Ujumbe alioutuma Mh. Selasini muda mfupi kabla hajapata ajali Bomang'ombe

Mkuu Eddie kuupataa msikiti Rombo ni sawa na kulipata kanisa Iraq, sioni shida kabisa hapo!Rombo nzima ina misikiti haifiki mi 5!labda uende ukawasaidie kuanzisha.
 
Last edited by a moderator:
NASIKIA KUNA BAADHI YA VIJANA WANAZUSHA KUWA SINA USHIRIKIANO NA WANANCHI WANGU NA NIKICHEZA 2015 JIMBO LITARUDI CCM!

Kwa ufupi sana naomba niandike hapa baadhi ya michango yangu kama Mbunge kwa Wananchi wangu.
1. Ndueni Sec. 2Million (Ununuzi wa computer na Printer)
2. Mbomai Sec. 2Million (Ununuzi wa Computer na Printer)
3. Tarakea Sec. 2Million (Ukarabati wa mabweni ya Wasichana)
4. Msangai S/Msingi 1Million (Ukarabati wa vyoo)
5. Kikundi cha Wajasiriamali 2.Million
6. Kijiji cha Mashima 1.5 Million (Ujenzi wa ofisi ya Kijiji)
7. Ngaleku Sec. 2Million (Uingizaji umeme)
8. Kirongo Samanga 2Million (Ujenzi wa Kituo cha Polisi)
9. Kijiji cha Samanga 1.Million (Ujenzi wa Ofisi ya Kijiji)
10. Kirachi Sec. 2Million (Ujenzi wa Jiko)
11. Kitirima Kingachi 1Million (Ujenzi wa Kituo cha Polisi)
12. Katangara Mrere 500,000/= (Kikundi cha Kinamama-MAZINGIRA)
13. Ofisi ya Kijiji Mrere 2Million (Kuezeka Ofisi)
14. Kiraeni Sec. 2Million (Ujenzi wa mabweni)
15. Bustani Sec. 2Million (Kuunganisha Maji)
16. Ugwasi Sec. 2Million (Kuunganisha Maji)
17. S/Msingi Kwangao 2Million (Ukarabati)
18. Kwaya ya KKT Mkuu 600,000
19. Huruma Convent 2Million (Ukarabati wa mabwawa ya kufugia Samaki)
20. Tumaini Center 2Million (Msaada kwa Watoto Yatima)
21. Kikundi cha Vijana na Maendeleo 1Million (Mradi wa Kufuga Kuku)
22. Kilamacho Sec. 1Million (Kuingiza Umeme)
23. Maharo S/Msingi 1Million (Umeme)
24. Makiidi Sec. 2 Million (Ujenzi wa Madarasa)
25. Parokia ya Mkuu 1Million (Mchango wa Ujenzi nyumba za mapadre)
26. Shimbili Saccos 1Million (Ujenzi wa ofisi)
27. Kwaikuru S/msingi 1Million (Ukarabati wa mitaro ya maji ya mvua)
28. Kikundi cha Wajasiriamali cha MWANGARI 2Million (Ukarabati wa mashine ya kusaga)
29. Booni Sec. (Ukarabati wa Madarasa)
30. Mamsera Sec. 1Million (Ujenzi wa madarasa)
31. mamsera Sec. 300,000 (Ujenzi wa jiko)
32. Tanya Sec. 1Million (Ujenzi wa Madarasa)
33. Parokia ya Mahida 1Million (Ujenzi wa nyumba ya mapadri)
34. Ngoyoni 2Million (Ujenzi wa Ofisi ya Kata)
35. Holili S/msingi 2Million (Ukarabati)
36. Holili 2Million (Ujenzi wa Ofisi ya Kata)
37. Olele 2Million(Ujenziwa ofisi ya kata).

Hayo ni baadhi tu ya mambo madogo madogo ambayo nimeweza kuisaidia Jamii ya WanaRombo... Mikakati yangu na Mipango ya Maendeleo nitaitoa Siku chache zijazo....

Joseph Selasini
Mb.Rombo (CHADEMA

SALA ZENU NI MUHIMU ILI AWEZE KUPONA NA KUENDELEZA GURUDUMU NA UKOMBOZI KWA WATU WA ROMBO NA WATANZANIA KWA UJUMLA.

Ujumbe huo aliuweka kwenye facebook wall yake

ukitazama kwa makini utagundua huyu mbunge wetu anawekeza kwenye elimu. Urithi wa maana kabisa unaoweza kujivunia kwa mwanao. Ana akili sana huyu Mbunge!
 
Mbona hakuna msaada kwenye msikiti, nyumba ya Imam nk? huyu ni mdini kama Chadema wenzie tu Mwenyezimungu amhukumu anachostahiki

Kuna maeneo ambayo hakuna misikiti. Muulize mtu aliyetoka jimbo la Moshi vijijini, vunjo. Vilevile kuna maeneo ambayo hakuna makanisa. Rombo ni mojawapo ya maeneo ambayo kuona msikiti ni kama kumwona kakakuona!
 
selasini ni mwongo kupindukia apone asipone kama chadema hawatamsimamisha m2 mwingine rombo itaenda kwa upinzani kuliko selasini laana za warombo hazitamwacha kwakuwahadaa wanarombo aliyoyaandika hapo juu ni mwongo mimi niko rombo. Ndo maana hata vijana wanajitokeza kutaka kuchukua jimbo maana mbunge tuliye nae si mchapa kazi.

pinga kwa hoja na mimi niko rombo ni kipengele gani alichoongopa nasi tujue
 
selasini ni mwongo kupindukia apone asipone kama chadema hawatamsimamisha m2 mwingine rombo itaenda kwa upinzani kuliko selasini laana za warombo hazitamwacha kwakuwahadaa wanarombo aliyoyaandika hapo juu ni mwongo mimi niko rombo. Ndo maana hata vijana wanajitokeza kutaka kuchukua jimbo maana mbunge tuliye nae si mchapa kazi.

pinga kwa hoja na mimi niko rombo ni kipengele gani alichoongopa nasi tujue.
 
Selasini ni mwongo kupindukia apone asipone kama chadema hawatamsimamisha m2 mwingine rombo itaenda kwa upinzani kuliko selasini laana za warombo hazitamwacha kwakuwahadaa wanarombo aliyoyaandika hapo juu ni mwongo mimi niko rombo. Ndo maana hata vijana wanajitokeza kutaka kuchukua jimbo maana mbunge tuliye nae si mchapa kazi.

Uchu wa madaraka umekukaba kama mtu aliyekabwa na kiazi! Kuchangia 55mil kwenye maendeleo bado unalalamika sio mchapakazi!? Hao wenzio wanaolifikiria jimbo la Rombo, waambie wajipange vizuri maana Mbunge wenu yupo bize kuwatumikia watu wake. Waje na hoja za msingi na sio stori za kwenye draft au maneno ya kwenye kahawa kama haya yako!
 
CHADEMA inawakati mgumu sana kujivua na dhana ya udini...ukabila naweza nikawatetea ila udini bado wanasafari ndefu....Mimi nipo nanyi lakini jitahidini...iweje mbunge anadiriki kutoa orodha ndeefu yenye misaada mingi ktk taasisi za dini ya kikristo pekee...Kumbukeni munahitajika kuwa makini muache udini ili mukubalike kwa waislamu...hii itawasaidia ktk harakati za kuingia ikulu 2015..

Mringo,
Nilikuwa Rombo mwaka jana na wenzangu tukifanya tafiti. Mwenzetu mmoja akataka kuswali Ijumaa. From Tarakea mpk Mkuu ndo tukakuta msikiti mmoja. That is more than 80 km!
Wilaya ya Rombo,ukitoa wageni....ni wakatoliki. Hata walutheri na wenzao ni wageni!
 
Jamani Selasini kuna nini kinamsibu na hizi ajali, kwenye kampeni alipata ajali akavujika mkono leo tena, ajali mbaya namwombea kwa Mungu apone haraka. Mama yake na hao wengine wapumzike kwa amani.
 
Kujitolea over 55m kwa maendeleo ya jimbo lako si jambo dogo! Get well soon Kamanda Selasini, na Pole kwa Msiba uliompata, Mungu ampe moyo wa Subira na ampatie faraja ya moyoni. Amen.

Ubunge ni kugawa hela?

Huyo Mbunge aoneshe hizo fedha anazitowa wapi na analipa kodi kiasi gani.

pinga kwa hoja na mimi niko rombo ni kipengele gani alichoongopa nasi tujue.

Huyu jamaa ni mbabaishaji. Hizi hela anazotaja ni fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo, sio zake wala hajafight kuzipata. Hata ungeweka mtoto mdogo ukampa hizo hela angegawa.
Tunamuombea Selasini apone then atuambie jimbo letu linapata sh ngapi za mfuko wa maendeleo ya jinbo, na yeye, kwa miaka hii miwili amezitumiaje...
Tunataka atuambie amefanya nini kuwasadia maelfu ya vijana wanaomaliza form four, na six...
Tunataka atuambie amefanya nini kusimamia ujenzi wa barabara za halmashauri ambazo sehemu nyingi hazipitiki...
Tunataka atuambie tatizo la maji kwa maeneo mengi ya Tarakea, na ugawaji maji unaopendelea matajri amelighulikia vipi...
Tunataka atuambie amefanya nini kukabiliana na tatizo kubwa la ukosefu wa walimu katika shule za sekondari Rombo...
Tunataka atuambie ni kwa nini performance za shule za Rombo kwenye mitihani ya form four inazidi kuwa mbovu, ana idea gani yeye kama mbunge na amefanya nini...
Tunataka atuambie emeshughulikia vipi suala la ugawaji wa mashamba maeneo ya forest kunakofanywa kibaguzi na kiupendeleo...
Tunataka atuambie ameshughulikia vipi suala la ukosefu wa madawa na magari ya wagonjwa katika vituo vya afya, useri na Tarakea...
Tunataka atuambie anafanya nini kusaidia tatizo la mamia ya watu walioomba umeme kwa miezi mingi sasa, wamelipa lakini hawajafungiwa, na waliofungiwa walifanikiwa baada ya kutoa rushwa nyingi sana...
Tunataka atuambie yeye kama mbunge amefanya nini kuwasaidia maelfu ya vijana wa Rombo kufaidika na mlima Kilimanjaro tofauti na sasa ambapo wanaofaidika kwa kiasi kikubwa ni wa wilaya nyingine...

Selasini kiukweli amekuwa mzigo kwa Wanarombo, na kama nilivyokwisha sema humu JF tangu mwaka jana, asipojirekebisha, asipokuwa karibu na wapiga kura wake akawasikiliza na kuwasaidia kupambana na adui umaskini, then ajue 2015 hana chake. Kama haamini akawaulize kina Mramba na Salakana...
 
Naona kuna juhudi za msingi mbunge huyu amefanya.kumbuka kuna mfuko wa jimbo kwa wale wanaoulizia katoa wapi pesa.huyu bora kasema ametoa pesa je wale ambao wanaliibia taifa na kuficha pesa nje ya nchi je
 
Mringo,
Nilikuwa Rombo mwaka jana na wenzangu tukifanya tafiti. Mwenzetu mmoja akataka kuswali Ijumaa. From Tarakea mpk Mkuu ndo tukakuta msikiti mmoja. That is more than 80 km!
Wilaya ya Rombo,ukitoa wageni....ni wakatoliki. Hata walutheri na wenzao ni wageni!

Acha uongo...
Tarakea mjini pale kuna msikiti mkubwa tu...
Kilimita nne kutoka Tarakea, eneo la Urauri kuna msikiti mzuri na wa siku nyingi. Recall kwamba eneo kubwa la Urauri na Msangai, wenyeji wengi ni waisalmu...
Kutoka Tarakea hadi mkuu sio km 80, ni km 30 tu na zimeandikwa...

Rombo nzima ipo misikiti zaidi ya kumi...
 
Hivi Chadema utu mmeupeleka wapi, badala ya kumpa pole mwenzenu kwa ajali na kufiwa mna jadili namna ya kuchukua jimbo lake 2015. Kama huu si unyama ni nini?
 
Mbona hakuna msaada kwenye msikiti, nyumba ya Imam nk? huyu ni mdini kama Chadema wenzie tu Mwenyezimungu amhukumu anachostahiki

wewe ni kilaza mzoefu,kama hawajaomba hiyo misaada yeye atajuaje kama wanahitaji wakati haendi kusali huko?Hao waliopewa waliomba.Mtu anakupa msaada baada ya kuomba.Acha siasa za kijinga na kidini
 
Mwenyezi Mungu awasaidie wapone. Kuna umuhimu wa kuwa na sera ya kiuongozi ambayo Mbunge atakuwa anajua majukumu yake kiusahihi na sio kuwa MFADHILI...
 
Huyu jamaa ni mbabaishaji. Hizi hela anazotaja ni fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo, sio zake wala hajafight kuzipata. Hata ungeweka mtoto mdogo ukampa hizo hela angegawa.
Tunamuombea Selasini apone then atuambie jimbo letu linapata sh ngapi za mfuko wa maendeleo ya jinbo, na yeye, kwa miaka hii miwili amezitumiaje...
Tunataka atuambie amefanya nini kuwasadia maelfu ya vijana wanaomaliza form four, na six...
Tunataka atuambie amefanya nini kusimamia ujenzi wa barabara za halmashauri ambazo sehemu nyingi hazipitiki...
Tunataka atuambie tatizo la maji kwa maeneo mengi ya Tarakea, na ugawaji maji unaopendelea matajri amelighulikia vipi...
Tunataka atuambie amefanya nini kukabiliana na tatizo kubwa la ukosefu wa walimu katika shule za sekondari Rombo...
Tunataka atuambie ni kwa nini performance za shule za Rombo kwenye mitihani ya form four inazidi kuwa mbovu, ana idea gani yeye kama mbunge na amefanya nini...
Tunataka atuambie emeshughulikia vipi suala la ugawaji wa mashamba maeneo ya forest kunakofanywa kibaguzi na kiupendeleo...
Tunataka atuambie ameshughulikia vipi suala la ukosefu wa madawa na magari ya wagonjwa katika vituo vya afya, useri na Tarakea...
Tunataka atuambie anafanya nini kusaidia tatizo la mamia ya watu walioomba umeme kwa miezi mingi sasa, wamelipa lakini hawajafungiwa, na waliofungiwa walifanikiwa baada ya kutoa rushwa nyingi sana...
Tunataka atuambie yeye kama mbunge amefanya nini kuwasaidia maelfu ya vijana wa Rombo kufaidika na mlima Kilimanjaro tofauti na sasa ambapo wanaofaidika kwa kiasi kikubwa ni wa wilaya nyingine...

Selasini kiukweli amekuwa mzigo kwa Wanarombo, na kama nilivyokwisha sema humu JF tangu mwaka jana, asipojirekebisha, asipokuwa karibu na wapiga kura wake akawasikiliza na kuwasaidia kupambana na adui umaskini, then ajue 2015 hana chake. Kama haamini akawaulize kina Mramba na Salakana...

Mbona na wewe una hoja mfu?yaani wewe ukipewa msaada unaanza ku-demand tena kuwa hizo fedha sio zake.Kwa hiyo ili mbunge asaidie lazima ziwe zake?Halafu hilo la tatizo la walimu na ufaulu wa wanafunzi wa form four na six mbona hiyo iko nje ya uwezo wa mbunge?Waambie wajitahidi kusoma,kwani mbunge hata akiwa malaika hatawafanyia mtihani.Usiweke malalamiko yasiyo na msingi,think critically.
 
Back
Top Bottom