Ujumbe Wa Maalim Seif Shariff Hamad Kwa Wazanzibar

Kama miaka 15 ya mfumo wa vyama vingi Maalim Seif kawa hana mpya, vp chama chetu kitukufu cha Mapinduzi(CCM) katka miaka zaidi ya 40 ya utawala wake,kuna lolote la kujisifia kwa mwananchi wa kawaida, mlala hoi bin miguu juu kama mm?(sjuwi ww mwenzangu)

Kwa hiyo mkuu tunaangali whose worse and whose the worst? Kama nae miaka 15 hajafanya kitu tutajuaje hiyo miaka 40 akipewa atafanya chochote. Sina ubaya na Maalim ila naona hoja uliyotoa haina nguvu. Mtazamo wangu tu.
 
Recruitment policy ikoje huko CUF! leteni vijana tuwaone majukwaani kila seif, lipumba duni...tumeanza kuchoka na majina...unajua mambo mengine unaweza ku-determine msimamo wa kila moja wa hawa jamaa jukwaani kuhusu issue yeyote?
tunataka kusikia vijana na majina mengine
 
Maalim Seif anamtaka Rais Kikwete asifuate nyayo za mtangulizi wake, Benjamin Mkapa, ambaye anajuilikana kwenye kama kiongozi aliyesimamia mauaji ya Januari 2001 na kuzalisha wakimbizi kwa mara ya mwanzo katika historia ya Tanzania huru
.

Hii imekaa vibaya
Anambembeleza JK, then anamponda Mr.Clean

Wazenj na waislamu wengi wametokea kumchukia sana Mr.Clean kwa yale mapigo ya zenj na m.chai

Huyu jamaa ni zero tuu, kuna lipi la kumsifia au kumshauria JK, ni wazi kuwa JK ndiye mbovu/m-baya kuliko Mr.Clean, lakini kwa kulinda misingi yao ya udini wanaona so kumkosoa JK hadharani.

Anyway, ngoja niwadokeze kidoooogo, tuuu.
Unajua ni kwanini JK hana ubavu wa kusema mbovu juu ya Mr.Clean?? Mkwara aliopigwa hatosahau maisha yake...."Akikamatwa Mkapa hii nchi lazima tumwage damu, jeshi litagawanyika, wakristu tutasimama kumtetea..."

Hahaahahahahah...give me a break
 
Duuuhhh naona pepo bado linakula akili zao

...anajulikana kwenye....!!!!!!!!!!!

Nijulize wanajamvi, anajulikana kwenye nini?(misikiti, OIC, kadhi)?
 
Maalim Seif Shariff Hamad awaachie wengine kila uchaguzi ni yeye tu haoni wenza Mbowe,Cheyo na Mzee wa Kiraracha wamekimbilia kwenye majimbo yao uchaguzi.
Sioni kama hawa ni mifano mizuri, mimi ningewapa credit mzee Edwin Mtei, Mzee Bob Makani, kwani wao hakukimbilia kwenye urais wakati kila mtu mwaka 1995 alioona ni mwaka wa wapinzani, walisema bado wakaviunga mkono vyama vingine wakaimarisha chama chao, ndio maana Mbowe aliweza kupata kura zote zile mwaka 2005, na ndio maana CHADEMA wananafasi nzuri sana sasa hizi ya kufika fainali. Mbowe hawezi kutajwa hapa hajaachia bado unaweza ukamuona kwenye urais 2010 au ndio kampeni za CCM kumsukuma aende jimboni? (janja ya nyani)
 
Kwa hiyo mkuu tunaangali whose worse and whose the worst? Kama nae miaka 15 hajafanya kitu tutajuaje hiyo miaka 40 akipewa atafanya chochote. Sina ubaya na Maalim ila naona hoja uliyotoa haina nguvu. Mtazamo wangu tu.
Hoja ilitolewa na mchangiaji mmoja kuwa "Maalim hana mpya bora agombee ubunge..." Lakini mchangiaji kashindwa kuona kuwa kipindi anachokizungumzia cha Maalim akiwa kama kiongozi wa chama cha Upinzani ni muda wa miaka kama 15 tu, utawezaje kumhukumu kwa kipindi kifupi cha siasa za upinzani zenye mashaka na vitimbi chungu nzima, katika serikali inayoongozwa na chama chenye historia ya mateso, vitisho na mauwaji dhidi ya wapinzani wake, na licha ya mfumo wa vyama vingi mambo hayajabadlika sana vitimbi hivyo(mifano ipo ukitaka). Licha ya hayo muda mfupi tu wa Maalimu kuongoza upinzani Zanzibar mafanikio ya msingi mengi yamepatikana kwa mfano:
1. Mabadiliko ya Katiba kutokana na Muafaka(1999) yaliyopelekea kuanzishwa kwa taasisi kadhaa za kutoa haki kwa wananchi kama vile Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) ambayo inaendesha kesi zote za jinai ambazo awali zilikuwa zikiendeshwa na Polisi, waliokuwa wakibambikia watu kesi ovyo ovyo tu,

2. Kubwa zaidi kurejeshwa kazini wafanyakazi waliofukuzwa kwa sababu za kisiasa ama kulipwa haki zao,

3.Uanzishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,

4.Uthubutu wa Maalimu kusema waziwazi uozo wa serikali na chama tawala umeamsha ari na mwamko mpya wa kimageuzi kwa wazanzibari na hasa vijana ambao awali walidanganywa kuwa " vyama vya upinzani vimekuja kuvuruga amani na utulivu na kumrejesha Sultani" kitu ambacho ni uongo.

Mambo ni mengi na sitaki kuchukuwa nafasi na muda wako lakini kwa ufupi tu nikuwa kama haya kayafanya kwa kipindi kifupi tu kama mpinzani "imagine" akipata serikali umbali gani atafika kuleta mabadiliko ya kiuchumi kisiasa na kijamii kwa ujumla, na pengine hata hiyo miaka 40 isifike.
Ukitizama kwa mizania kama hiyo utaona kuwa miaka 40 ya CCM madarakani tofauti na 15 ya CUF kama chama cha upinzani kwa mengi tu.
 
.

Hii imekaa vibaya
Anambembeleza JK, then anamponda Mr.Clean

Wazenj na waislamu wengi wametokea kumchukia sana Mr.Clean kwa yale mapigo ya zenj na m.chai

Huyu jamaa ni zero tuu, kuna lipi la kumsifia au kumshauria JK, ni wazi kuwa JK ndiye mbovu/m-baya kuliko Mr.Clean, lakini kwa kulinda misingi yao ya udini wanaona so kumkosoa JK hadharani.

Anyway, ngoja niwadokeze kidoooogo, tuuu.
Unajua ni kwanini JK hana ubavu wa kusema mbovu juu ya Mr.Clean?? Mkwara aliopigwa hatosahau maisha yake...."Akikamatwa Mkapa hii nchi lazima tumwage damu, jeshi litagawanyika, wakristu tutasimama kumtetea..."

Hahaahahahahah...give me a break
This is treasonous!!!
 
Recruitment policy ikoje huko CUF! leteni vijana tuwaone majukwaani kila seif, lipumba duni...tumeanza kuchoka na majina...unajua mambo mengine unaweza ku-determine msimamo wa kila moja wa hawa jamaa jukwaani kuhusu issue yeyote?
tunataka kusikia vijana na majina mengine
Vijana wa CUF wapo, wanakomazwa bado wakitolewa ukumbini ni kama Paka vile anapoingia katika kichaka cha panya(CCM), hakuna haraka wamewekwa katika maeneo (strategically) ili wajifunze kutoka kwa magwiji ambao bado wana nguvu zao.
 
.

Hii imekaa vibaya
Anambembeleza JK, then anamponda Mr.Clean

Wazenj na waislamu wengi wametokea kumchukia sana Mr.Clean kwa yale mapigo ya zenj na m.chai

Huyu jamaa ni zero tuu, kuna lipi la kumsifia au kumshauria JK, ni wazi kuwa JK ndiye mbovu/m-baya kuliko Mr.Clean, lakini kwa kulinda misingi yao ya udini wanaona so kumkosoa JK hadharani.

Anyway, ngoja niwadokeze kidoooogo, tuuu.
Unajua ni kwanini JK hana ubavu wa kusema mbovu juu ya Mr.Clean?? Mkwara aliopigwa hatosahau maisha yake...."Akikamatwa Mkapa hii nchi lazima tumwage damu, jeshi litagawanyika, wakristu tutasimama kumtetea..."

Hahaahahahahah...give me a break

Mzee haijakaa vizuri, wakristo wengi hawatakussuport kwenye hii, you need a fair warning! Matamshi kama yako ni hatari kama tutayaendekeza sio hapa tu mahali popote pale ndani ya TZ huru tunayoitaka ijali haki za binadamu na ifuate utawala washeria. PLS Futa maneno yako
 
.

Hii imekaa vibaya
Anambembeleza JK, then anamponda Mr.Clean

Wazenj na waislamu wengi wametokea kumchukia sana Mr.Clean kwa yale mapigo ya zenj na m.chai

Huyu jamaa ni zero tuu, kuna lipi la kumsifia au kumshauria JK, ni wazi kuwa JK ndiye mbovu/m-baya kuliko Mr.Clean, lakini kwa kulinda misingi yao ya udini wanaona so kumkosoa JK hadharani.

Anyway, ngoja niwadokeze kidoooogo, tuuu.
Unajua ni kwanini JK hana ubavu wa kusema mbovu juu ya Mr.Clean?? Mkwara aliopigwa hatosahau maisha yake...."Akikamatwa Mkapa hii nchi lazima tumwage damu, jeshi litagawanyika, wakristu tutasimama kumtetea..."

Hahaahahahahah...give me a break

Wakristo wapi hao? Mimi Mkristo na siwezi kutetea ujinga kama huo. Siwezi kutetea maovu ya mtu kisa tuna dini moja.
 
Hoja ilitolewa na mchangiaji mmoja kuwa "Maalim hana mpya bora agombee ubunge..." Lakini mchangiaji kashindwa kuona kuwa kipindi anachokizungumzia cha Maalim akiwa kama kiongozi wa chama cha Upinzani ni muda wa miaka kama 15 tu, utawezaje kumhukumu kwa kipindi kifupi cha siasa za upinzani zenye mashaka na vitimbi chungu nzima, katika serikali inayoongozwa na chama chenye historia ya mateso, vitisho na mauwaji dhidi ya wapinzani wake, na licha ya mfumo wa vyama vingi mambo hayajabadlika sana vitimbi hivyo(mifano ipo ukitaka). Licha ya hayo muda mfupi tu wa Maalimu kuongoza upinzani Zanzibar mafanikio ya msingi mengi yamepatikana kwa mfano:
1. Mabadiliko ya Katiba kutokana na Muafaka(1999) yaliyopelekea kuanzishwa kwa taasisi kadhaa za kutoa haki kwa wananchi kama vile Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) ambayo inaendesha kesi zote za jinai ambazo awali zilikuwa zikiendeshwa na Polisi, waliokuwa wakibambikia watu kesi ovyo ovyo tu,

2. Kubwa zaidi kurejeshwa kazini wafanyakazi waliofukuzwa kwa sababu za kisiasa ama kulipwa haki zao,

3.Uanzishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,

4.Uthubutu wa Maalimu kusema waziwazi uozo wa serikali na chama tawala umeamsha ari na mwamko mpya wa kimageuzi kwa wazanzibari na hasa vijana ambao awali walidanganywa kuwa " vyama vya upinzani vimekuja kuvuruga amani na utulivu na kumrejesha Sultani" kitu ambacho ni uongo.

Mambo ni mengi na sitaki kuchukuwa nafasi na muda wako lakini kwa ufupi tu nikuwa kama haya kayafanya kwa kipindi kifupi tu kama mpinzani "imagine" akipata serikali umbali gani atafika kuleta mabadiliko ya kiuchumi kisiasa na kijamii kwa ujumla, na pengine hata hiyo miaka 40 isifike.
Ukitizama kwa mizania kama hiyo utaona kuwa miaka 40 ya CCM madarakani tofauti na 15 ya CUF kama chama cha upinzani kwa mengi tu.

Mkuu hizi ndiyo hoja za kutoa. Unataja mafanikio yake.
 
Aagh huyu Ba Hamad hana mpya hata mimi sina tatizo na cuf, tatizo ni huyu jamaa. Hivi zbar hakuna chama cha tatu chenye nguvu!
Imani uliyo nayo ni udhaifu na choyo hakuna jingine,mna roho dhaifu binadamu kumchukia binadamu mwenzake bila ya sababu za msingi binadamu huyo anakuwa ni mtu duni mwenye moyo uliojaa chuki.

Chama Cha CUF ni Chama chenye waasisi Seif akiwa mmoja wao ,sasa huwezi ukasema unamchukia muasisi ukakipenda kilichoasisiwa itakuwa unajidanganya,tafuta pengine au unda chama chako ,ikiwa taratibu za kuwepo hapo alipo amezifuata na kushinda basi ukimlaumu utakuwa humtendei haki ,na zaidi ikiwa yeye mwenyewe binafsi anapenda kuwepo hapo alipo na anapenda kugombea Uraisi basi hiyo ni haki yake kikatiba na kichama na zaidi ya zaidi ikiwa bado wananchi walio wengi wana imani nae hakuna sababu ya yeye kutoendelea kuwania Uraisi.

Tatizo Seif hamlazii yeyote yule na humhujumu kisiasa yeyote yule ambae anawafanyia watu mizengwe kwa kiswahili sanifu panasemwa hamlazii mtu damu na hilo ndilo linalowapa shida CCM.

Seif anajaribu kuilaza hali ya watu wa Pemba kutaka kujitenga ndipo hapo aliposema waandikisheni wananchi msiwawache ,unamkosesha mtu kujiandikisha katika kupata cheti cha uraia unategemea nini ,maana nionavyo hapo pana mtego ikiwa watakaokataliwa watafika laki basi hata walioandikishwa nao watajiunga nao na kuzidi kupeleka hati za madai kunakohusika juu ya madai ya kuwepo kwa Taifa la Pemba ,au hamlioni hilo ?
 
Maalim Seif - Hongera kwa msimamo wako. Katika wanasiasa wenye Msimamo, Maalim Seif yupo juu sana. Maalim anakubalika kabisa kama kiongozi mwenye kauli ya kweli na mwenye imani na taifa lake. Nyinyio wengine muna chuki tu kwakuwa ni mtu mwenye mwanga wa kuoina maovu ya utawala wa CCM.
 
Seif Shariff Hamad,

Nakubaliana na ujumbe na harakati zako kwa Wazanzibari, ila ujumbe wako kwa Kikwete kuhusu uchimbaji wa mafuta ya Zanzibar unaonyesha kutokuelewa need for integration of tiny economies like that Z'bar.

Hivi J.K. aka-respond kwa kuwaambia TANESCO wa-switch off umeme to Z'bar, si utashindwa hata kuendelea na kampeni zako kwa ufanisi?
 
VP na Wazanzibari nao waki respond na kwa kuamua sasa bas, tunaungana na marafiki wengine(Kenya) au USA, bakini na umeme wenu, itakuwaje?
 
Nahisi Mwiba umelewa tende! Ukitaka kuwajua wengi wapemba watajie Ba Hamad.Watajitokeza kila kona na ubaguzi wao, tunayaona huku nchi za nje!
 
Maalim Seif Shariff Hamad awaachie wengine kila uchaguzi ni yeye tu haoni wenza Mbowe,Cheyo na Mzee wa Kiraracha wamekimbilia kwenye majimbo yao uchaguzi.Maalimu Seif badala ya kuimarisha CUF bara kaamua kubaki na Pemba yake !!!.Ndiyo maana Lwakatare kawakimbia baada ya kubaini hyiki chama macho na masikio yako Zanzibar tu.

Maalim Seif Shariff Hamad hajui mafuta ni mambo ya muungano na yataendelea kuwa ya muungano atake asitake.Lau kama anataka kubadili katiba sharti hoja ilepelekwe bungeni si Gombani au Chake chake.

Maalim Seif Shariff Hamad na Ibrahim Lipumba maadamu wanakubaliwa kugombea Urais wa Zanzibar na Tanzania na wanachama wao wa CUF kwa mujibu wa katiba ya chama chao,
wana haki ya msingi ya kugombea nafasi hiyo kwa miaka 26 na zaidi. Haki hii hata Julius Nyerere alikuwa nayo katika TANU na CCM pia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom