Wana jamvi,
Kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa magorofa unaendelea Kigamboni. Ni Kigamboni ndandani mbele Zoo na naambiwa unaitwa "Dege Eco Village".
Wengi wa wafanyakazi ni wazungu wenye asili ya Kituruki. Kazi inafanyika usiku na mchana.
Wenye ukweli kuhusu mradi huo mtujuze.
Karibuni wanajamvi.
=====
BAADHI YA MAJIBU:
MBUNGE:
====
MDAU:
Kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa magorofa unaendelea Kigamboni. Ni Kigamboni ndandani mbele Zoo na naambiwa unaitwa "Dege Eco Village".
Wengi wa wafanyakazi ni wazungu wenye asili ya Kituruki. Kazi inafanyika usiku na mchana.
Wenye ukweli kuhusu mradi huo mtujuze.
Karibuni wanajamvi.
=====
BAADHI YA MAJIBU:
MBUNGE:
Ni mradi wa ujenzi wa nyumba takribani 7,000. Mradi huu ni ubia kati ya kampuni ya Azimio na NSSF.
Bw Iqbal ni mwenye eneo hilo na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Azimio.
Dkt Faustine Ndugulile
MB-Mbunge Kigamboni
====
MDAU:
Jamani huyo ni Iqbal mdogo wake na Bahgdad aliyefungwa kwa rushwa.
Iqbal ni kijana mdogo tu na ndiye aliwahi kupewa eneo la Mnazi Mmoja. Alikuwa rafiki mkubwa mno na meya wa Dar wakati huo, Kitwana Kondo.
Hayo mambo ya kampuni ya Azimio ni mchongo tu, mradi wa mji wa kisasa wa Kigamboni ni wa George Bush mtoto. Na amekuwa akija hapa nchini kimya kimya hadi anamaliza siku sita kufuatilia mradi wake.
Mradi huu unaouzungumzia, wa NSSF na Azimio ni magumashi kama yale ya Manji na NSSF. TUSUBIRI.
Jiulizeni huko Kigamboni huyo mwarabu Iqbal na mwenzake Manji wamenunua maeneo makubwa mno ya ardhi na ndiyo ati wanaingia ubia na miradi ya mashirika ya umma.
Wanachukua ardhi ya umma wanaiuzia serikali, nchi hii!
Kwa taarifa yenu, ukanda wote wa Pwani (karibu kilometa 300) toka Kigamboni hadi Mtwara umeshanunuliwa WOTE na vigogo serikalini ili kuvizia wawekezaji na kuwinda ule mradi mfu wa Mtwara Dev. Corridor.