Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,534
- 8,619
Si kweli mkuu, kuna ukweli mwingi wa kifo cha udsm in re building UDOM,
mfano mzuri ni ukwapuaji wa wataalamu toka ud to UDOM, hili wanalifanikisha kwa kukiwezesha chuo cha UDOM financially, kiasi kwamba, wakimchukua lecturer ud, mshahara kidogo, akifika udom anakuwa sr. lecturer, na marupu rupu kibao, nani hapendi pesa? mwishowe walimu wazuri wanachukuliwa toka UD kwenda UDOM
Hiyo ya mlimacity sawa, lakini madhara makubwa yapo katika ukosefu wa pesa ili hali UDOM zinamwagwa kama njugu, chakushangaza vyote ni vyuo vya uma!
Naunga mkono ujenzi wa chuo kikuu dodoma ...lakini isiwe sababu ya kuuwa vyuo vyetu tulivokuwa navyo.....mwisho wa siku tukishindwa kufikia malengo dodoma tutajikuta na hivi vingine vimekufa......bajeti za vyuo vikuu vyote zipitiswe bila kupendelea vyote ni vyetu...la sivyo itajenga makundi ...na kukifanya chuo kikuu cha dodoma kijengwe kama moto wa mabua...kikakosa misingi imara ya kukifanya kiendelee baada ya wale waazilishi kuwa hawapo.....
matatizo ya wanafunzi vyuo kama sokoine ,mlimani etc yasiifanye wanasiasa wakaamua kuviacha....kwani tayari vyuo hivi vinaheshimiaka.....na tungependa pia UDOM nayo ifuate nyayo kwa kuwa chuo kikuu kikubwa kusini mwa sahara kwa ukubwa na ubora...
upanukaji wa chuo lazima uendane na muda na upimwe kwa ubora....ukiangalia chuo kikuu cha makerere kina miaka karibu 75 na kina wanafunzi 50,000......sisi tunataka kufikisha wanafunzi 40,000 ndani ya miaka 5....nafikiri kisomi hii sio sawa....ukuaji lazima uende na uzoefu ,,...na muhimu ni ubora si namba...,tutajikuta bila kuwa na misingi imara tunaanguka ,...tuwe makini na hii ni changamoto kwa wasomi pale...how do we sustain the growth in such in short life span......the test of time is always a good experimint!!!
nadhani kabla ya kufikisha wanafunzi 40,000 udom ....tungeanza na angalau 10,000 tuangalie matatizo na mafanikio ...wakisha dahilishwa [graduate] thats 4 years ..tunafanya ongezeko la asilimia 50.....na kuendelea ...ingekuwa busara kutumia miaka 15 kufikisha wanafunzi 40,000.......na wakati huo huo tukifikisha wanafunzi 50,000 mlimani.., sokoine 20,000 ,mzumbe 10,000, etc ...na kuwezesha vyuo vikuu binafsi kimazingira kutoa jumla wanafunzi 100,000 ndani ya miaka 10 ijayo.....tukiweza kupeleka asilimia 75% ya wanafunzi wenye sifa vyuo vikuu itakuwa hatua kubwa kufikia maendeleo ya kielimu......sambamaba na kutumia open university kusaidia wale walio makazini kupata sifa bila kuadhiri tija!!