Ujio wa Nicodemus

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
.ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;} Jioni moja katika nyumba ya Flavius alikuja kumuona Yesu mtu mmoja Nicodemus,tajiri,mtu wa makamu,mmoja wa Sanhendrin ya Wayahudi. Alikuwa amesikia mengi kuhusu mafundisho ya huyu Mgalilaya,kwa hiyo alikwenda jioni moja kumsikiliza alivyofundisha katika viwanja vya hekalu. Angekwenda mara nyingi kumsikia Yesu anafundisha lakini alihofu kuonwa na watu kwamba anahudhuria mafundisho yake,kwa sababu tayari viongozi wa Wayahudi walikuwa wanapingana na Yesu kiasi kwamba hakuna mtu yoyote katika Sanhendrin ambaye alikuwa yuko tayari kuhusishwa kwa njia ya wazi. Kwa ajili hiyo,Nicodemus alipanga na Andrew kumuona Yesu faragha na baada ya giza kuingia katika jioni hii. Peter,James na John walikuwepo katika bustani ya Flavius wakat imahojiano yalipoanza,lakini baadaye wote walikwenda katika nyumba ambapo mazungumzo yaliendelea.

Katika kumpokea Nicodemus Yesu hakuonyesha heshima yoyote ya zaidi; katika kuongea naye hakukuwepo kulegeza msimamo au kushawishi kupita kiasi. Mwalimu hakufanya jaribio lolote kumkwepa huyu mgeni aliyekuja kwa siri,wala hakuongea kwa kejeli. Katika mahusiano yote yake na huyu mgeni mheshimiwa,Yesu alikuwa shwari na makini,na mwenye staha. Nicodemus hakuwa mjumbe ameletwa na Sanhendrin;alikuja kumuona Yesu kwa ajili yeye binafsi alikuwa kwa dhati ana hamu ya kufahamu mafundisho ya Yesu.

Alipoletwa na Flavius,Nicodemus akasema,''Rabbi,tunajua kwamba umeletwa na Mungu,kwa vile mtu wa kawaida tu hawezi kufundisha namna hii isipokuwa tu kama Mungu yuko naye. Na mimi ningependa kujua zaidi haya mafundisha yako kuhusu ufalme unaokuja.''

Yesu akamjibu Nicodemus,''Hakika,hakika,nakuambia,Nicodemus,mtu asipozaliwa kutoka juu hawezi kuuona ufalme wa Mungu.'' Halafu Nicodemus akajibu,''Lakini mtu anawezaje kuzaliwa kama ameshakuwa mzee? Hawezi kuingia tumboni kwa mama yake kuzaliwa mara ya pili.'' Yesu akasema,''Hata hivyo,nakuambia,mtu asipozaliwa katika roho,hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. Kile kinachozaliwa na mwili ni mwili na kile kinachozaliwa na roho ni roho. Lakini usishangae kwamba nimesema lazima uzaliwe kutoka juu. Upepo unapovuma,unasikia majani yanavuma,lakini huuoni upepo-unakotoka na unakokwenda-na hivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa kila anayezaliwa kwa roho. Na macho ya mwili unaweza kuona matokeo ya roho,lakini roho yenyewe huwezi kuibaini.'' Nicodemus akajibu,''Lakini sielewi-hiyo inawezekanaje?'' Akasema Yesu,''Inawezekana kwamba wewe ambaye ni mwalimu katika Israel lakini bado unashindwa kuyaelewa haya yote? Inawajuzu,kwa hiyo,wale wanaozifahamu kweli za roho kuyafunua haya mambo kwa wale ambao wanabaini matokeo tu ya dunia tunayoishi. Lakini utatuamini tukikuambia kuhusu kweli za mbinguni? Unao ujasiri,Nicodemus,kuweka imani yako kwa yule ambaye ameshuka kutoka mbinguni,yaani Mwana wa Mtu? Nocodemus akajibu,''Lakini naweza vipi kuanza kuikamata hii roho ambayo itanitengeneza upya kunitayarisha kuingia katika ufalme?'' Yesu akajibu,''Tayari roho ya Baba wa mbinguni inaishi ndani mwako. Ukikubali kuongozwa na hii roho kutoka juu,baada ya muda si mrefu utaanza kuona kwa macho ya roho,na halafu kwa kuamua kwa moyo wako wote kukubali kuongozwa na roho utazaliwa katika roho kwa vile madhumuni yako yote ya kuishi yatakuwa ni kufanya utashi wa Baba yako aliye mbinguni. Kwa hiyo utakapojikuta umezaliwa katika roho na una furaha katika ufalme wa Mungu,utaanza kuzaa katika maisha yako ya kila siku matunda mengi ya roho.''

Nicodemus alifika kwa nia njema. Alipendezwa lakini aliondoka amechanganyikiwa. Nicodemus alikuwa ni mtu ambaye amejiendeleza nafsi,mwenye nidhamu na pia mtu mwenye maadili mazuri. Alikuwa ni mstaarabu,pia mtu wa kufikiri sana,mtu anayependa kujitolea kuwasaidia wengine;lakini hakufahamu jinsi ya kutiisha utashi kwa utashi mtakatifu wa Baba kama ambavyo mtoto mdogo yuko radhi kukubali mwongozo na maelezo ya baba wa dunia mwenye hekima na upendo, na kwa kufanya hivyo kuwa kwa hakika mtoto wa Mungu,kuwa mrithi mwnandamizi wa ufalme wa milele.

Lakini Nicodemus alikusanya imani ya kutosha kuushikilia ufalme. Alilalamika kidogo wenzake katika Sanhendrin walipomhukumu Yesu bila kumsikiliza;na pamoja na Joseph wa Arimathea,baadaye kwa ushupavu alitangaza imani na kuudai mwili wa Yesu,hata wakati mitume karibu wote walikimbia kutoka kwenye matukio ya mwisho ya mateso na kifo cha Mwalimu wao.
 
Back
Top Bottom