Ujue ukweli kati ya mwingira na afro plus

Wanaotaka kujua ukweli wa umiliki wa eneo na matukio katika eneo la Efatha, Mwenge, Dar es Salaam wasome taarifa iliyoambatanishwa hapa. Mwenye data za umiliki wa eneo tofauti na hizi aziweke hapa ili ukweli ujulikane kwa umma.
 

Attachments

  • EFATHA FOUNDATION LTD PRESS RELEASE.pdf
    59.3 KB · Views: 181
Wanaotaka kujua ukweli wa umiliki wa eneo na matukio yaliyotokea eneo la Efatha, Mwenge, Dar es Salaam wasome taarifa iliyoambatanishwa hapa. Kama kuna mtu mwenye data za umiliki wa eneo hilo tofauti na hizi aziweke hapa ili ukweli ujulikane kwa umma.
 
Thanks mkuu....huku nje kila mtu anaongea lake....lakini nafikiri Efatha ni wakati wa kuonesha njia ya kutatua migogoro mikubwa hii kwa njia mbadala..kaeni na vyombo mbalimbali vya usalama muangalie namna gani mgogoro huu unatatuliwa kwa ushuhuda. Bwana Yesu awasaidie
 
Wanaotaka kujua ukweli wa umiliki wa eneo na matukio yaliyotokea eneo la Efatha, Mwenge, Dar es Salaam wasome taarifa iliyoambatanishwa hapa. Kama kuna mtu mwenye data za umiliki wa eneo hilo tofauti na hizi aziweke hapa ili ukweli ujulikane kwa umma.
Mshauli Mwingira apeleke mahakamani atapata haki,ila aache Papara na unabii wa uongo ni aibu kwa Ukristo.Hiyo tabia ya mwingira inaitwa Fanaticism
 
Wanaotaka kujua ukweli wa umiliki wa eneo na matukio yaliyotokea eneo la Efatha, Mwenge, Dar es Salaam wasome taarifa iliyoambatanishwa hapa. Kama kuna mtu mwenye data za umiliki wa eneo hilo tofauti na hizi aziweke hapa ili ukweli ujulikane kwa umma.

fungua uiweke hapa tuione. natumia simu.
 
EFATHAFOUNDATION LTD P.O BOX32174, MWENGE, DAR ES SALAAM TELEPHONE:+255732993196, FAX:+255732993196 WEBSITE:www.efathafoundation.org EMAIL:efathafoundationltd@yahoo.com / info@efathafoundation.org OUR REF:EFL/ADMN/4/2012 DATE: 11thApril, 2012
TAARIFA KWAUMMA

1. UMILIKIWA KIWANJA NA. 90, ENEO LA MWENGE (NURU CENTRE)

1.1Utangulizi
Tarehe 9 mwezi April 2012, Jumatatu ya Pasaka,baadhiya vyombo vya habari vilitangaza habari ya umiliki na matukio yaliyotokeakatika eneo hilo. Habari zilizotangazwa ni za upande mmoja na hazina usahihi.Huduma ya Efatha inapenda kuelezea umma taarifa sahihi juu ya upatikanaji wakiwanja na 90, umiliki na matukio yaliyotokea katika eneo hilo.

1.2Upatikanaji na umiliki wa eneo
Serikali kupitia Tume ya Kurekebisha naKubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC) ilitangaza zabuni ya uuzwaji wa eneo laMang'ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika, Kiwanja namba90, Mwenge katika magazeti ya Uhuru na Daily News ya tarehe 4 mwezi Mei 2005. Tarehe 18 Mei 2005, huduma ya Efatha kupitiakitengo chake cha uchumi, Efatha Foundation Ltd, ilipeleka maombi ya zabuni yakununua eneo hilo PSRC. Efatha Foundation Ltd ilipokea barua kutoka PSRCyenye kumbukumbu Na. PSRC/1/13/93 ya tarehe 30 Mei 2005 ikiarifu kwamba zabuniyetu ya kununua eneo hilo imeshinda kwa kiasi cha shilingi za kitanzaniamilioni mia nne. Masharti ya Malipo ya zabuni yalikuwa asilimia kumiilipwe wakati wa kupeleka maombi na asilimia tisini ilipwe ndani ya miezimitatu baada ya kushinda zabuni. Efatha Foundation Ltd ililipa shilingi milioniarobaini yaani asilimia kumi ya bei siku ya kupeleka maombi ya zabuni kwa hundiNa. 000261 ya benki ya Azania na kupewa risiti ya PSRC Na. 6956 ya tarehe 31Mei 2005. Na shilingi milioni mia tatu sitini ililipwa kupitia hundi Na. 000319ya benki ya Azania ambayo ni asilimia tisini tarehe 10 mwezi Juni 2005 nakupewa risiti ya PSRC Namba 6984 na hivyo malipo yote yakawa yamekamilishwa. Baada ya kukamilisha malipo Efatha Foundation Ltdilikabidhiwa hati miliki Namba 41641 ambayo ilipelekwa wizara ya Ardhi iliibadilishwe jina kutoka mmiliki wa mwanzo na kuandikishwa jina la EfathaFoundation Ltd. Kwa hiyo Serikali ikahamisha umiliki kutoka Mang'ula Mechanicaland Machine Tools Company Ltd iliyofilisika kwenda Efatha Foundation ltd tarehe15 Novemba 2005 saa sita kamili mchana kwa uhamisho Namba 98648. Kabla ya Huduma ya Efatha kununua eneo hilokulikuwa na wavamizi ambao ni makampunina watu binafsi kumi na moja ambao walikuwa wamewekwa katika eneo hilo na Mang'ula Mechanical and Machine ToolsCompany Ltd iliyofilisika bila kibali cha mfilisi yaani PSRC. Kwa kuwa hawakuwawapangaji halali walikuwa wavamizi (trespassers).Wavamizi hao wakapewa notisi ya kuondoka na PSRC lakini hawakuondoka. Baadae shughuli za mfilisi,PSRC, zikachukuliwa kisheria na Consolidated Holding Corporation (CHC). CHC nao wakawapawale wavamizi notisi kuwa waondoke kwasababu eneo hilo limeuzwa lakini hawakuondoka. Efatha Foundation Ltdilipomiliki eneo hili kihalali na kisheria wakawapa wavamizi notisi ya kuondokamwaka 2005, wavamizi nane wakatii amriwakaondoka na wavamizi watatu walikaidi kuondoka ambao ni pamoja na Afro Plus Industries Ltd. Baada ya hapo wavamizi watatu waliokataa kuhamawakafungua kesi mahakamani dhidi ya Efatha Foundation Ltd wakipinga kuhamishwa.Ni vyema ieleweke kuwa Efatha Foundation Ltdiliponunua eneo hili thamani yake ilijumuishamajengo yaliyokuwa yamejengwa humo na Mang'ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika. Hiini pamoja na jengo alilokuwa anatumia Afro Plus Industries Ltd ambalolinalalamikiwa kubomolewa na kwamba tumeharibu mali. Jengo lililobomolewa ni mali ya EfathaFoundation Ltd na siyo mali ya Afro Plus Industries Ltd kama ilivyodaiwa.

2. UVAMIZIWA POLISI NDANI YA KANISA LA EFATHA MWENGE
Tarehe 9 Aprili 2012, jumatatu ya pasaka, majira yasaa kumi na mbili asubuhi waumini waEfatha walikuwa katika ibada ya morning glory katika kanisa la Efatha Mwenge wakiongozwa katika ibada hiyo na MchungajiDavid Mwakisole ndani ya kanisa. Kanisa limezungushiwaukuta pande zote nne na lina mageti ya kuingilia kanisani ambayo yanafungwa.Polisi walipanda ukuta wakachungulia wakasikika wakisema hawa huku ndani. Baadae polisi wakarukia ndani kupitiaukutani. Wakati ibada inaendelea ghafla wauminiwalivamiwa kutoka nje na watu ambao baadae walitambuliwa kuwa ni polisi. Walipoingia kwa nguvu wakatupa mabomu yamachozi ndani ya kanisa huku wakifyatua risasiza moto wakati ibada ikiendelea. Kwa kitendo hicho ibada ilivurugika nakusimama na waumini wakaanza kukimbiaovyo ndani ya kanisa. Risasi na mabomu ya machozi yalitupwa kuelekea madhabahuni na kuelekea kwawaumini waliokuwa katika ibada. Wauminiwengine waliokuwa wakija kwenye ibada walizuiliwa nje na kukamatwa. Kilichofuata ni vurugu huku waumini wakikimbiana polisi wakiwapiga kwa virungu, vitakovya bunduki na mateke. Baadhi ya waumini walijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili na ukumbi wa kanisaulitapakaa damu. Pia polisi walivunja madirisha,viti, milango na spika kama ilivyoonyeshwa katika baadhi ya vyombo vya habari hasa ITV. Kabla hawajavamia, mmoja waaskari aliwatahadharisha wenzake kuwa wasipigemabomu na risasi kwa kuwa hapo ni kanisani lakini wenzake walipinga wakisema kuwa huyu mtu ana kiburi na watu hawani wakorofi. Wakati risasi na mabomuyakipigwa baadhi ya askari walikuwa wakiokota maganda ya risasi na mabaki ya mabomu ya machozi ili kuondoa ushahidi.Hata hivyo baadhi ya risasi za moto, magandaya risasi za moto na mabaki ya mabomu yalibaki kanisani na yamehifadhiwa mahali maalum kwa hatua zaidi. Kanisani kulikuwa na idadi ya waumini kati yasitini na sabini waliokuwa wanaabudu. Polisiwaliwakamata jumla ya waumini 53 pamoja na wachungaji waliokuwa wakiongoza ibada wakiwapiga na kuwasweka katika magari yapolisi kuwapeleka kituoni pamoja na kuvutagari zilizokuwa zimeegeshwa nje ya kanisa kwa breakdown. Tumepata habari kuwa walikuja na baadhi ya waandishi wa habariwalioandaliwa kabla ili kurekodi tukio hilona ushahidi tunao. Kwetu sisi inaonyesha kuwa tukio hilo liliandaliwa kwamakusudi ili likatekelezwe katika kanisala Efatha. Tukio hili linatupa hisia kuwa kuna chuki kubwa kwa Huduma ya Efatha. Kitendo cha polisi kuvamia na kuvuruga ibada nikinyume na sheria na katiba ya jamhuri yaMuungano wa Tanzania iliyoweka uhuru wa kuabudu na sheria za nchi zinazoeleza kwamba ibada ziheshimiwe na zisiingiliwe.Tunajiuliza kulikuwa na tatizo gani polisi wasisubiri nje ibada iishe na wawachukue watuwanaotaka kuwachukua. Ndani ya kanisahakukuwa na vita, wala mtu mwenye silaha, wala mtu anayeuawa ambaye polisi walilazimika kwenda kumwokoa. Sisi tunalionahili kuwa ni kumdharau Mungu, kuvurugaibada na kuwadhalilisha waumini wa Efatha waliokuwa wakitumia uhuru wao wa kuabudu. Leo wamefanya hivyo kwa dharaundani ya kanisa la Efatha, kesho tutegemeewatakwenda kufanya nini kwa dhehebu jingine, Msikiti, Dini nyingine au watu waliokusanyika kihalali na kwa sababuhalali?

3.MAJUMUISHO
Vielelezo vyote kuhusu umiliki wetu halali wa eneohili vilishawasilishwa polisi mkoani nawilayani. Kutokana na maelezo haya Efatha Foundation Ltd inapendakuuthibitishia umma kuwa EFATHAFOUNDATION LTD ndiyo mmiliki halali wa KIWANJA NA. 90, ENEO LA MWENGE (NURUCENTRE) na si vinginevyo.

KATIBU
EFATHAFOUNDATION LTD
 
Mbona taarifa haielezi nani aliyevunja jengo la afro plus?kwa nini efatha imekua na migogoro ya ardhi sehemu nyingi?
 
Mbona taarifa haielezi nani aliyevunja jengo la afro plus?kwa nini efatha imekua na migogoro ya ardhi sehemu nyingi?

Tatizo lako Unalaza ubongo wako:

Efatha Foundation Ltd ilipomiliki eneo hili kihalali na kisheria wakawapa wavamizi notisi ya kuondoka mwaka 2005, wavamizi nane wakatii amri wakaondoka na wavamizi watatu walikaidi kuondoka ambao ni pamoja na Afro Plus Industries Ltd. Baada ya hapo wavamizi watatu waliokataa kuhamaw akafungua kesi mahakamani dhidi ya Efatha Foundation Ltd wakipinga kuhamishwa. Ni vyema ieleweke kuwa Efatha Foundation Ltd iliponunua eneo hili thamani yake ilijumuisha majengo yaliyokuwa yamejengwa humo na Mang'ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika. Hii ni pamoja na jengo alilokuwa anatumia Afro Plus Industries Ltd ambalo linalalamikiwa kubomolewa na kwamba tumeharibu mali. Jengo lililobomolewa ni mali ya Efatha Foundation Ltd na siyo mali ya Afro Plus Industries Ltd kama ilivyodaiwa.
 
Back
Top Bottom