Uji wa viazi vitamu

Jimena

JF-Expert Member
Jun 10, 2015
25,844
95,792
Sio kila siku uji wa ulezi tu jamani tuwe tunabadilisha ili kutowachosha walaji

Mahitaji:

Kiazi kitamu 1
(pia unaweza kuongeza vipimo kulingana na ukubwa wa familia yako)
Maziwa fresh kikombe 1 na nusu
Sukari 1/4 kikombe
Iriki ya unga 1/4 kijiko cha chai
Karanga kiasi zilizosagwa

JINSI YA KUTAYARISHA
Chemsha kiazi kitamu ila sasa kama utatumia presha cooker basi ni hadi zile filimbi zilie mara 2 na kama una chemsha kawaida basi chemsha hadi kiive vizuri.
Baada ya kuchemsha menya maganda kisha kisage kwenye blender
Weka kiazi kilichokwisha sagwa kwenye sufuria
Weka maziwa, karanga na sukari kisha changanya vizuri hadi vichanganyike
Weka moto wa kiasi ili uji upate kuchemka vizuri
Weka Iriki na koroga tena
Punguza moto na acha kwa dakika 10 ili uji uive vizuri
Epua uji maana uko tayari sasa
 
IMG_20161101_200059.jpeg
IMG_20161101_200506.jpeg
IMG_20161101_200529.jpeg

Mtamu
 
Back
Top Bottom