Ujinga wa utotoni

Mie nilikuwa naogopa sana wanyonya damu, duuuuuuuu! kama kulikuwa na sinema kwenye hall la Tanesco Muungano peke yangu nilikuwa siendi kabisa mpaka mabroo wawepo ndo tunaenda pamoja

dah, umenikumbusha primary school siku moja ilikuja asia comb.. Kuanzia std1 hadi 7 + baadhi ya waalimu tulikula kona saa nne asubuhi, tena kupitia madirishani.
 
wali maharage,loh!tuko wengi!pia,tulikuwa tukicheza kombolela,kama kuna mabinti,tukienda kujificha nao haturudi tena....
 
ujinga wa kwanza nakumbuka niliwahi kumdaka nyuki kwenye maua,kilichotokea ni kuvimba mkono.
 
Mi, nilikua nikiingia bafuni siogi na nawa miguu najilowesha maji sehem zinazooneka, ukinigusa mgongo wa motoo, maza akanigundua hicho kibano sitasahau.

mdau hiyo inaitwa kupiga passport size wengi tumeifanya sana
 
Nilikuwa na chupi fulani naizimia kichizi. Ilipoanza kuchakaa lastic ikakatika (si unajua chupi zetu za long time) basi nikawa nikitaka kuivaa lazima nikanunue bazoka (kwa wasiojua ni kama big G) naitafuna ikiisha utamu nabandikia chupi. Basi kila ikiachia lazima nifunue sketi niibandikize vizuri, aisee utoto noma ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Kawaida Nilikuwa nikitumwa kununua vitu kwa jumla mfano mchele,unga,n.k. Halafu nampa mbebaji sh 200 kwa kila kiloba lkn siku moja niliona nijaribu kubeba ili nichikichie nikatwishwa cha kilo 50 wakati huo niko na 14yrs lkn nilikomaa Mpaka home kufika hoi nilikitupa huko na kwenda kulala shingo iliniuma kweli mpaka nikapata homa kwa ajili ya sh 200.

Hahahaaaa, rudisha balance ye2 bana; miaka 14 kilo5o utazibebea wapi? hihihiiiiii, umetuibia bana...lakini kwa sababu ni stori za utotoni na uwongo kidogo kunogesha stori si mbaya!!
 
Nilikuwa na chupi fulani naizimia kichizi. Ilipoanza kuchakaa lastic ikakatika (si unajua chupi zetu za long time) basi nikawa nikitaka kuivaa lazima nikanunue bazoka (kwa wasiojua ni kama big G) naitafuna ikiisha utamu nabandikia chupi. Basi kila ikiachia lazima nifunue sketi niibandikize vizuri, aisee utoto noma ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Wallah vituko viko vingi duniani, chupi ubandike kwa bigijii? hihihiii!
 
Ngoja niwaibie siri ya enzi zile utotoni; najua wengi humu ni wadogo zangu sana tu, na wengine nii wanangu-stori zao za kileoleo, enzi zetu sisi hata dalalala hazikuwepo unachapa mguu kwenda skuli, au unasubiri kudandia lifti ya karandinga au landrover ya polisi!

Basi zetu ilikuwa kwenda kuogelea Ziwa Tanganyika, kuleee Bangwe, mwanaume umetoka ziwani ukikauka tu unapauka balaaa, na nyumbani wanajua mara1 kuwa ulienda kuogelea.....kibano chake balaa; basi tukagundua kutembea na kipande cha sabuni aina ya MBUNJU mfukoni, mkimaliza kuogelea mnajipakaa povu la sabuni ngozi inakakamaa na kung'aa; hapo basi usiombe ukwaruzwe na kijiti....hahahaaaa!

Enzi za kudoji shule na kuenda kupopoa maembe au kungu kwa kina Manka, hahahaaa, kwenda kuchokoza mbwa kwa "baptist" ahahaaaa! dah, nakumbuka enzi zile ukifanyiwa Birthday mnakunya Vimto na karanga!

Ebanaaaa, nilisahauuu...kupigana vita kwenye msitu wa kule nyuma ya Jeshi karibia na Kigoma Sec (Naskia siku hizi mitaa ile hakuna Msitu tena, ni Majumba tu), basi siku hiyo hamli mnashindia matunda pori na mise kijeshijeshi, kule kulikluwa na kanga wengi sana, mkikuta mtego wa watu umenasa mnaiba na kuchoma!

hhihihiii, eish Kibaba na Mama, basi Amosi (Mfanyakazi wa ndani) ananiambia "Mfanye", mimi sijui hata kufanya naanza kumfanya kinguonguo hahaaa! Enzi zile Mkiona mtu amevaa "Tafu" na Afro Kubwa mnamwita Msela Nondo!

Mojawapo ya mabasi nayakumbuka kipindikile ni Nusu Mkate...hihiiii! Bad Luck sijawahi kukutana na Rafiki yangu wa Utototni hata mmoja, sooooo baad!
 
Enzi hizo jaguar na wadogoze,mama yetu alibuni utaratibu wakati wa kula,yule wa mwisho kumaliza kula ndo atakayetoa vyombo mezani na kufuta meza.Tulikuwa tunashindana kula kwa speed ile mbaya ukichukulia watoto wote tulikuwa wakiume tu,basi jaguar akabuni utaratibu tofauti,wenzie wakisepa anabaki anafaidi minofu taaratibu bila karaha.i will never 4get those moments!

Mtuwangu unaonekana wewe ni bongeflani halafu unapenda sana kula!!! hahaaa
 
Ukaguzi J3 na Alhamisi nyie watu, mambo ya J5 ni nyie vijana wa miaka ya 90, tena unakaguliwa kuanzia kifuani kama umeoga, meno, nywele, nguo, soksi (kama una viatu). Nakumbuka ilikuwa hairuhusiwi kuvaa malapa/ndala, basi kama umevaa ndala mwanaume ikifika kwenye ukaguzi unazivua na kuzificha; kisha unajichafua miguu ili alama za ndala zisionekane.......sjui ilikuwa kipi bora kuvaa ndalla au kupekua!!!!!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom