Ujio wa filam ya maisha ya kikwete iitwayo "mr.president" ni disemba 9. Kaa mkao wa kula

ibontoko

Member
Oct 31, 2011
62
14
MWIGIZAJI na mchekeshaji maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere' ameandaa filamu inayoitwa Mr. President ambayo ndani yake inachambua maisha ya kifamilia na kikazi ya Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa miaka 50 ya uhuru imemkuta akiwa madarakani.

"Hii ni zawadi kwa Rais Kikwete pamoja na Watanzania kwamba, hata rais ni binadamu, anaishi kama wengine, tofauti ni madaraka tu. Ndani ya hii filamu kuna vituko vya hapa na pale vilivyotumika kuonesha maisha halisi ya Mheshimiwa JK, yaani burudani mwanzo mwisho," alisema msanii huyo.

CHANZO <<HAPA>>
 
wale wachekeshaji bana.hakuna kitu kama hicho.mi nmeshaona kipande cha hiyo movie. Stive kajaribu kuongea kama kikwete na kuchekacheka.haitusaidii chochote kukabiliana na matatizo yanayo tukabili tofauti na kuendelea kudumaza akili na mawazo ya kitanzania.bora wangeonyesha maovu yake na mapungufu.lakini yeye kang'ang'ana na walinzi wake na mkewe tu.lakini kwa wapenda comedy ipo poa.mia
 
Kweli JK gangwe! Katengenezewa hadi filamu inaonyesha maisha yake na njia anazotumia kutumaliza! Kweli huyu jamaa gangwe
 
Huyo Steven Ngerere ndiye miongoni mwa wale watu waliokua kwenye misafara ya JK nchi nzima wakati wa kampeni za Urais mwaka 2010.
 
Back
Top Bottom