Ujenzi Mkubwa unaoendelea Kigamboni(Dege Eco Village), ni mradi wa nani?

Wakuu je maeneo ya mwembe mdogo inakuwaje haya maeneo yapo powa kununua au hayafai kununua???na maeneo gani ambayo kwa sasa yanafaa kununuliwa???

Naombeni msaada wenu

Njoo tu Mwembemdogo ni salama
 
Dr F. Ndugulile, hongera sana.

Unaondoa sintofahamu nyingi sana kwa wakazi/wawekezaji wa kigamboni. Inasaidia kumwezesha mtu kujipanga accordingly.

Maana kuna wengine walishaanza kufunya wakijua fidia za mil 250 zinakuja mwaka huu
 
Ningependa sana kusikia majibu ya Mh Ndugulile kwa swali la king kong kuhusu bwana Aqbal kumiliki mashamba kwa zaidi ya miaka mitatu bila kuyaendeleza na bado anatazamwa tu.. Kwa nini sheria haichukui mkondo wake?
 
Last edited by a moderator:
Pia mheshimiwa mbunge naomba utujuze mipango iliyopo ya kufikisha umeme mwasonga
 
Asante ndugu mbunge.niulize jambo dogo.je makadirio ya fidia na ujenzi yanakadiriwa kuwa trilion ngapi.umesema wananchi hawakopesheki je hii ni kigamboni yote au eneo la mji mpya tu.pili umesema zuio lilikoma tangu 2010 sasa kwanini usihamasishe watu kuendelea na ujenzi
 
Kuna jamaa zangu kisarawe 2 wametaka kupima wakaambiwa hakupimiki.hata mimi nimenunua eneo kisarawe 2 surveyor wa temeke akaniambia siwezi kupima labda nito rushwa kubwa hii imekaaje mkuu
 
Mh.mbunge je hizi nyumba 7000 ni za kuuza. Kupangisha au kukopesha.lakini je vipi huduma zingine za msingi humo ndani ni zipi.nakumbuka bango lake kama Nssf haonekani au sikusoma vizuri
 
Mh.mbunge hebu tujuze kuhusu upanuzi wa barabara toka feri hadi kimbiji na kongowe.maana juzi natokea mji mwema usiku karibia kugongana barabara ni finyu.hiyo inatakiwa walau njia 6 kwa kuanzia
 
Mh.mbunge hebu tujuze kuhusu upanuzi wa barabara toka feri hadi kimbiji na kongowe.maana juzi natokea mji mwema usiku karibia kugongana barabara ni finyu.hiyo inatakiwa walau njia 6 kwa kuanzia

Duh! Njia 6 Kwa kuanzia, halafu baadae ziongezeke mpaka ngapi? Na Kwa sababu gani? Barabara gani TZ leo ina zaidi ya njia nne?
 
Wa riziwani kikwete... umefurahi sasa sio..
Umekaa kiu nafiq nafiq tu....husda na umbea umewajaa...
 
Wana jamvi kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa magorofa unaendelea Kigamboni. Ni Kigamboni ndandani mbele Zoo. Wengi wa wafanyakazi ni wazungu wenye asili ya Kigiriki. Kazi inafanyika usiku na mchana. Wenye ukweli kuhusu mradi huo mtujuze. Karibuni wanajamvi.

Dah..... yaaani taarifa zote zile zilizotoka hata kabla ya mradi haujaanza hamkuwa na habari kweli watanzania ni vilazaaaaaaaa.
Hivi hamuna habari kuwa kigamboni inataka kubadilishwa kuwa mji wa kimataifaa mambo ndio hayoo yanaaanza
 
Pia mheshimiwa mbunge naomba utujuze mipango iliyopo ya kufikisha umeme mwasonga

Kwa sasa umeme umefikia eneo la Camel Oil. Nimewataka Tanesco kuingiza kwenye Mipango yao mradi wa kufikisha umeme Mwasonga.
Kwa kupitia mradi umeme vijijini (REA) maeneo ya Kimbiji na Kisarawe II yatapata umeme. Kazi hii kwa sasa inaendelea.
 
Asante ndugu mbunge.niulize jambo dogo.je makadirio ya fidia na ujenzi yanakadiriwa kuwa trilion ngapi.umesema wananchi hawakopesheki je hii ni kigamboni yote au eneo la mji mpya tu.pili umesema zuio lilikoma tangu 2010 sasa kwanini usihamasishe watu kuendelea na ujenzi

Makadirio ya fidia ni takribani Trillioni 15, inakaribia bajeti ya Taifa.
Hakuna Sheria wala kizuizi cha kukuzuia kuendeleza ardhi yako.
 
Kuna jamaa zangu kisarawe 2 wametaka kupima wakaambiwa hakupimiki.hata mimi nimenunua eneo kisarawe 2 surveyor wa temeke akaniambia siwezi kupima labda nito rushwa kubwa hii imekaaje mkuu

Ni kweli. Tulikuwa tunasubiria Masterplan Mpya ya Mji wa Dar Es Salaam. Natumai upimaji utaanza tena hivi karibuni.
 
Mh.mbunge je hizi nyumba 7000 ni za kuuza. Kupangisha au kukopesha.lakini je vipi huduma zingine za msingi humo ndani ni zipi.nakumbuka bango lake kama Nssf haonekani au sikusoma vizuri

Nyumba zitauzwa kwa Wanaotaka. Kama utahitaji maelezo ya ziada, ni-PM nikuunganishe na wahusika.
 
Mh.mbunge hebu tujuze kuhusu upanuzi wa barabara toka feri hadi kimbiji na kongowe.maana juzi natokea mji mwema usiku karibia kugongana barabara ni finyu.hiyo inatakiwa walau njia 6 kwa kuanzia

Niliomba upanuzi wa Barabara toka Kokoto-Kongowe. Kutokana na ufinyu wa Bajeti, hili halikufanyika. Hakuna mpango kwa sasa wa kupanua barabara za Feri-PembaMnazi na Mjimwema-Kongowe.
 
Back
Top Bottom