Ujenzi holela Dar-Sinza Africa Sana

kiroba

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
324
114
hapa jamaa wameamua kufunga barabara ili wenyewe waendelee na ujenzi. Jamani hii nchi yetu inanuka rushwa! Angalia hiyo attachment nimeweka picha.
 
Attachments

  • 01032012.jpg
    01032012.jpg
    203.7 KB · Views: 650
Nchi ina laana hii..ukienda mamlaka husika watakuambia upuuzi mtupu..ndio mana mm napendekeza tulianzishe tu ili watu watii sheria...
 
Watu wa ardhi wpo, serikali ipo! Inasikitisha 97% ya jiji la Dar lina makazi holela ambayo hayajapimwa!
 
Naomba mtume malalamiko kwa mamlaka inayohusika, unaweza kukuta mkuu wa serikali ya mtaa tayari ameshanunuliwa.
 
Halmashauri ya Kinondoni IMEOZA ,imejaa watendaji wabovu na wala rushwa; wao ndio wanaoharibu ramani za mji kwa kufanya CREATIONS za viwanja sehemu za wazi na pia kufumbia macho wenye pesa wanapojenga mpaka kuziba barabara za watu kupita; Mfano mzuri ni pale Jangwani beach mtu amejenga ukuta maksudi na kuziba barabara na malalamiko ya wananchi mpaka kwa waziri hayajafanyiwa kazi.!!Iliyobaki sasa ni wanannchi kujichukulia shera mkononi na kuvunja hizi kuta.
 
sina uhakika na sheria ila malipo hufanyika manispaa kwa kufunga barabara
hata kama ni msiba lazima ulipie manispaaa!!!!
 
Halmashauri ya Kinondoni IMEOZA ,imejaa watendaji wabovu na wala rushwa; wao ndio wanaoharibu ramani za mji kwa kufanya CREATIONS za viwanja sehemu za wazi na pia kufumbia macho wenye pesa wanapojenga mpaka kuziba barabara za watu kupita; Mfano mzuri ni pale Jangwani beach mtu amejenga ukuta maksudi na kuziba barabara na malalamiko ya wananchi mpaka kwa waziri hayajafanyiwa kazi.!!Iliyobaki sasa ni wanannchi kujichukulia shera mkononi na kuvunja hizi kuta.

ukifuatilia sana utakuta ni system nzima anzia top mpaka bottom MEMO zinatembea kwa kwenda mbele!
 
Kama spika wa bunge amefunga barabara kwa nini na sisi tusiweze?
 
Ghorofa kubwa hazina hata parking...tunaishia kuacha magari Ambiance
 
Hivi Afrika Sana ni Sinza ama Mwenge?

Mimi miaka yote napajua kama Mwenge!
Africa sana ni Sinza mkuu.
Lakini si ajabu maana maeneo ambayo yapo mpakani mwa eneo moja na lingine huwa yana utata sana kuyaainisha kuwa yapo wapi?
 
Nini hiyo baba nenda Mbezi kwa Msuguri, Jamaa kajenga kwenye hifadhi ya barabara, kawekewa X abomoe. Kwa jeuri kawapa Serikali ya mtaa chumba kama ofisi akamalizia kujenga na sasa anaendelea bila wasi wasi wowote ule
 
Back
Top Bottom