Ujenzi wa barabara ya Morogoro: Contractor ni third class

tulijengewa na MECCO hiyo Balabala toka Magomen mpaka Fire njia ilifungwa miezi 6 twapita kigogo..Salender..hao wazuri ndio waliojenga MANDELA ROAD hao hiyo Balabala ina Kazi nyingi kwa wakati 1 ndio maana wapo ivyo

Nakumbuka mkuu, barabara ikawa inapitia huku mapipa Mwinyimkuu hadi Madaba then bonde la kigogo, wakati ule vibaka walijaa sana nyakati za usiku pale bonde la kigogo kwenda msimbazi mpaka ilala na ile kampuni mkuu iliitwa KAJIMA na sio MECCO kama sikosei.
 
Hivi hakuna wadau wenye taaluma zao waje watujuze juu ya hili? Wapi ndugu zangu wa DART? Hebu njooni mkate kiu ya wadau hapa.
 
Naona mnalalamika sana.
Nitarudi baadae kuchangia vizuri
Ila tatizo la wabongo wao wanapenda kuona lami inamwagwa siku ujenzi unapoanza, kumbe hiyo ni hatua ya mwisho kabisa.

Ndugu wengi tunaelewa Ujenzi Huwa unasababisha usumbufu Mkubwa!! Ila kwa Hili hawa wakandarasi siwatetei kwa lolote Ng'o. Unajua huwezi Kupewa hela kwa ajili ya Traffic Diversion, na unatumia hela Hizo Kuweka Concrete posts tuu Bila utaratibu unaoeleweka!! The road reserve is Huge@! Why don't They Utilize the space by Making a new diversion road? si wanalipwa kwa kazi Hiyo? Imagine 20bil TZS Kwa Traffic diversion ni nini wamefanya? Watu tunalazimika kulala Njiani bila kufika makwetu!! Please lets shout they will start utilizing the 20bil tzs for traffic diversion!! to make things fine!! Please lets shout for our rights and others rights
 
huko kwao inawezekana ni kampuni kubwa lakini hizi branch ama franchise zao ni bomu...utaibomoa vp 35 kms road the uje uanze kuimaliza kwa pamoja?
its seems hawa kuplan mapema, hawakujua madhara ya ufungaji wa this road,

twaweza kulalamika lakini mambo mengine yanasababishwa na ubabaishaji uliopo kwenye nchi yetu swala la diversion lingewezekana kama kungekuwa na reserve ya kutosha ya barabara wakati magufuli alipotaka kubomoa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara muheshimiwa kikwete na pinda walimkataza si kwa sababu za msingi bali kwa sababu za kisiasa kwa fikra kwamba zikibomolewa CCM itachukiwa na wananchi lakini sheria zipo na magufuli alikuwa anafwata sheria lakini siasa ndiyo ilionekana kupewa kipaumbele.

kunasuala lingine la nguzo za umeme zilizopo pembezoni mwa barabara ambazo zinapaswa kusogezwa ili kupisha upanuzi wa barabara lakini imeshindikana tanesco wanadai hawajalipwa fidia lakini hata ukizisogeza unazipeleka wapi maslani eneo la mazese na hapo kimara mwisho kiutaratibu inabidi nyaya za umeme zisipite juu ya mapaa ya nyumba kwa hiyo ilibidi kwanza nyumba zibomolewe then nguzo zisogezwe na kwa hali niionavyo hata ujenzi wa mitaro na njia za waenda kwa miguu endapo nyumba hazitabomolewa itakuwa ni issue
 
Sikatai...lakini ninachosema kutakuwa na sababu nyingi tu kwanini zege limechelewa kumwagwa. Kwa mfano, zege linalotumiwa sio la kuchanganya mifuko ile ya 50kgs tuliyozoea. Ni zege special ambalo likely linatoka Wazo (Twiga Cement) for special order in some x metric tons. How come Wazo cannot deliver ? Hatujui.Kunaweza kuwa na sababu milioni. Huo ni mfano mmoja tu.

Point yangu ni kwamba lazima tuangalie msururu wote katika supply-chain ili kujua kwanini mradi unasuasua na ndiyo maana nasema sababu za kusuasua huko "most likely" zitakuwa zimesababishwa na sisi wenyewe wabongo.

Mkuu Mradi wala Haujasua sua!! Ila malalamiko yetu ni Poor Planning kwenye Highly demanding road!! Live road!! Wao wanataka tuwaone wanaweza kufanya kazi na kumaliza before time ila katika ujenzi Hili huwa ni Gumu!! Always if you plan nicely you can avoid a lot of inconveniences.
Kuna maeneo ambayo ni Highly demanding Yanahitaji Ujenzi wake Uwe wa Haraka na Umakini!! Kama kimara mwisho ambapo ni Kitovu Kikubwa cha usumbufu, Hasa Heavy Trucks!! Assume wangeendeleza hii service road ya upande wa kulia (Heading to Moro) Hadi Maeneo ya stop over si wangepunguza Msongamano Mkubwa maeneo ya Kimara Mwisho!! Hii road reserve ya Magufuli Mbona Hawaitumii wakati Hela wamepewa?? Ujenzi ni Usumbufu ila Huu umezidi!! Hela ya Diversion wametia Kibindoni!!
 
tulijengewa na MECCO hiyo Balabala toka Magomen mpaka Fire njia ilifungwa miezi 6 twapita kigogo..Salender..hao wazuri ndio waliojenga MANDELA ROAD hao hiyo Balabala ina Kazi nyingi kwa wakati 1 ndio maana wapo ivyo

Ni barabara sio balabala ..
Ila kuna uzembe mwingi sana labda tatizo ni letu wenyewe
 
Nahisis DSM huijui au maeneo ya Ubungo hadi Magomeni hupajui, kuna njia nyingi sana za mitaa ambazo zikikarabatiwa kidogo tu, basi kuanzia pale yrafiki inakuwa siyo issue, njia ni nyingi sana mkuu

njia za mitaa ni kazi ya halmashauri za manispaa, sio lawama kwa mkandarasi tena
 
Wadau, naelewa adha na hasira inayowapata lakini kuna facts nyingine tuzifahamu:

1. Strabag sio kampuni ya kujenga barabara kiwango duni. It is a 10+ billion euros company (revenue alone), employing over 76,000 staffs worldwide.

2. Strabag imeshafanya projects nyingi na kubwa ulimwenguni (e.g.Germany,UAE,Malaysia,Denmark,Libya,Cameroun,Rwanda, etc) ambazo ni kubwa kuliko hiyo project ya Dar.

3. Strabag wanatumia latest construction technologies -na kwa hili nyie ni mashahidi ya vifaa wanavyotumia kujenga hiyo Kimara-Jangwani stretch.

Ingawa sitetei kucheleweshwa ujenzi kutokana na adha watumizi tunazopata lakini kutoka na history na weledi wa kampuni kuna sababu nyingine zinazoleteleza na I can bet you zinaweza kuwa ni sisi (waTz) tunasababisha. Mfano unaweza ukakuta kuna baadhi ya vitu vimekwama bandari kwetu kutokana tu na urasimu usio na msingi.

There could numerous reasons as to why the project is stalled but the point I am trying to make is that STRABAG is a very serious company that can deliver.

Nimeweka links hapa chini na brochure that I sourced from their website.

STRABAG SE - BUILDING VISIONS. BUILDING VALUES. BUILDING EUROPE.

Mkuu hayo makampuni makubwa yakija kwenye nchi zenye serikali legelege hazifuati standards zao wanajifanyia wanavyotaka wakijua hamna wa kuwauliza
 
njia za mitaa ni kazi ya halmashauri za manispaa, sio lawama kwa mkandarasi tena

Mkuu Mtu anapopewa Hela kutengeneza Diversion roads Haijalishi inapita km Ngapi Kutoka kwenye eneo la Mradi ila Inajalisha Watumiaji wawe ni waathirika wa eneo la Mradi (Watumiaji) Hivyo Hizo 20billions za diversion Zinaweza Kutengeneza vichochoro Vingapi? Ili kuondoa usumbufu huu? The money is there what is needed is for somebody keen to ask them to utilize the intended money to construct the diversions scope!!
 
Naona mnalalamika sana.
Nitarudi baadae kuchangia vizuri
Ila tatizo la wabongo wao wanapenda kuona lami inamwagwa siku ujenzi unapoanza, kumbe hiyo ni hatua ya mwisho kabisa.

kweli kabisa....kuna watu wanajua kulalamika tu.........hawana jema.......
 
eheeeeeee nyie jamani zuri mtarijua lini au mnataka haraka kama ya mbagala? ona sasa matunda yake
 
Tatizo la Tanzania ni wizara inayoshughulikia swala zima la ujenzi wa barabara. Kwanza huwezi kufunga barabara bila kuweka alternative route ambayo inapitika. Mfano kwa sababu wanatakiwa kupanua hii barabara ilitakiwa wajenge barabara nyingine sambamba ambayo ingetumika na kuweka traffic management ili kusiwe na ajali na foleni. Then wanatakiwa wafanye kazi zao wakati magari sio mengi barabarani yaani usiku.

Huu umburukenge unaangaliwa tu na wizara bila kutoa mwongozo, wamezoea kula pesa za walipa kodi bila kufanya kazi zao inavyihitajika. Yuko wapi waziri wa ujenzi ahojiwe na kutoa kiu ya madereva na wanaoadhirika na huu ujinga ambao huyu mkandarasi analipwa pesa lukuki kwa kuweka shoddy job.
 
Jamani hata unapo karabati chumba chako mwenyewe huwa unakumbwa na usumbufu
 
Sawa ni kampuni kubwa nakubali, lakini kwa mfano kuna haja gani kufunga na kukwangua barabara kuanzia makutano ya bibititi na morogoro kuingia samora wakati hawajamaliza maeneo kama kimara, ubungo na magomeni?
 
Wadau, naelewa adha na hasira inayowapata lakini kuna facts nyingine tuzifahamu:

1. Strabag sio kampuni ya kujenga barabara kiwango duni. It is a 10+ billion euros company (revenue alone), employing over 76,000 staffs worldwide.

2. Strabag imeshafanya projects nyingi na kubwa ulimwenguni (e.g.Germany,UAE,Malaysia,Denmark,Libya,Cameroun,Rwanda, etc) ambazo ni kubwa kuliko hiyo project ya Dar.

3. Strabag wanatumia latest construction technologies -na kwa hili nyie ni mashahidi ya vifaa wanavyotumia kujenga hiyo Kimara-Jangwani stretch.

Ingawa sitetei kucheleweshwa ujenzi kutokana na adha watumizi tunazopata lakini kutoka na history na weledi wa kampuni kuna sababu nyingine zinazoleteleza na I can bet you zinaweza kuwa ni sisi (waTz) tunasababisha. Mfano unaweza ukakuta kuna baadhi ya vitu vimekwama bandari kwetu kutokana tu na urasimu usio na msingi.

There could numerous reasons as to why the project is stalled but the point I am trying to make is that STRABAG is a very serious company that can deliver.

Nimeweka links hapa chini na brochure that I sourced from their website.

STRABAG SE - BUILDING VISIONS. BUILDING VALUES. BUILDING EUROPE.
nakubaliana na wewe mkuu...jamaa Wapo vizuri kitechnologia na vifaa..hata malalamiko ya Mtoa thread hayajaangalia vigezo vingi..kumbuka Ujenzi Wa Mandela road
 
Ukweli hawa jamaa wanaojenga hii barabara ya morogoro kutoka ubungo mpaka city centre ni third class, yaani wana create unnecessary folini mji mzima
style yao inasababisha kero kubwa kwani wameanza kuivunja bara bara yote bila ya kuweka alternative roads na pia hawajali kuongoza magari
tumewahi kuona ujenzi wa bara bara zote za dar es salaam kuanzia city centre mpaka kariakoo lakini haikua kama hivi
wale jamaa walikua wanamaliza kipande kimoja baada ya chengine , wakimaliza section moja wanaanza pengine
lakini stye hii ya kuvunja barabara muhimu yenye zaidi ya kilomita 35 hii inaonesha wazi hawa jamaa hawana uzoefu wa kufanya kazi ndani jiji lenye harakati
tunaomba tanroads na city waingile kati ..kabla hawaja shindwa kama konoike na barabara ya kilwa
Mkuu update data base yako, hao Konoike hawajawahi kutengeneza barabara ya Kilwa, pengine ulimaanisha Kajima.
 
Wadau, naelewa adha na hasira inayowapata lakini kuna facts nyingine tuzifahamu:

1. Strabag sio kampuni ya kujenga barabara kiwango duni. It is a 10+ billion euros company (revenue alone), employing over 76,000 staffs worldwide.

2. Strabag imeshafanya projects nyingi na kubwa ulimwenguni (e.g.Germany,UAE,Malaysia,Denmark,Libya,Cameroun,Rwanda, etc) ambazo ni kubwa kuliko hiyo project ya Dar.

3. Strabag wanatumia latest construction technologies -na kwa hili nyie ni mashahidi ya vifaa wanavyotumia kujenga hiyo Kimara-Jangwani stretch.

Ingawa sitetei kucheleweshwa ujenzi kutokana na adha watumizi tunazopata lakini kutoka na history na weledi wa kampuni kuna sababu nyingine zinazoleteleza na I can bet you zinaweza kuwa ni sisi (waTz) tunasababisha. Mfano unaweza ukakuta kuna baadhi ya vitu vimekwama bandari kwetu kutokana tu na urasimu usio na msingi.

There could numerous reasons as to why the project is stalled but the point I am trying to make is that STRABAG is a very serious company that can deliver.

Nimeweka links hapa chini na brochure that I sourced from their website.

STRABAG SE - BUILDING VISIONS. BUILDING VALUES. BUILDING EUROPE.

Uwezo wanao ila sema wanafanya kazi nchi maskini hawawezi kusafirisha vifaa vyote muhimu vya kiteknolojia au hawawezi kutengeneza concrete wall (mfano wa matofali mapana na marefu) kwa sababu ya kuogopa gharama, ila nadhani sheria kama ipo ingeweza kutumiwa kuwabana ili itulinde sisi watumiaji wa barabara kwani tunahaki ya kuendelea kutumia barabara wakati wanaendelea na ujenzi.
 
huko kwao inawezekana ni kampuni kubwa lakini hizi branch ama franchise zao ni bomu...utaibomoa vp 35 kms road the uje uanze kuimaliza kwa pamoja?
its seems hawa kuplan mapema, hawakujua madhara ya ufungaji wa this road,

Yani hao jamaa wanavyojenga hiyo barabara utadhani ni brand new huko mapolini!
 
Back
Top Bottom