji safi na salama katika maneo ya watu, shule za viwango na elimu bora, huduma bora za afya karibu na jamii, utengenezwaji wa miundo mbinu kurahisisha usafiri na usafirishaji, uwazi katika upatikanaji wa viwanja vya makazi, kupiga vita kila aina ya ufisadi katika halmashauri mlizoshinda na Taifa kwa ujumla na kutetea jamii kutumia rasilimali zinazo wazuguka pasipo kuvunja sheria.

Kwa hayo machache mtawatia moyo zaidi wananchi na kuwavutia wengine ili muweze kufanya vizuri zaidi katika chaguzi zingine zitakazo jitokeza. CHADEMA OYEE!
 
Mheshimiwa sana, JJ, Hongera sana. Wana-Ubungo wamefurahi sana safari hii kura zao zimetosha, last time wali-sikitika sana kura zilipokuwa chache. Sasa kazi ni moja tu Mkuu shughulikia, matatizo sugu ya huduma za jamii kwa wana-Ubungo yapate majibu ya wazi kama ulivyo-ainisha na ku-ahidi. Ukumbuke ahadi ni Deni.

Naomba niweke msisitizo kwenye tatizo la maji pia, ina-sikitisha sana kuona kina mama na watoto wana-hangaika na ndoo na vidumu vya maji Dar es Salaam badala ya kufanya kazi za uzalishaji. Hebu wape raha watu wa Ubungo kwa kuwaondolea hii kero, tatizo la maji liwe historia.

Nakutakia Kila la kheri Mkuu. Mungu akutangulie!
 
Dah, yani hapo ndio nachoka na huyu kamanda.

Hawezi kuhimili kujadili hoja bila kumtaja bi shosti wa watu, kha!!

Nachoka kabisa.

Yaani hawezi kabisa aisee!! Naanza kuhisi ataanza na kumwota usiku kama bado hajafanya hivyo tayari. Funny....so funny.
 
nianze kwa salamu yetu...TANZANIA OYEEE....TANZANIA JUU...JUU...JUUU ZAIDI...! mimi ni miongoni mwa wakazi wa jimbo ka ubungo ambao ni miongoni mwa niliokupa kura yangu moja tu. japo nafasi hiyo angesimama NAPE kura yangu moja ningempa yeye.
nimesoma na kuelewa vyema vipaumbele vye jimbo la ubungo....mimi naendelea kusema ni sahihi na havijakaa kiubaguzi wala ki-maslahi ya chama...... pambana katika kutetea wananchi oycome yake itaonekana... BIG UP DOGO KEEP FIGHTING...!
 
Naam, Asante sana Mhe.
Sasa kazi ianze kwa kasi. Elimu kwa wananchi ni muhimu ili waweze kushirikiana kwa hali na mali.

Pamoja tunaweza. Nimefurahi mbunge wangu kwa mipanga mizuri.

Mungu akulinde and kukuongoza siku zote. Usisahau kusali.
 
Hongera, pongezi, JJ, sisi vijana ( watu wa rika lote) tumefurahi kuchaguliwa kwako.
Mm naomba mfanya yafuatayo na nitagusia maswala ya Kitaifa ili CHADEMA 2015 tuongoze hii nchi, kumbuka wananchi ni wengi mnooo na wanawapenda, sera CHADEMA zipo clear, constructive, na imani ya wananchi ni kubwa sana kwa CHADEMA, please piganieni haya
bungeni na kufanya operation Sangara au jina lingine zuri
1. Dr Slaa sasa atangaze sana chama mikoani, atumie muda sasa kufanya mikutano mingi kadiri muwezavyo, remember hata
uchaguzi huu alishinda, tukaibiwa, so hata mtu kufaulu mtihani anajiandaa mapema, Dr Slaa anapendwa mno, kama nyie
wabunge wa CDM, wananchi wanaamini ni nyie mtawakomboa
2. NEC lazima ijengwe mpya, na Rais asihusike na uteuzi wa viongozi wa NEC, iwe huru, bila hivyo hata iweje ushindi ni mgumu mno,
hili pia iainishwe kwenye katiba mpya, maana katiba mpya ni lazima sasa, tumechelewa kwanza, na najua hata ww unajua zaidi.
3. Mfundishane sana nyie wabunge wa CHADEMA, muonekane tofauti kabisa kimawazo, kimsimamo, na wabunge wengine kama ilivyo bunge lililopita, Dr Slaa, Zitto, nk, tumieni akili sana kufundishana muwe kitu kimoja, msiwe wabunge wa kuropoka magazetini hovyo
narudia teach each other well, share u r talents kama za Dr Slaa, utaniambia 2015 CCM ni aibu tupu
4. Bila uoga fichueni mafisadi, mikataba mibovu, viongozi wazembe serikalini kama tuijuavyo CHADEMA thru Dr Slaa bungeni, yupo Lissu, Mbowe , ww mwenywe, Zitto nk, nyie ni makamanda tosha, Dr Slaa inagawa hayupo ndani, ila naamini yupo, yupo tena sana sasa, you know what i mean.
5. TAKUKURU si aminifu si huru, hili lipiganiwe, najua mpo wachache dhidi ya CCM MPs ila ukweli utajulikana, mbona EPA, Richmond, etc
watu wamewajibika, na aibu, na ukweli umejulikana, tena sasa mpo wengi ikilinganishwa na bunge lililopita, so uchache wenu si kigezo, na ikishindikana bungeni kama kwaida ya CHADEMA mnapeleka
kwa wananchi wajue wanavyoliwa.
ww unajua mengi na tunawaamini,
Nakutakieni kazi njema, tupo pamoja, tumeona, tumeyasikia mengi, jikingeni sana maana mnapambana na mafisadi, msije mkadhurika na msijidanganye na maneno haya SIASA si UHASAMA/UADUI, siasa ni uhasama/uadui mkubwa sana hasa hapa Africa. So play safe
Mungu awabariki
 
Nakushukuru. Vipaumbele hivyo ni vya kijimbo, nitasimamia pia vipaumbele vya kitaifa kupitia bunge na suala la katiba mpya ni moja ya hoja/haja nitakazoshiriki kwa uzito mkubwa kwa ajili ya kuleta mustakabali mwema wa demokrasia na maendeleo katika nchi yetu

JJ

Mheshiniwa, kuna vitu vingine ambavyo wananchi na serikali havihitaji fedha kuvifanya, hii ni tabia ya usafi , ninaomba sana madiwani walisimamie hili, kuna uchafu unaoanzishwa ktk makazi ya watu, kuna watu wanaosha magari darajani huku wameweka bendera za CCM na CDM hii ni hatari inamomonyoa daraja, kuna watu wameweka soko barabarani na ni highway,pale kugongwa ni rahisi, hapo mbele ya TANESCO ubungo napo ni soko lisilo rasmi, naomba uzingatie unadhifu wa jimbo kusisitiza kupanda miti na maua na kunadhifisha eneo,kutotupa taka hovyo, naufahamu mto mmoja watu wanachota maji, baadae naambiwa kuna baadhi ya watu wasio na vyoo hujisaidia humo, kwa hali hii kipindupindu hakiepukiki, mh jitahidi sana usafi hauna gharama ni wajibu wetu
 

WanaJF wenzangu,
Nawashukuru kwa kuniunga mkono katika uchaguzi na kuniwezesha kuwa mbunge wa wote wa Jimbo la Ubungo. Tuendelee kushirikiana kutimiza wajibu katika kipindi cha mwaka 2010-2015 tukitekeleza ahadi jimboni kwa kuweka kipaumbele kwenye Akili, Ajira, Miundombinu, Maji, Uwajibikaji, Usalama, Ardhi na Afya (AMUA) kama ifuatavyo:

AKILI:
Akili na vipaji ambavyo kila mwanadamu amejaliwa ndiyo mtaji mkuu wa kujikwamua kimaisha. Kwa hiyo, tushirikiane kuwezesha elimu bora:
· Tuhakikishe ruzuku ya bajeti ya elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, inafika na kuboresha upatikanaji wa vifaa vya elimu na huduma zingine za muhimu.

· Tutumie sehemu ya fedha za mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo(CDCF) kutoa elimu maalum ya kuwawezesha wananchi kujua haki zao, fursa zilizopo na namna ya kujiendeleza, haswa kwa akina mama, vijana na walemavu. Mfano; haki za mirathi kwa wajane na kukuza vipaji kwa vijana.

· Tuendelee kupigania haki na maslahi ya wanafunzi wote wakiwemo wa elimu ya juu.

AJIRA:
· Tuwezesha kupatikana mitaji, mafunzo ya ujariliamali na kutetea wafanyabiashara na wazalishaji wadogo wadogo wawe na maeneo ya biashara.

· Tuhakikishe vitega uchumi vilivyopo kama kituo cha mabasi Ubungo, Kiwanda cha Urafiki, Songas na kituo cha kiuchumi cha “EPZ”, vinatoa ajira kwa wakazi wa jimbo la Ubungo na kuchangia miradi ya maendeleo.

· Tuchochee uwekezaji na uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo ili kupunguza hitaji la ajira hasa kwa vijana.

· Tutetee ujira bora na stahili za wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi kama walimu, manesi, polisi, madereva nk.

MIUNDO MBINU:
· Ili kupunguza msongamano katika barabara kuu, pamoja na mbinu zingine tuhakikishe barabara za pembezoni zinajengwa. Mfano: barabara ya Mbezi-Goba, Kimara-Makuburi n.k. Pia turahisishe usafiri wa maeneo ya pembezoni kwa ukarabati wa barabara na madaraja. Mfano: Golani, Mburahati Kisiwani, Msakuzi, King’ong’o, Kwembe, Makoka n.k

· Tupiganie kupunguzwa kwa gharama za kuvuta umeme kwa kujenga hoja bungeni ili gharama za nguzo na nyinginezo ziwekwe kwenye bili ya mteja kama umeme uliolipiwa. Hii itasaidia wengi kuvuta umeme kwa gharama nafuu.
MAJI:
· Tusimamie uwekaji mabomba katika maeneo yaliyorukwa na kuhakikisha DAWASCO inatimiza wajibu wake wa kuhakikisha maji yanatoka wakati wote.

· Tuhamasishe ujenzi wa visima kwenye maeneo ambayo hayafikiki kirahisi na mtandao wa maji ya bomba kama suluhisho la muda, huku tukifuatilia ufumbuzi wa kudumu katika maeneo hayo.

· Tuhakikishe bei ya maji inayotozwa kwenye Viosk inaendana na viwango vilivyopangwa na mamlaka husika (EWURA).
UWAJIBIKAJI:
· Tupambane na ufisadi kwenye Halmashauri na kuhakikisha fedha nyingi zinazopatikana kila mwaka zinatumika kuwahudumia wananchi, ikiwemo kushughulikia mapungufu yaliyoanishwa na mkaguzi mkuu wa serikali katika vipindi vilivyopita.

· Tuhamasishe wafadhili wa ndani na nje ya nchi kuchangia fedha na rasilimali nyingine za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakazi wa Ubungo.

· Tufungue ofisi mbili za Mbunge wa Jimbo la Ubungo, ili kila ofisi ihudumie kata saba. Hii itasaidia wananchi kukutana kwa urahisi na mbunge wao kabla ya kwenda kuwawakilisha kwenye vikao vya bunge.

· Tuzisimamie mamlaka za serikali kutekeleza wajibu wake, mathalani EWURA katika nishati/mafuta, SUMATRA katika usafiri, TANESCO katika umeme, TBS katika ubora wa bidhaa nk

USALAMA:
· Tuhamasishe ujenzi wa vituo vya polisi katika maeneo yasiyokuwa na vituo kama Goba na kupanua vituo vya polisi vilivyopo ili kuviongezea uwezo na hadhi katika kuwahudumia wananchi.

· Tushirikiane polisi na viongozi wa kata/mitaa kuhakikisha doria inakuwepo ili kupunguza vitendo vya wizi, ukabaji na ujambazi hususani kwenye maeneo yenye vitendo vingi vya uhalifu
ARDHI:
· Tuhakikishe wananchi wanapewa fidia wanazostahili katika maeneo yote yenye migogoro ya ardhi kama Kwembe,Kibamba,Ubungo Maziwa n.k

· Tuhakikishe viwanja vya umma vilivyouzwa kinyemela na viwanja vya wazi vilivyovamiwa, vinarejeshwa. Mfano: viwanja vya Makurumla, Sinza, Ubungo, Makuburi, Mbezi nk.

· Tusimamie mpangilio mzuri wa makazi na kuhamasisha upimaji wa viwanja ili wananchi wapate hati na leseni za makazi kwa urahisi na kwa bei nafuu.
AFYA:
· Tuhakikishe wanaoishi na UKIMWI/VVU, Wazee, Walemavu na wagonjwa wa kifua kikuu, wanapata huduma za matibabu kwa wakati na kwa fedha za serikali na wadau wengine wa maendeleo.

· Tusimamie vizuri fedha za bajeti ya afya kwa kuhakikisha zinatumika kuboresha huduma katika zahanati za kata na hospitali ya Mwananyamala inayohudumia pia wakazi wa jimbo la Ubungo.

· Tupiganie ujenzi wa zahanati mpya kwenye uhaba wa zahanati.

Inawezekana, Ungana nami -Shiriki Sasa!!



Hongera sana Mhe. Mnyika, makucha yako tumeyaona wakati wa uteuzi wa Pinda, endelea kijana mwenzetu, tuko nyuma yako, tunakuamini.
 
Mh.Mbunge,
Kwanza shukrani kwa kurejea na kutujulia hali. Pili hongera sana kwa kuingia mjengoni. Somo la muhimu hapa ni uvumilivu. Miaka 5 iliyopita ulichakachuliwa lakini ukawa na subira ukiamini kuwa dhamira yako ni kuwatumikia wananchi na si umaarufu wala kipato. Dua zako amezijibu muumba nawe una mzigo mzito mbele yake na wapiga kura wako.
Wewe ni mbunge wa jimbo la wasomi na wajanja, hawa hawakubahatisha bali walijua wanataka nini. Kwanza kabisa, nakushauri uwe karibu na wapiga kura wako. Watembeleee katika nyumba kumi zao na vijiwe vyao ili uzijue shida zao. Usipoteze muda mwingi kwenye kamati za bunge ambazo hazikukuchagua. Pili, Simamia kile unachokiamini kwa dhati, kama ni mradi basi usimamie kwa hekima na nguvu zako. Sema wazi usiogope maana CCM watakukwaza ili wapate sababu. Waambie wapiga kura wako mnataka mfanye nini, kwanini na manakwama wapi.
Una bahati upo jimbo la wasomi, si tu watakushauri bali pia watakusaidia.
Pili, shughulikia kero za kawaida za wananchi, watu wa goba hawahitaji maghorofa, wanataka daraja la kuvuka mvua ikinyesha.
Tatu, bungeni wewe na wenzako muwe kitu kimoja, vunje makundi yanayoanza kujitokeza mkijua kuwa uwepo wenu bungeni ni mtihani na si mazoea kama wenzenu wa CCM.
Jengeni hoja hata kama zitazuiliwa na yule mama aliyetumwa na mafisadi, sisi wananchi ni wasikivu, Tanzania ya leo si ya jana. Ukifukuzwa bungeni kwa kukemea wizi na uhalifu wa genge la wale watu wasiozidi 10 wanaolitafuna taifa, sisi tutakupokea chalinze uje tuijenge nchi.
Mwisho, waambie wenzako akina Halima, Regia, Zitto, n.k ninyi ni taswira ya nini watanzania watarajie 2015. Uwepo wenu bungeni uwe chachu na hamasa kwa umma ili kufungua njia kwa wajao. Umma unawaangalia kwa macho mawili mkumbuke. Akijipaka kinyesi mbunge wa kijani hiyo itaitwa mfadhaiko wa akili, akipiga chafya wa chadema hiyo ni habari tena ya kashfa.
Enendeni kwa amani mkawatumikie waishio kwa dola 1 kwa siku, wanaofunga Kwaresima au Ramadhani kila siku! kwasababu wanaishi chini ya mstari mwekundu.
 
Siyo kuwatega, wao wenyewe ndio wamelisema hili kama issue, sasa nataka watuonyeshe tu kwamba wako serious na wanaposema sio wanasema kwa ulaghai wa kisiasa bali kwa ukweli wa dhamira zao.
Punguza hasira, jipangeni 2015 kulirudisha jimbo
 
hongera sana mheshimiwa john mnyika. ulipata ushindi mzuri na wa kujivunia na umeanza vizuri kazi uliyopewa. mimi pia ni mmoja wa wakazi wa jimbo lako kwani nina makazi kimara na muda mwingi familia yangu inaishi huko, kwa hiyo wewe ni mbunge wangu na ninaona fahari kuwa na mbunge kijana, mbunifu, mwepesi na mchapakazi. nitaangalia baadaye uwezekano wa kufahamiana na wewe kibinafsi ili kama lipo la kushirikiana na kushikana mikono, basi tufanye hivyo kwa manufaa ya wananchi wakazi wa eneo letu na taifa kwa ujumla.

nakutakia kila la heri katika utumishi wako. Mungu akutangulie na daima maslahi ya taifa yakae mbele

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
nianze kwa salamu yetu...TANZANIA OYEEE....TANZANIA JUU...JUU...JUUU ZAIDI...! mimi ni miongoni mwa wakazi wa jimbo ka ubungo ambao ni miongoni mwa niliokupa kura yangu moja tu. japo nafasi hiyo angesimama NAPE kura yangu moja ningempa yeye.
nimesoma na kuelewa vyema vipaumbele vye jimbo la ubungo....mimi naendelea kusema ni sahihi na havijakaa kiubaguzi wala ki-maslahi ya chama...... pambana katika kutetea wananchi oycome yake itaonekana... BIG UP DOGO KEEP FIGHTING...!
nice gesture mwanaCHECHEMEE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom