Ujumbe alioutuma Mh. Selasini muda mfupi kabla hajapata ajali Bomang'ombe

Tuangalie ni mua gani ametumia kuyafanya hayo aloyafanya na je anamuda gani mbele kuyafanya yajayo na c kujadili mickit na makanisa
 
Pole sana Mheshimiwa Mbunge wetu. Mungu akupe nguvu.

Mimi ni Mhorombo, na najua kwamba unachofanya ndicho haswa wanachotaka asilimia 99.9 ya watu wa Rombo. Mbunge anapashwa kusaidia kile wanachotaka wananchi wake, na si vinginevyo.

Lazima nisahihishe kitu kimoja. Wengi hapa wansema ajali ilikuwa “mpango wa Mungu”. Not so. Mungu hapangii mtu ajali. Anaona yote yatakaoyotokea lakini hiyo haimaanishi anatupangia mabaya. Anayajumuisha tu kwenye mipango yake. Ni kama mzazi ukiona mtoto anazembea shuleni na ukajua, ahead of time, kwamba atafeli, na ukajumuisha hilo kwenye mipango yako ya mwanao. Haina maana umepanga afeli.

Mungu ni UPENDO. Mtu akipata ajali sio mpango wa Mungu. Nimeona niseme hilo kwani ni kosa linalofanywa na wengi.

Chadomo kina udini,iwe ni hisia au ndo sera yenu kuegemea ukristu,kwanza mjitakase na hili kwani hata matendo yenu yanaonyesha, na kwa jinsi mlivyo mjue kwamba mna hallucinate tu kuingia ikulu,TANZANIA YA LEO UONGOZI UNAPIMWA KWA KUGAWA MISAADA BADALA YA UWEZO WA KUHAMASISHA WATU KUJILETEA MAENDELEO
 
Lazima nisahihishe kitu kimoja. Wengi hapa wansema ajali ilikuwa "mpango wa Mungu". Not so. Mungu hapangii mtu ajali. Anaona yote yatakaoyotokea lakini hiyo haimaanishi anatupangia mabaya. Anayajumuisha tu kwenye mipango yake.
Nani mwingine ambae anapanga halafu Mungu "anajumuisha kwenye mipango yake," shetani? Na kama ajali haikuwa mpango wa Mungu ni nini ilikuwa mpango wake na ni nani aliyevuruga mipango ya Mungu? Au Mungu hakuwa na mpango wowote na safari hii siku hiyo? Ina maana Mungu hapangi kila kitu, au? Na kama "Mungu anaona yote yatakayotokea" na "Mungu ni Upendo" kwa nini hakuzuia haya maafa?

Hakuna mpango wa mtu wala Mungu-Mtu hapa, ajali imetokea kwa sababu tairi limepasuka, period. Tairi limepasuka kwa sababu 1) tairi lilikuwa limepita muda wa matumizi, au 2) manufacturing defect, au 3) uzembe wa kutumia matairi ya technolojia ya zamani ya tube ambayo ikitoboka inalipuka kama unavyotoboa puto!

Wengine wamefariki wengine wamepona kwa sababu tumeambiwa Mheshimiwa kiongozi alikuwa amefunga mkanda lakini bahati mbaya hakumuongoza Mama yake kufunga mkanda! Ni vitu vinavyoelezeka kwa akili ya kawaida kabisa kabisa. Uzembe wa kutisha na, au, matatizo ya kiufundi.
 
Huyu jamaa ni mbabaishaji. Hizi hela anazotaja ni fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo, sio zake wala hajafight kuzipata. Hata ungeweka mtoto mdogo ukampa hizo hela angegawa.
Tunamuombea Selasini apone then atuambie jimbo letu linapata sh ngapi za mfuko wa maendeleo ya jinbo, na yeye, kwa miaka hii miwili amezitumiaje...
Tunataka atuambie amefanya nini kuwasadia maelfu ya vijana wanaomaliza form four, na six...
Tunataka atuambie amefanya nini kusimamia ujenzi wa barabara za halmashauri ambazo sehemu nyingi hazipitiki...
Tunataka atuambie tatizo la maji kwa maeneo mengi ya Tarakea, na ugawaji maji unaopendelea matajri amelighulikia vipi...
Tunataka atuambie amefanya nini kukabiliana na tatizo kubwa la ukosefu wa walimu katika shule za sekondari Rombo...
Tunataka atuambie ni kwa nini performance za shule za Rombo kwenye mitihani ya form four inazidi kuwa mbovu, ana idea gani yeye kama mbunge na amefanya nini...
Tunataka atuambie emeshughulikia vipi suala la ugawaji wa mashamba maeneo ya forest kunakofanywa kibaguzi na kiupendeleo...
Tunataka atuambie ameshughulikia vipi suala la ukosefu wa madawa na magari ya wagonjwa katika vituo vya afya, useri na Tarakea...
Tunataka atuambie anafanya nini kusaidia tatizo la mamia ya watu walioomba umeme kwa miezi mingi sasa, wamelipa lakini hawajafungiwa, na waliofungiwa walifanikiwa baada ya kutoa rushwa nyingi sana...
Tunataka atuambie yeye kama mbunge amefanya nini kuwasaidia maelfu ya vijana wa Rombo kufaidika na mlima Kilimanjaro tofauti na sasa ambapo wanaofaidika kwa kiasi kikubwa ni wa wilaya nyingine...

Selasini kiukweli amekuwa mzigo kwa Wanarombo, na kama nilivyokwisha sema humu JF tangu mwaka jana, asipojirekebisha, asipokuwa karibu na wapiga kura wake akawasikiliza na kuwasaidia kupambana na adui umaskini, then ajue 2015 hana chake. Kama haamini akawaulize kina Mramba na Salakana...

Hapa ndipo mijitu inaposhindwa kujua nini majukumu ya mbunge. I hope JF mtatuletea maelezo nini wajibu wa mbunge. Mbunge ni kuisimamia serikali. Kama hakuna ajira kamuulize CCM. Yeye anaweza kufuatialia ishu za madawa na magari ya wagonjwa lkn nani anapaswa kununua? Zindukeni acheni ***** mnapochangia hoja. Tafadhali usije nisababishia ban. Nakumbuka kama mijitu mingine ilipokuwa inamsema JJM kuwa hana anachofanya wakati inaonekana kabisa jinsi anavyofuatialia. Jamani kumbukeni hela zinatoka serikalini kuja halmashauri wewe mimi wale ni vema kuhakikisha kama tumechagua upinzani basi hakikisheni mafiga yote matatu Mbunge Diwani na rais hapo ndipo waweza kuja kukilaumu au kumlaumu mbunge wa upinzani. Au kama za raisi hazitoshi hakikisheni madiwani wengi kama sio wote kwenye halmashauri watoke upinzani kama karatu walivyo fanya
 
hapana, kujenga msikit na nyumba ya imam ndo maendeleo, pia upewe tende na kibalagashia.
Rafiki sijaona kitufe cha Like, ila hii nimeipenda!
Ndugu Eddie, nani kakuambia alikosaidia kote wanaishi wakristo pekee! Acha udini na ubinafsi ndugu yangu! Tufanye kazi!
 
Huyu jamaa ni mbabaishaji. Hizi hela anazotaja ni fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo, sio zake wala hajafight kuzipata. Hata ungeweka mtoto mdogo ukampa hizo hela angegawa.
Tunamuombea Selasini apone then atuambie jimbo letu linapata sh ngapi za mfuko wa maendeleo ya jinbo, na yeye, kwa miaka hii miwili amezitumiaje...
Tunataka atuambie amefanya nini kuwasadia maelfu ya vijana wanaomaliza form four, na six...
Tunataka atuambie amefanya nini kusimamia ujenzi wa barabara za halmashauri ambazo sehemu nyingi hazipitiki...
Tunataka atuambie tatizo la maji kwa maeneo mengi ya Tarakea, na ugawaji maji unaopendelea matajri amelighulikia vipi...
Tunataka atuambie amefanya nini kukabiliana na tatizo kubwa la ukosefu wa walimu katika shule za sekondari Rombo...
Tunataka atuambie ni kwa nini performance za shule za Rombo kwenye mitihani ya form four inazidi kuwa mbovu, ana idea gani yeye kama mbunge na amefanya nini...
Tunataka atuambie emeshughulikia vipi suala la ugawaji wa mashamba maeneo ya forest kunakofanywa kibaguzi na kiupendeleo...
Tunataka atuambie ameshughulikia vipi suala la ukosefu wa madawa na magari ya wagonjwa katika vituo vya afya, useri na Tarakea...
Tunataka atuambie anafanya nini kusaidia tatizo la mamia ya watu walioomba umeme kwa miezi mingi sasa, wamelipa lakini hawajafungiwa, na waliofungiwa walifanikiwa baada ya kutoa rushwa nyingi sana...
Tunataka atuambie yeye kama mbunge amefanya nini kuwasaidia maelfu ya vijana wa Rombo kufaidika na mlima Kilimanjaro tofauti na sasa ambapo wanaofaidika kwa kiasi kikubwa ni wa wilaya nyingine...

Selasini kiukweli amekuwa mzigo kwa Wanarombo, na kama nilivyokwisha sema humu JF tangu mwaka jana, asipojirekebisha, asipokuwa karibu na wapiga kura wake akawasikiliza na kuwasaidia kupambana na adui umaskini, then ajue 2015 hana chake. Kama haamini akawaulize kina Mramba na Salakana...

Kwa hakika haya ni baadhi tu ya matarajio ya wapiga kura wako mheshimiwa, hebu jaribu kuyafikiria - Yako mengi sana ila ni muhimu sana kila unapopanga vipaumbele vyako ukakumbuka kuwapa darasa wananchi wako wajue kabisa kwamba huwezi kutatua matatizo yote kwa wakati mmoja lakini kumbuka pia matatizo mengine ya wananchi yanatatuliwa kwa kuwawezesha ili wazalishe na kuinua vipato vyao na sio kuwagawia HARD-CASH hata kama ni za ujenzi wa nyumba za Mapadre.
 
Back
Top Bottom