Ujio wa CHADEMA Iringa: Tafsiri Yangu

Yes, naona Maggid sasa amekuwa mtu mzima baada ya uchaguzi kuisha. Anaanza kuelezea hisia za jamii.
Nashukuru sana Maggid tupupasha kuhusu mwitikio wa wananchi wa Iringa. It is good ....
Hakuna kulala mpaka kieleweke na kitaeleweka tu!
 
Majid ndo analiona leo hilo? Wakati anaipigia kampeni ccm hakuliona hilo?
Nadhani blog yake imekosa mashiko kwa hiyo anatafuta wasomaji kinguvu.
 
Wakuu,

Sikuamini kama hii post ni ya "maggid mjengwa"

Ni vizuri kusimamia ukweli maggid!! Hongera bro... join our world.
 
Siku nyingine Maggid anajivua gamba na kuamua kuongea ukweli!

Amekosa wasomaji kwenye blogu yake ameamua kuwafuata huku.
Majid amegundua alifanya kosa kushabikia ccm na kuikandamiza cdm wakati wa kampeni, na sasa anataka kujirudi. Karibu chadema Majidi.
 
Hapa hakuna habari mpya kwangu, kama Maggid mpaka aone mkutano mkubwa kwao Iringa ndio ajuwe ccm haitakiwi na Watanzania, basi natilia shaka na upeo wake. Watanzania hawaitaji tena makala za waandishi wajanja wajanja kudai haki zao, watu wameshajitambuwa.

Big up ! Namjua Majid kwa hili amenena, mwenye masikio na asikie! Aaaaah kijana wa Upsallah!!!!Labda utabiri unatimia kwamba,JK aliunda TANU (1954); JK anaua CCM(2011) miaka 50 baadaye ????

Voxy populy voxy dei!!!!
 
CCM siyo inayumba tu bali imeshayumba ikadondoka sasa inakata roho

Kimsingi, dira imepotea lazima itayumba LAKINI angalizo kuyumba kwake kusiwe kubweteka kwa cdm na wengine !!!! :mod:
Wingi wa watu ktk maandamano si kigezo cha ukomavu kwa siasa za WA-TZ!!! unamkumbuka Lyatonga??? Katika Kujivua-gamba (re-born-again) ndani ya ccm wapo watakaoiyumbisha ccm pia watakao imarisha ni muhimu sana cdm wakae chonjo ktk hili!!!!

MTIKIKISIKO KTK NYUMBA HUMARISHA KUTA!!!!!
Strike the iron when its hot!!!!!
 
naona gamba limevuka

King na wengine,
Ahsanteni, nirudie tu, maana nilishasema hili, kwamba mimi ni Maggid yule yule na nitabaki kuwa hivyo. Sijawahi kuvaa, kuvalisha au kuvalishwa gamba. Hivyo basi, nimekuwa mwandishi huru na nitabaki kuwa hivyo. Nina staili zangu za kuandika, nyingine hunisaidia kuchokoza mijadala. Si kila mmoja atanielewa.

Haya mengine nimeshayazoea. Leo kuna wanaokubali ninachoandika, kesho kuna watakaosema; " Amenunuliwa na mafisadi!". Hivi hao mafisadi wa nchi hii wana hela kiasi gani wamnunue kila anayekamata kalamu na kuandika mawazo yake?
 
CCM kutuzuia tusiende ikulu kwa staili ya kizamani ya kuiba kura kwa kutumia NEC imepitwa na wakati. Hawataweza. Nguvu ya umma ya staili ya ubungo itakuwa nchi nzima 2015. Hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Mwandishi wa Habari Samson Chacha , ametishiwa Maisha na wafuasi wa Chama Cha Demkorasia na Maendeleo Chadema Wilayani Tarime , kwa kile walichodai kuwa asingepaswa kutangaza kuhusu Kushambuliwa kwa Mawe kwa Mbunge wao Godbles Lema kutoka Arusha katika mji mdogo wa Sirari wakati akiwashawishi Vijana wa Mji huo kuungana na Chadema kwenda kufanya Vurugu Nyamongo na Tarime,

Tukio hilo la kutishiwa Maisha na Wafuasi hao wa Chadema waliokuwa wakiongozwa na Chacha Heche Suguta ,akiongozana na kundi la vijana zaidi 10 wakiwa na Sare za Chadema akiwemo Diwani wa Viti Maalumu kata ya Sirari kupitia chama hicho cha Chadema Veronika Sando, Amos Mondawela,Keraryo Mwita, wakiwa na Mutangazaji wa Chanel Ten Mkoani Mara Mabere Makubi ambaye amekuwa akiongozana na kundi hilo linalopita katika miji ya Watu na kuwashawishi Uchochezi wa kwenda Nyamongo kuvamia Mgodi Wakitumia Kivuli cha Watu 5 kuuawa na Polisi wakati wa kuvamia Mgodi wa North Mara Barrick hapo Mei 16 mwaka huu,

Akisimulia tukio hilo kwa vyombo vya habari , Mwandishi huyo bw, Samson ,alisema kuwa "Nakumbuka mnamo Mei 22 mawaka huu saa 12 Jioni nikiwa maeneo ya Nyumbani huko Sirari, tukiwa tunakunywa Soda na wengine wakila Chakula katika Hotel ya Robart Ndugu , Walifika Wafuasi wa Chadema wakiwa wamevalia Sare zao wakiongozwa na Chacha Heche na wenzake , walitukuta nje ya Hotel katika Veranda na kutuzunguka Meza yetu ambapo Chacha Heche alianza kuniuliza kuwa kwa nini nimemwandika Mbunge wao Godbles Lema kuwa alirushiwa Mawe hapo Sirari ",

Mwandishi huyo bw, Samson Alisema kuwa "Mwandishi wa habari wa Chanel Ten Mabere Makubi naye alianza kuuliza kuwa "Nasikia kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime alishiriki kumrushia mawe Mbunge Lema ?, nilimjibu kuwa mambo ya Mwenyekiti Kamuulize Mwenyewe akupe uhakika , na jaribu kufata maadili ya uandishi wa habari usitumiwe na kikundi cha watu kushawishi na kuchochea vurugu , Sheria zipo kwa nini uungane na wafuasi wa Chadema kupitapita katika miji ya watu kuwashawishi kwenda kuvamia Magodi ?, hapo ndipo kundi hilo la Wafuasi hao wakiongozwa na Chacha Heche walianza kutoa lugha ya Matusi kwangu na kunitishia maisha , hali iliyosababisha Uvunjivu wa amani katika maeneo hayo ya Hoteli hiyo ,"

Katika Meza hiyo Mwandishi Samson Chacha alikuwa amekaa na Mwanasheria ambaye pia ni Afisa Ardhi wilaya ya Tarime bw, Sebastian Mangenyi, Afisa Usalama wa taifa wilaya ya Tarime bw, Nyambita , na Wakazi wengine 4 wa mji wa Sirari , ambao waliwaonya Wafuasi hao wa Chadema na Mtangazaji wa Chanel Ten Mabere kwa vitendo vyao vya kuchochea watu kutaka kufanya vurugu na kuvamia katika maeneo ya Mgodi , ambapo kundi hilo na Mwandishi huyo lilondoka huku likitishia kupambana na Mwandishi Samson ,lakini watu waliokuwepo walisema kuwa Habari ambazo zimeandikwa na Mwandishi Samson ni za sahihi sasa wao wanataka Waandishi wa kununuliwa kama Mabere Makubi kitendo ambacho kinakiuka maadili ya Uandishi wa Habari, kwani hata Mbunge Nyambari Nyangweni CCM na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Tarime waliporushiwa Mawe na kuharibiwa magari Samson aliitangaza iweje ya Lema isitangazwe waliuliza wananchi wa Sirari,

Mwandishi Samson Chacha alikwenda kituo cha Polisi Sirari na kufungua Jarada la kutishiwa Maisha namba SIR/IR /743 /2011, ambapo Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Uchunguzi unaendelea , alisema Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Costantine Massawe .
 
Back
Top Bottom