Huyo Mbunge aoneshe hizo fedha anazitowa wapi na analipa kodi kiasi gani.
kawaulize TRA
Huyo Mbunge aoneshe hizo fedha anazitowa wapi na analipa kodi kiasi gani.
Huyu jamaa ni mbabaishaji. Hizi hela anazotaja ni fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo, sio zake wala hajafight kuzipata. Hata ungeweka mtoto mdogo ukampa hizo hela angegawa.
Tunamuombea Selasini apone then atuambie jimbo letu linapata sh ngapi za mfuko wa maendeleo ya jinbo, na yeye, kwa miaka hii miwili amezitumiaje...
Tunataka atuambie amefanya nini kuwasadia maelfu ya vijana wanaomaliza form four, na six...
Tunataka atuambie amefanya nini kusimamia ujenzi wa barabara za halmashauri ambazo sehemu nyingi hazipitiki...
Tunataka atuambie tatizo la maji kwa maeneo mengi ya Tarakea, na ugawaji maji unaopendelea matajri amelighulikia vipi...
Tunataka atuambie amefanya nini kukabiliana na tatizo kubwa la ukosefu wa walimu katika shule za sekondari Rombo...
Tunataka atuambie ni kwa nini performance za shule za Rombo kwenye mitihani ya form four inazidi kuwa mbovu, ana idea gani yeye kama mbunge na amefanya nini...
Tunataka atuambie emeshughulikia vipi suala la ugawaji wa mashamba maeneo ya forest kunakofanywa kibaguzi na kiupendeleo...
Tunataka atuambie ameshughulikia vipi suala la ukosefu wa madawa na magari ya wagonjwa katika vituo vya afya, useri na Tarakea...
Tunataka atuambie anafanya nini kusaidia tatizo la mamia ya watu walioomba umeme kwa miezi mingi sasa, wamelipa lakini hawajafungiwa, na waliofungiwa walifanikiwa baada ya kutoa rushwa nyingi sana...
Tunataka atuambie yeye kama mbunge amefanya nini kuwasaidia maelfu ya vijana wa Rombo kufaidika na mlima Kilimanjaro tofauti na sasa ambapo wanaofaidika kwa kiasi kikubwa ni wa wilaya nyingine...
Selasini kiukweli amekuwa mzigo kwa Wanarombo, na kama nilivyokwisha sema humu JF tangu mwaka jana, asipojirekebisha, asipokuwa karibu na wapiga kura wake akawasikiliza na kuwasaidia kupambana na adui umaskini, then ajue 2015 hana chake. Kama haamini akawaulize kina Mramba na Salakana...
Mringo hivi unaweza kunikumbusha ni lini Lowasa alikuwa anaendesha harambee za kujenga misikiti? au labda mimi sielewi kwamba misaada inatolewa bila kuombwa!!....i mis some point here.CHADEMA inawakati mgumu sana kujivua na dhana ya udini...ukabila naweza nikawatetea ila udini bado wanasafari ndefu....Mimi nipo nanyi lakini jitahidini...iweje mbunge anadiriki kutoa orodha ndeefu yenye misaada mingi ktk taasisi za dini ya kikristo pekee...Kumbukeni munahitajika kuwa makini muache udini ili mukubalike kwa waislamu...hii itawasaidia ktk harakati za kuingia ikulu 2015..
18. Kwaya ya KKT Mkuu 600,000
19. Huruma Convent 2Million (Ukarabati wa mabwawa ya kufugia Samaki)
20. Tumaini Center 2Million (Msaada kwa Watoto Yatima)
25. Parokia ya Mkuu 1Million (Mchango wa Ujenzi nyumba za mapadre)
33. Parokia ya Mahida 1Million (Ujenzi wa nyumba ya mapadri)
Ubunge ni kugawa hela?
jamaa amewezaje kufanya yote haya kwa muda huu mfupi? Big up sana.jamaa ni jembe la ukweli, imani yangu ni kubwa kwa mungu kuwa selasini atapona na kuendeleza harakati za kuingamiza ccm na hila zake zote!!!!
mungu amlinde apone haraka na waliotangulia mbele ya haki mungu awape njia ya amani huko mbinguni.
Mbona hakuna msaada kwenye msikiti, nyumba ya Imam nk? huyu ni mdini kama Chadema wenzie tu Mwenyezimungu amhukumu anachostahiki
Vyombo vya habari ni mhimu sana duniani....
Huu ni upuuzi!