Ujazaji wa form za Board ya Mikopo kwa wanaotaka kujiunga na vyuo

Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
523
360
Wakuu nimejaribu kwa muda wa week nzima sasa kujaribu kujaza form za mkopo kwa ajili ya ya ndg yangu anayetarajia kujiunga chuo mwaka huu. Licha ya kufanikiwa kupata Password na username baada ya kujaza preliminary information lakini imeniwia vigumu ku log in tena. Kila nikijaribu ku log in naambiwa
Sorry, either your username or password is not valid!

Lakini nikiangalia username ipo sahihi na katika mfumo uleule wanaoutumia yaani
(e.g. S0143.0078.1990). Licha ya kupewa option ya kureset password kwa kuchagua swali nililoulizwa na kutakiwa kujibu jibu lile lie nililojaza, nimefanikiwa kupewa password mpya lakini nazo nikizitumia hazinisaidii zaidi ya kupewa message hiyo juu. Sasa najiuliza tatizo liko wapi?
Nimejaribu kufill upya form naambiwa hiyo namba ipo regestered tayari kwa sababu ni ileile. Nikireset password inakubali na napewa nyingine ila nikiitumia hainiwezeshi kufungua ili niendelee kujaza form.
Je kuna mtu amekumbana na tatizo kama hili?
Je kuna mtu anajua jinsi ya kulitatua anisaidie!
Nimejaribu kupiga simu kwenye hizo number walizotoa kwenye website yao kwa wanaohitaji msaada lakini hazikupatikana zote na hapo ilikuwa mchana ndani ya muda wao wa kazi.
Nisaidieni ili niwezekumsaidia huyo mtu na jinsi ya kumsaidia ni lazima nijaze form za bodi ya mikopo.
 
"Je kuna mtu amekumbana na tatizo kama hili?" limenikuta sana mpaka sasa sijapata solution yake, ukifanikisha tujuze jinsi ya ku deal nalo. Hizi ndo system zetu mkuu
 
hawaw bodi wamerkia technologia ambayo hawaiwezi, kutakuwa na mapungufu kibao tu kwenye hizo fomu
 
Mie naona wajihudhuru 2 mana hakuna wanalofanya? Mkubwa tatizo hilo ni sugu kwa hawa maboc .endelea kuhagaika uckate tamaa.hao ndo zao.
 
Pengine muda wa kuomba udhamini haujafika. ninavyofahamu mpaka mwezi wa April.
 
Back
Top Bottom