TWIZAMALLYA
JF-Expert Member
- Oct 1, 2011
- 397
- 81
Hivi hiyo gas ni kwa ajili ya umeme tu hakuna matumizi mengine?.Dar kuna viwanda vingi vinaweza kuuziwa hiyo gas ili iwe mbadala wa mafuta ambayo ni ghali sana. Vilevile gas inahitajiwa dar kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya majumbani. Cha msingi tu Mtwara wasiachwe mbali sana, hiyo kampuni itakayoshughulikia gas basi ijihusishe kwenye mambo ya kijamii ya wana mtwara.likiwamo ujenzi wa mashule,hospitali,barabara nkKatika siku za karibuni husani mwaka 2000-2010 wanaharakati wamekuwa wakipiga kelele jinsi mataifa ya nje yanavyoshirikiana na baazi ya viongozi wasio waaminifu kuhamisha rasilimali za nchi kutoka tz kupeleka mataifa ya magharibi.
Mifano imejitokeza kwenye secta ya madini ambapo wawekezaji wamediriki kuchukua mchanga na kupeleka ulaya ukachekechwe kisa teknolojia ya kufanya hiyo shughuli haipo hapa kwetu.
Siku za hivi karibuni Mh. JK ameweka bayana juu ya mpango wa serikali kuweka pipeline ya gas kutoka Mtwara kuipeleka Dar ili kuzalisha umeme.Habari zilizopo ni kwamba baazi ya wakazi wa Mtwara wameanza kuhasishana kuupinga mradi huo kwa kilelezo cha kuwa kwa nini umeme usizalishwe Mtwara kisha ukasafirishwa? Kuna ugumu gani kwa hilo?.
Mara nyingi serikali kupitia viongozi wasio na uzalendo wamekuwa wakikwepesha miradi kwenye maeneo fulani na kuipeleka kwenye maeneo wanayotoka bila kujali uwiyano ktk mgawanyo wa rasilimali .Hili la mtwara kuukwepesha mradi wa ujenzi wa power plant unakwepeshwa makusudi