Ujumbe kwa wanandoa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
Je, wanandoa wote tungekuwa tupo makini (maombi) mara zote kiasi hiki ingekuwaje?

kitadani.bmp


Mzuri kitandani?
Tunapooana kama wanandoa tunakubaliana kwamba tutakuwa tunafanya tendo la ndoa sisi wawili tu maisha yetu yote (monopoly) haijalishi tunafanya kwa kufikiria, au kwa kutofikiria, au tunafanya bora liende au kwa ufanisi, tunfanya kwa kupenda au kulazimishwa, tunafanya kwa ubunifu au kwa uchoyo au kwa kubania au kwa hiari au vyovyote vile kitabu kimefungwa na lazima kila mmoja apate kile mwenzake anampa iwe nusu au kitu kizima au kunyimwa kabisa au kupewa kila ukihitaji.

Hakuna kuangalia kushoto wala kulia ngoma ni ninyi wawili tu kuicheza hadi kifo kitakapowatenganisha.

Ukweli wengi wetu huwa tunachukua kila kitu for granted, hakuna efforts zozote tunaweza kuziwekeza kuhakikisha mwenzako anapata the best kutoka kwako hasa linapokuja suala la tendo la ndoa kwani ni wewe tu ndiye mwanamke au mwanaume duniani ambaye amekubali kuishi na wewe na kushirikiana kupeana hiyo zawadi ya mwili ambayo ni mali ya ndoa yenu na sivinginevyo.

Naomba ujiulize ndani ya moyo wako tena ukiwa na akili nzuri kabisa kama Mungu alivyokujalia kuoana na mwanaume au mwanamke special kama huyo uliyenaye.

Je, ni kweli unataka leo kumbariki mke wako au mume wako kwa mwili wako kwa kuwa hakuna kwingine anaweza kupata hii huduma?
Je, una hamu ya kumpa kitu cha uhakika (mapenzi, mahaba) kwa sababu ya jinsi anavyokupenda, anavyokujali na jinsi alivyoshirikiana na wewe hadi hapa mmefika?


Au umefika mahali umechoka, huna hamu tena ya kuhakikisha mume wako anapata kila mlikubaliana wakati mnaoana?
Au unasubiri hadi umpoteze ndipo ujue thamani yake?

Je unajua huko nje ya ndoa yako kuna wanawake au wanaume wengi kiasi gani wanamtamani sana huyo mume wako au mke wako?

Je, kwa nini huweki juhudi yoyote kuhakikisha kitanda chenu kinakuwa mahali bora kukimbilia kama mke na mume?

Sex ni mali ya ndoa na ndivyo Mungu alivyo design, hivyo kama upo kwenye ndoa ina maana suala la tendo la ndo lisichukuliwa just for granted, panga, andaa na wekeza kwa uwezo wako wote kuhakikisha mke wako au mume wako anaridhika na wewe na utendaji wako.

Kumbuka Bibilia inasema:
“Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote.
Waebrania 13:4

 
Hii habari njema kabisa kwa kila mwanandoa! Ila sijajua ni kwa nini habari hii ni maalum kwa Sofia Simba!
 
Una maana kwamba Sophia Simba hajui masharti ya ndoa ni nini? Au amekiuka masharti ya ndoa,au ameolewa na mtu mmoja,lakini anafanya mambo ya kumpendeza mtu mwingine.?

Basi,labda Sohia Simna atasoma haya halafu atafanya mambo ya kuimarisha ndoa yake,na kuacha kumtazama mwanaume mwingine zaidi ya mume wake wa ndoa. Kwani Sophia Simba ameolewa na nani? Kwa sababu huyu mume wake hatafurahi kuona Sophia Simba anakosa uaminifu,tena mbele ya kadamnasi.
 
Watu ni lazima waongee kwa uwazi zaidi,ama sivyo decisions are made before all the facts have been revealed.
 
Hii ni post ya kwenye udaku au haina mahali kabisa. Hapa si mahali pake. Maana title na content havifanani. Unless title iwe edited
 
alikua anajaribu kuweka attention!, coz huyu mwanamama anauza sana magazeti within these two weeks
 
mtabiri...elia alitabiri mengi sana...naona ulichoandika kama ulikuwepo na mimi...ubarikiwe g-porjie

hahaaaaaa, duh. ulinitisha mkuu!.
anyways mwanamama kaboa sana utulivu wa nchi, imagine NDIO UTAWALA BORA kweli huo?, Loh.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom