Ujue Ukweli na Uwongo kuhusu Ndoa ...........

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Ndugus
FYI

Ujue ukweli na uongo kuhusu ndoa zetu;

Uongo
Ndoa ni mkataba (contract) na kwa kuwa ni mkataba basi unaweza kuvunjwa.
Ukweli:
Ndoa ni agano (covenant) lililowekwa na Mungu. Ilikuwa ni mpango wa Mungu hata kabla ya binadamu kuweka mikataba ya kisheria kuhusu ndoa. Mungu ana define ndoa ni agano na agano halijajikita katka msingi ya kupokea zaidi ya unavyotoka (quid pro quo)

Uwongo:
Unaoa au kuolewa ni yeye tu hakuna uhusiano na familia yake
Ukweli:
unapooa au kuolewa si mwenzi tu bali ni pamoja na package ya familia yale.

Uwongo:
Naweza kumbadilisha mwenzi wangu:
Ukweli:
Huwezi kumbadilisha, unachoweza ni kumuathiri na tabia zako.
Kama unaamini utaweza kumbadilisha mwenzi wako unanidanganya na zaidi utakuja kukatishwa tamaa kwa hali ya juu sana.

Uwongo:
Tupo tofauti sana ndoa haiwezi kufika popote
Ukweli:
Tofauti zinazokuwepo kati ya mke na mume haziwezi kuiua ndoa bali jinsi tofauti zinavyoshughulikiwa ndicho kitu kinachoweza kuleta maafa.
Hakuna familia mbili ambazo hufanana kila kitu na hakuna watu wawili wanaweza kwenda sawa kwa kila kitu hivyo lazima kutakuwa na tofauti kati ya mke na mume. Kumbuka ukikutanisha vitu viwili katika mwendo (moving) lazima msuguano utatokea na mke na mume ni watu na watu ni moving object hivyo tofauti na kusuguana lazima.

Uwongo:
Nimepoteza zile hisia za kumpenda tena na zimepota kabisa, aitawezekana kumpenda tena.
Ukweli:
Hisia za kumpenda huweza kurejeshwa. Ukielekeza katika positive kuliko negative unaweza kurejesha mapenzi kama mwanzo. Kuwa na kiwango kikubwa cha negative kwa mwenzi wako hupelekea kujiweka mbali (emotional distance) na kupoteza upendo ingawa siri ni kuendelea kuangalia upande wa positive.

Uwongo:
Siwezi kubadilika hivyo nichukue kama nilivyo au niache.
Ukweli:
Unaweza kubadilika ingawa unahitaji hamu ya kutaka kubadilika, utiifu katika kutaka kubadilika na uwezo wa kutaka kubadilika. Kwako binafsi ni vigumu kubadilika ila kwa uwezo wa Mungu Inawezekana kubadilika

Uwongo:
Mwenzangu amenisaliti kwa kutoka nje ya ndoa hivyo jibu ni talaka
Ukweli:
kutoka nje ya ndoa huumiza na huangamiza lakini si zaidi ya kushindwa kufanya marekebisho na upatanisho. Ni jambo la msingi kujua sababu ya affair ilikuwa ni nini, then kwa msaada wa Mungu kusameheana, kutubu na kujitolea kuacha na kubadilika. Kumbuka katika Biblia hakuna sehemu inayoruhusu talaka bali kusameheana na upatanisho. Hii haina maana kwamba unaruhusiwa kuwa na affair kwa sababu kuna kusamehewa na kupatanishwa.

Uwongo:
Ndoa imefika mahali ambapo hatuwezi kuirejesha tena:
Ukweli:
Bado hamjachelewa, kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Je, hata ndoa ambayo imekufa inaweza kufufuliwa? Ni kweli Inawezekana kwani Mungu wetu ni Mungu wa muujiza. Kama Mungu hawezi kufanya kile ametuahidi atakuwa Mungu gani? Mungu anaweza kubadilisha mioyo na kutoa njia na mwelekeo mpya kabisa katika ndoa na mahusiano.

Source: The Hill Of Wealth
 
The Boss dini ni utumwa mbaya zaidi wa fikra. Upenzi wa duni ni mzito kuliko upenzi wa yule uliyenaye
 
Last edited by a moderator:
uwongo mwingine: kupunguza stress za ndoa ni kujipatia nyumba ndogo au buzi.
 
The Boss na Kaizer hii post ni ya zamani sana but ndiyo iliyonifanya nikauwin moyo wa Soulmate jamani LOL!!
Nitamfikishia salamu zenu.
 
Last edited by a moderator:
thread nzuri sana nimeipenda sana:A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2::A S-heart-2:
 
Asante kwa mada, I missed busara zako!
Ila nina swali: kwanini mimi siwezi kumbadili ila unasema mimi naweza kubadilika?
Uwongo:
Naweza kumbadilisha mwenzi wangu:
Ukweli:
Huwezi kumbadilisha, unachoweza ni kumuathiri na tabia zako.
Kama unaamini utaweza kumbadilisha mwenzi wako unanidanganya na zaidi utakuja kukatishwa tamaa kwa hali ya juu sana.

Uwongo:
Siwezi kubadilika hivyo nichukue kama nilivyo au niache.
Ukweli:
Unaweza kubadilika ingawa unahitaji hamu ya kutaka kubadilika, utiifu katika kutaka kubadilika na uwezo wa kutaka kubadilika. Kwako binafsi ni vigumu kubadilika ila kwa uwezo wa Mungu Inawezekana kubadilika
 
imekaa vyema natamani mods wangekuwa wanaturejeshea hizi thread za aina hii katika page ya kwanza coz siku hizi nikawaida kukuta thread zimejipanga ya kwanza mpaka ya 20 lakini ukisoma kilichomo ni upuuzi tu.
 
Ndugus
FYI

Ujue ukweli na uongo kuhusu ndoa zetu;

Uongo
Ndoa ni mkataba (contract) na kwa kuwa ni mkataba basi unaweza kuvunjwa.
Ukweli:
Ndoa ni agano (covenant) lililowekwa na Mungu. Ilikuwa ni mpango wa Mungu hata kabla ya binadamu kuweka mikataba ya kisheria kuhusu ndoa. Mungu ana define ndoa ni agano na agano halijajikita katka msingi ya kupokea zaidi ya unavyotoka (quid pro quo)

Uwongo:
Unaoa au kuolewa ni yeye tu hakuna uhusiano na familia yake
Ukweli:
unapooa au kuolewa si mwenzi tu bali ni pamoja na package ya familia yale.

Uwongo:
Naweza kumbadilisha mwenzi wangu:
Ukweli:
Huwezi kumbadilisha, unachoweza ni kumuathiri na tabia zako.
Kama unaamini utaweza kumbadilisha mwenzi wako unanidanganya na zaidi utakuja kukatishwa tamaa kwa hali ya juu sana.

Uwongo:
Tupo tofauti sana ndoa haiwezi kufika popote
Ukweli:
Tofauti zinazokuwepo kati ya mke na mume haziwezi kuiua ndoa bali jinsi tofauti zinavyoshughulikiwa ndicho kitu kinachoweza kuleta maafa.
Hakuna familia mbili ambazo hufanana kila kitu na hakuna watu wawili wanaweza kwenda sawa kwa kila kitu hivyo lazima kutakuwa na tofauti kati ya mke na mume. Kumbuka ukikutanisha vitu viwili katika mwendo (moving) lazima msuguano utatokea na mke na mume ni watu na watu ni moving object hivyo tofauti na kusuguana lazima.

Uwongo:
Nimepoteza zile hisia za kumpenda tena na zimepota kabisa, aitawezekana kumpenda tena.
Ukweli:
Hisia za kumpenda huweza kurejeshwa. Ukielekeza katika positive kuliko negative unaweza kurejesha mapenzi kama mwanzo. Kuwa na kiwango kikubwa cha negative kwa mwenzi wako hupelekea kujiweka mbali (emotional distance) na kupoteza upendo ingawa siri ni kuendelea kuangalia upande wa positive.

Uwongo:
Siwezi kubadilika hivyo nichukue kama nilivyo au niache.
Ukweli:
Unaweza kubadilika ingawa unahitaji hamu ya kutaka kubadilika, utiifu katika kutaka kubadilika na uwezo wa kutaka kubadilika. Kwako binafsi ni vigumu kubadilika ila kwa uwezo wa Mungu Inawezekana kubadilika

Uwongo:
Mwenzangu amenisaliti kwa kutoka nje ya ndoa hivyo jibu ni talaka
Ukweli:
kutoka nje ya ndoa huumiza na huangamiza lakini si zaidi ya kushindwa kufanya marekebisho na upatanisho. Ni jambo la msingi kujua sababu ya affair ilikuwa ni nini, then kwa msaada wa Mungu kusameheana, kutubu na kujitolea kuacha na kubadilika. Kumbuka katika Biblia hakuna sehemu inayoruhusu talaka bali kusameheana na upatanisho. Hii haina maana kwamba unaruhusiwa kuwa na affair kwa sababu kuna kusamehewa na kupatanishwa.

Uwongo:
Ndoa imefika mahali ambapo hatuwezi kuirejesha tena:
Ukweli:
Bado hamjachelewa, kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Je, hata ndoa ambayo imekufa inaweza kufufuliwa? Ni kweli Inawezekana kwani Mungu wetu ni Mungu wa muujiza. Kama Mungu hawezi kufanya kile ametuahidi atakuwa Mungu gani? Mungu anaweza kubadilisha mioyo na kutoa njia na mwelekeo mpya kabisa katika ndoa na mahusiano.

Source: The Hill Of Wealth

mwanajamiiOne... Nimekupenda bure ndugu yangu kwa thread yako hebu tuletee nyingine tena yenye adabu kama hii ili na sisi wagen tupate kunufaika
 
Kwa kweli sijawahi kutana na thread ya kijinga toka kwa MJ1. Tafuta in archives uelimike.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom