Ujinga wa utotoni

Rosweeter

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
1,171
4,432
Nilipokuwa mtoto nilikuwa ninaogoa sana ule mwezi mkubwa wa njano, majira hayo yalipokuwa yanafika nilikuwa nina adabu sana kwani nilikuwa nikikosea tu ninafungiwa nje dk chache tu kama adhabu kwa sababu waliijua weakness yangu, kilio nilichokuwa ninakiangusha hapo siku hizi nikikumbuka nacheka sana.

Ucheki hapa lakini, unatisha ee
Lunar.jpg

Hebu wekeni wazi ujiinga wenu ulikuwaje?
 
Du me nakumbuka nilikuwa naoga kwa hiari yangu tukipika bweche na mandondo,nilikuwa nafurahi sana hasa ninapomuona mama anachambua mchele,siku hiyo naoga mapema sana alafu nikitumwa nachangamka kinoma,lakini kama ni vyakula vingine sionekani kabisa kuoga kwenyewe mpaka nilazimishwe,yaani nikikumbuka huwa nacheka sana.
 
Du usinikumbushe wali na maharage, ilikuwa tukishakula usiku tunaenda kulala, usiku wa manane mtu kadhaa mnagongana jikoni mmeurudia, teh teh teh................. utoto bwana
 
Mimi kila nilipokuwa nasikia kuna mtu kakatwa mapanga najiuliza kwa nini Mungu asingetuumba wa chuma, du sasa hivi najiuliza tungeumbwa wa chuma sijui ingekuwaje.
 
nilikuwa nalala na cousin zangu wawili, nikikojoa kitandani, naamka, nabadilisha chupi then namsogeza one of the couzin upande wangu wenye mikojo ili nisiimbiwe kindumbwe ndumbwe.
 
Du me nakumbuka nilikuwa naoga kwa hiari yangu tukipika bweche na mandondo,nilikuwa nafurahi sana hasa ninapomuona mama anachambua mchele,siku hiyo naoga mapema sana alafu nikitumwa nachangamka kinoma,lakini kama ni vyakula vingine sionekani kabisa kuoga kwenyewe mpaka nilazimishwe,yaani nikikumbuka huwa nacheka sana.[sisi kwetu cku ukipkwa wali unabakisha punje moja karibu na mdomo halafu unaenda kuwalingishia wenzio basi hapo wanakuonea wivu ile mbaya ]
 
Jumatano siku ya ukaguzi shuleni
Jumanne usiku nasugua malapa na gunzi
Naanika karibu na mafiga .. asubuhi naoga
Halafu natembea peku mpaka shuleni .
Sababu ya vumbi staki yachafuke .
Navaa malapa kengele ya mstarini ikisha
gongwa..
 
Mimi kila nilipokuwa nasikia kuna mtu kakatwa mapanga najiuliza kwa nini Mungu asingetuumba wa chuma, du sasa hivi najiuliza tungeumbwa wa chuma sijui ingekuwaje.

ningekuuza kama chuma chakavu.
 
Du me nakumbuka nilikuwa naoga kwa hiari yangu tukipika bweche na mandondo,nilikuwa nafurahi sana hasa ninapomuona mama anachambua mchele,siku hiyo naoga mapema sana alafu nikitumwa nachangamka kinoma,lakini kama ni vyakula vingine sionekani kabisa kuoga kwenyewe mpaka nilazimishwe,yaani nikikumbuka huwa nacheka sana.

Hapa kwenye beche tulikuwa wengi hee!
 
Enzi hizo cjaanza hata chekechea nikiulizwa ushaanza shule? Najibu watoto wa kiume hatuendi shule eti 7bu wakubwa wangu wote ni wa kike afu ndo nawaona wanaenda shule tu
 
Nakumbuka nikinunuliwa chupi mpya ntafanya juu chini ionekane, wakishaiona tunaanza ule mchezo wa kuroll kigauni kidogo2 kutokea magotini kuelekea mwisho wa paja na kuonyesha chupi kidogo.
 
Ule mchezo wa kupeana vyakula shuleni Kama una big g itaigawa hata Kama mpo 10 unafinyiwa kiduchu roho yako ilizike.
 
Mi, nilikua nikiingia bafuni siogi na nawa miguu najilowesha maji sehem zinazooneka, ukinigusa mgongo wa motoo, maza akanigundua hicho kibano sitasahau.
 
Du usinikumbushe wali na maharage, ilikuwa tukishakula usiku tunaenda kulala, usiku wa manane mtu kadhaa mnagongana jikoni mmeurudia, teh teh teh................. utoto bwana

by Shine
Hapa kwenye beche tulikuwa wengi hee!

Mi nadhani pengine bado sijakua kwa kuwa hapo kwenye beche na maharage hunitoi...
 
hahahahahahah usinikumbushe mana ndio ulokuwa mchezo wangu naenda kumwambia mwenye duka mama anataka mchele mzuri ulionao akauone, ananiambia chota ikifika hapo ameumia nachukua mwingi naenda kupikapika...siku 1 akanifuatilia akakuta napika alinibeba hadi home nilikula kichapo cha paka mwizi siwezi kusahau
 
Enzi hizo jaguar na wadogoze,mama yetu alibuni utaratibu wakati wa kula,yule wa mwisho kumaliza kula ndo atakayetoa vyombo mezani na kufuta meza.Tulikuwa tunashindana kula kwa speed ile mbaya ukichukulia watoto wote tulikuwa wakiume tu,basi jaguar akabuni utaratibu tofauti,wenzie wakisepa anabaki anafaidi minofu taaratibu bila karaha.i will never 4get those moments!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom