Ujenzi na Siasa UNIVERSITY OF DODOMA

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Kule nako kuna madudu kibao yanaendelea na pamoja na uhuni unaofanywa na baadhi ya watu kama vile kutolipa intime ni ukweli usiopingika kuwa itakuwa ni project ambayo CCM na JK atajivunia sana.

Yote ni katika kukamilisha ilani ya uchaguzi ya 2005 ambayo sura ya 6 ibara ya 63 (b) imejieleza vilivyo

Sema nina objection kuhusu baadhi ya faculties zilivyojengwa na sijui hapa tatizo ni architect , Financier au sijui ni contractor lakini ile faculty of Medicine majengo yao yanitia kichefu chefu machoni wakati huo huo ukitazama majengo ya masomo yetu (HUMANITIES / SOCIAL SCIENCES) utaona tofauti yake ni sawa na mbingu na ardhi ukilinganisha na faculties zingine kwanza yanaonekana kuwa kazi imefanywa na watu ambao wako serious, pili ...and that so called dispensary..well, lets say sitoshangaa wakiamua kuifanyahospitali ya ma VIP

sasa challenge hapa iko kwa ma clients, consultants, architects,contractors na subcontractors.

Upande wa siasa za shule ni wazi kuwa uongozi wa chuo nao ushachoka na ziara za kustukiza zisizo kwisha za watawala kuanzia SPIKA mpaka ma DC. hawa jamaa wanatakiwa muda wao mwingi uwe kwenye mamabo ya elimu lakini haya mambo ya SPIKA sitta kupeleka shemeji zake wakapewe ziara ya chuo na uongozi ni abuse ya hali ya juu

Na wakati huo huo uongozi wa chuo (IDRISSA KIKULA na swahiba wake SHAABAN MLACHA ambaye ni Deputy Vice Chancellor, Planning, Finance and Administration) nao umekuwa na tabia za kihuni za kusema uongo mbele ya wakuu wa nchi na mfano ni ule uwongo ulisemwa na MLACHA mbele ya waziri mkuu ile ilikuwa ni embarassment kubwa kwa chuo na wanalalamikiwa na wajenzi kuwa wanawaingilia sana kwenye kazi zao...ohh how can we forget wale wahuni wengine kule Ministry of Finance? ahh anyway

sina picha lakini nikizpata nitaziweka hapa

all in all its a project ambayo we should all be proud of na challenge ni jamaa wa mipango miji kuweza kuicorporate hii project kama Nigeria walivyofanya kule Abuja amba sivyo itakuja kuwa vurugu kama sehemu zingine maana sisi kwa kuharibu tuu hatuna mfano
 
Last edited:
Usilaumu sana, consultants wanakimbizwa na wanasiasa bila kuangalia hali halisi nao wanataka hela hawawezi acha.

ndio maana utaona College ya Humanities Phase I hostel ni copy ya mabibo, hawakupewa muda wa kudesign ila wanaambiwa baada ya miezi 6 wanafunzi walale!!

Naamini hatua zitakazofuata muda utakuwa wa kutosha kwani sasa siasa ilitawala maamuzi. Kiujumla ni mradi wenye manuufaa makubwa baadae kwa jamii, shida wakandarasi wazawa hawajafaidi kwani wote ni wachina kasoro mmoja nadhani. Hii inatukosesha kukuza uchumi kwani ile pesa wanayolipwa ingezunguka na kuwekezwa nchini ajira nyingi na hali ya kiuchumi ingeguswa.
 
......NADHANI KIKWETE AMEKUWA MNO OCCUPIED NA DODOMA KIASI KUWA WANAACHA MLIMANI INAKUFA...kumbukeni mlimani kipo au kilikuwa kati ya vyuo vikuu 100 bora duniani...naambiwa sasa kinashuka kwa kasi ya ajabu....

miradi yote ya elimu ya juu lazima iende sambamba na kuimarisha ile tuliyokuwa nayo.....wote ni watoto wetu...hatuwezi kuwatenga wengine tu kwa kuwa ni watukutu....mtoto wako akikunyea hukati mkono..sasa watu wanahisi kuwa wanasiasa wana chuki na mlimani hasa kutokana na misimamo yao kisiasa...rais kikwete hajapata kufanya ziara rasmi mlimani zaidi ya kuhudhuria graduation ya rzwani na salama kama mzazi!!..hapo dodoma kila akiwa pale lazima apite UDOM...Wote wanao baba!!
 
sasa hebu niambie katika hao makandarasi wazawa wapewe tuuu hata kama hawawezi kudliever on tme na kutupatia costing ambazo ni kubwa?

Enzi za kubebana kwa sababu ni mkandarasi wa ndani tuu ndahni zishakwisha na kilichobaki ni kujitutumua

Hebu niambie wale jamaa waliodesign na kujenga ile faculty of Engineering na Medicine kweli wanapaswa kupewa kazi? wamejenga mabweni utafikiri bweni la treni

waChina wanatumia nafasi walionayo kwa sababu wanaweza kusource materials cheaply na sidhani kamasiri kuhusu sehemu za kusource hizo materials hivyo construction costs zao zinakuwa chini
 
hebu nifafanulie kwa undani na kwa data zaidi namna gani Mlimani inaachwa kufa..sijakuelewa
 
UDOM ni project nzuri na yenye tijaa..

nampongeza mtoa wazo (BWM) kwa kuwa visionary na kuhakikisha chuo kinaanzaaa....

mapungufu hayo yaweza kurekebishwaa tuu kwani lengo ni muruaa sanaaaa...

sipendi kukumbuka mfumo wetu wa elimu ya juu ulivyokuwa wa kibaguzii kwa kuweza kuchukua wanafunzi wachache tuuu kati ya wengi waliofauluuuuu...mungu apitishie mbaliii dhahma ileeee...tunasongaaa sasa
 
halafu wale ma armchair critics ambao hawajawahi kukanyaga ardhi ya Tanzania wanapiga kelele ohh CCM haina inachokifanya! hakuna anayekataaa kuna matatizo kwenye system lakini ukiwa on the ground mazuri yanayofanyika lazima ukubali kuwa wako mbele kukamilisha ilani ya uchaguzi ya 2005
 
halafu wale ma armchair critics ambao hawajawahi kukanyaga ardhi ya tanzania wanapiga kelele ohh ccm haina inachokifanya!

1-....................

2-.....................

3-.....................

4-.....................

5-.....................

?????/??/?????????
 
......NADHANI KIKWETE AMEKUWA MNO OCCUPIED NA DODOMA KIASI KUWA WANAACHA MLIMANI INAKUFA...kumbukeni mlimani kipo au kilikuwa kati ya vyuo vikuu 100 bora duniani...naambiwa sasa kinashuka kwa kasi ya ajabu....

miradi yote ya elimu ya juu lazima iende sambamba na kuimarisha ile tuliyokuwa nayo.....wote ni watoto wetu...hatuwezi kuwatenga wengine tu kwa kuwa ni watukutu....mtoto wako akikunyea hukati mkono..sasa watu wanahisi kuwa wanasiasa wana chuki na mlimani hasa kutokana na misimamo yao kisiasa...rais kikwete hajapata kufanya ziara rasmi mlimani zaidi ya kuhudhuria graduation ya rzwani na salama kama mzazi!!..hapo dodoma kila akiwa pale lazima apite UDOM...Wote wanao baba!!

Mlimani inajiua yenyewe, viongozi wake hawana vision, otherwise hakuna mwingiliano na Dodoma University hapo.
mbona hujauliza walifanikishaje Mlimani City? na mipango ya mwanzo ilikuwaje na je ndiyo hali ilivyo sasa kwenye hiyo project ambayo ipo kwenye plots zao?
viongozi wetu mara nyingi wanasahau wajibu wao na pia wanashindwa kupanga kufuatana na priorities
 
sasa hebu niambie katika hao makandarasi wazawa wapewe tuuu hata kama hawawezi kudliever on tme na kutupatia costing ambazo ni kubwa?

Enzi za kubebana kwa sababu ni mkandarasi wa ndani tuu ndahni zishakwisha na kilichobaki ni kujitutumua

Hebu niambie wale jamaa waliodesign na kujenga ile faculty of Engineering na Medicine kweli wanapaswa kupewa kazi? wamejenga mabweni utafikiri bweni la treni

waChina wanatumia nafasi walionayo kwa sababu wanaweza kusource materials cheaply na sidhani kamasiri kuhusu sehemu za kusource hizo materials hivyo construction costs zao zinakuwa chini
Sasa wewe unataka hao makandarasi wazawa from nowhere wawe na uwezo wa kudeliver on time na waweze kumeet quality and cost standards bila ya kupeewa hizo kazi na support ya umma (silikali) ili wapate uzoefu na mitaji mikubwa?
Jiulize hao wachina wameanzia wapi... au unafikiri wamwanzia Dodoma?
 
Si kweli mkuu, kuna ukweli mwingi wa kifo cha udsm in re building UDOM,
mfano mzuri ni ukwapuaji wa wataalamu toka ud to UDOM, hili wanalifanikisha kwa kukiwezesha chuo cha UDOM financially, kiasi kwamba, wakimchukua lecturer ud, mshahara kidogo, akifika udom anakuwa sr. lecturer, na marupu rupu kibao, nani hapendi pesa? mwishowe walimu wazuri wanachukuliwa toka UD kwenda UDOM

Hiyo ya mlimacity sawa, lakini madhara makubwa yapo katika ukosefu wa pesa ili hali UDOM zinamwagwa kama njugu, chakushangaza vyote ni vyuo vya uma!
 
Sasa wewe unataka hao makandarasi wazawa from nowhere wawe na uwezo wa kudeliver on time na waweze kumeet quality and cost standards bila ya kupeewa hizo kazi na support ya umma (silikali) ili wapate uzoefu na mitaji mikubwa?
Jiulize hao wachina wameanzia wapi... au unafikiri wamwanzia Dodoma?

mbona sekta zingine wazawa wameweza?

tatizo ni kuwa ma archietcts wetu walikuwa wapo kwenye comfort zones na sasa baada ya hii sekta kufunguka kwa wengine wanaishiwa hawawezi kucompete kwenye hii competitive market sasa wapewe tuu kwa sababu ya uzawa?

Hivi ushaona majengo mengi yaliyokuwa designed na local architectss? acha tuuu. hao akina MD Consultancy na wengineo they have yet to buld anything utakachosema kuwa ni worth it

Mfano tazama jengo jipya la ARECO pale samora, ni zuri kwa kulitazama lakini unajiuliza how energy friendly will it be? ukwli ni kuwa hakuna kitu kama lile la pale Bibi Titi MOhammed

kwa kuanza wangeanza kumerge na makampuni ya nje ili wapate ujuzi na connections zaidi kuliko kukngangania kufanya boashara kizamani.
 
Ni kweli kabisa siasa imo ndomaana kuna dharau, viburi tele na kutojaliana, watu hawathaminiani wengine elimu ndogo lakini mishahara juu mno na wengine elimu kubwa mshahara kiduchu kama sio siasa ni kitu gani? pachunguzwe kwa kweli hata kama siasa ndo iko kunyanyasa wafanyakazi?????? Lengo lao la kuanzisha chuo ni zuri lakini uongozi uliopo labda tuseme ndo una shida au ndo siasa zenyewe???!!!! wengine wako juu ya sheria, halii ikiendelea kwa sasa UDOM iko juu lakini baada ya miaka michache itazimika kama mshumaa katika upepo mkali maana walimu wameshaanza kuacha kazi wenyewe, CCM amka usichanganye siasa na elimu
 
mbona sekta zingine wazawa wameweza?[/QUOTE]

ujenzi ni kitu tofauti kulinganisha na sekta nyingine mkuu!unajua hawa clients wetu(mashirika ya uma,LAPF,NSSF,PSPF) they have only one criteria kumchagua mkandarasi:THEY WILL ALWAYS FO FOR THE LOWEST BIDDER!

chinese companies will always quote very low,kwa sababu kubwa mbili:
-materials zao wanazisource kwao kwa cheaper price,tena kwa EXEMPTION YA DUTIES

-labour charge yao ni ndogo sana!MFANO CRJE,ni kampuni ya serikali ya uchina,wamefinanciwa equipments za kutosha(plants),na labourers wao ni criminals huko kwao wakija huku hawalipwi chochote ,nadhani ni allowance ya 30usd.

Pia wanahonga sana wachina hawa!wanakuwa wanajua mradi tangu ukiwa kwenye visibility study

Sasa mzawa atashindana vipi na huyu mchina,KAMA SERIKALI HAIJAWEKA SERA NZURI YA KUWAWEZESHA WAZAWA?

kama serikali haitaingilia kati basi makampuni yetu wazawa yatakufa NATURAL DEATH
 
halafu wale ma armchair critics ambao hawajawahi kukanyaga ardhi ya Tanzania wanapiga kelele ohh CCM haina inachokifanya! hakuna anayekataaa kuna matatizo kwenye system lakini ukiwa on the ground mazuri yanayofanyika lazima ukubali kuwa wako mbele kukamilisha ilani ya uchaguzi ya 2005

nyerere amekaa 24yrs ameacha mlimani, muhimbili, ifm, mzumbe, dat tech, changombe and more.......
na bado elimu na matibabu yalikuwa bure, na wataalamu walikuwa kidogo kwa ajili ndio alikuwa anawasomesha

tokea ameondoka leo hii ni miaka 24yrs tunachoonyeshwa ni UDOM ambayo bado haijamalizika
matibabu, elimu vya kulipia migodi kila kona, kuna vat halafu hata UDOM inashindwa kumalizika

hamna kazi inayofanyika TZ
 
GT ili nakubaliana na wewe, wazawa hafanyi kazi vizuri, hata ukimpa project ndogo haimaliziki....

wazawa watoswe mpaka wajue kufanya kazi vizuri, anakuangalia usoni kabla hajakutajia bei
 
sasa hebu niambie katika hao makandarasi wazawa wapewe tuuu hata kama hawawezi kudliever on tme na kutupatia costing ambazo ni kubwa?

Enzi za kubebana kwa sababu ni mkandarasi wa ndani tuu ndahni zishakwisha na kilichobaki ni kujitutumua

Hebu niambie wale jamaa waliodesign na kujenga ile faculty of Engineering na Medicine kweli wanapaswa kupewa kazi? wamejenga mabweni utafikiri bweni la treni

waChina wanatumia nafasi walionayo kwa sababu wanaweza kusource materials cheaply na sidhani kamasiri kuhusu sehemu za kusource hizo materials hivyo construction costs zao zinakuwa chini

Ni kweli kuwa wazawa hakuna wengi wenye uwezo kama wachina ila kuwajengea uwezo ni lazima. hao wachina (na yeyote mgeni) wangelazimishwa kufanya joint venture na wazawa ili baada ya muda tusirudi kwao tena.

hao wachina nakuambia bei ni ndogo kwa sababu ya vitu vyao vya kichina ambovyo vinapendeza kwenye macho lakini kiukweli si imara kama inavyotakiwa. Pia wengi wanaunderprice ili kupenya kwenye soko, kiujumla kwenye ujenzi si watu kuwaendekeza.

Hao waliodesign matreni huwezi sema wasipewe kazi tena, design ni haivutii ila ilikubalika. kwani ni lazima upeleke design ya awali ili upate ridhaa ya mteja.
 
Back
Top Bottom