Ujauzito, utoro wawakosesha masomo wanafunzi 87 Iringa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
pregnance%287%29.jpg

Ujauzito



Zaidi ya wanafunzi 87 wa Shule ya Sekondari Pawaga iliyopo wilaya ya Iringa Vijijini mkoani hapa, wameshindwa kuhitimu kidato cha nne kutokana sababu kadhaa zikiwemo ujauzito na utoro.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki katika mahafali ya kuhitimu elimu ya sekondari shuleni hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa Afisa Elimu wa Mkoa wa Iringa, Salumu Maduhu.
Akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Omari Mtembe alisema walipoanza kidato cha kwanza mwaka 2007 walikuwa wanafunzi 200 na hivi sasa wanahitimu 113 tu.
Alisema tatizo lingine linaloikabili shule hiyo ni ukosefu wa maji na kwamba yaliyopo kwa

matumizi ya binadamu si safi na salama.
Mtembe alisema pamoja na kutokuwa safi na salama, lakini maji hayo yanapatikana umbali wa zaidi ya kilomita nne kutoka shuleni hapo.
Alisema umbali huo unasababisha miongoni mwao kuchelewa masomo darasani hasa nyakati za asubuhi.
Kero nyingine zilizotajwa kuwaathiri wanafunzi hao ni ukosefu wa huduma za afya na usafiri.

Mtembe alisema uvamizi wa wanyama wakali ni sehemu ya matatizo yanayowakabili..
Alitoa mfano kuwa wanafunzi wawili walipoteza maisha shuleni hapo kwa kuvamiwa na kuuawa na tembo, hali inayochangiwa na ukosefu wa uzio.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Frank Mahenge, alithibitisha taarifa zilizotolewa na mwanafunzi huyo.

Kuhusu idadi ya wanaoshindwa kuhitimu kidato cha nne, alisema wengi wao wanatokana na ujauzito, ingawa hakutoa takwimu rasmi.
Pia Mahenge alisema vifo vya wanafunzi waliouawa na tembo ni tatizo linalowakabili pia wakazi wa vijiji vilivyo karibu na shule hiyo.

Mahenge alisema tatizo la utoro linarudisha nyuma maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi hao na kwamba zaidi ya asilimia 10 ya wanaochaguliwa kujiunga na kitado cha kwanza hawafiki shuleni kila siku.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Iringa, Salumu Maduhu, alisema ni jambo jema kwa shule wasichana wa shule kuongoza kitaaluma hasa kwa masomo ya sayansi.
Alisema kutokana na hali hiyo, wazazi wanapaswa kujitahidi na kuhakikisha watoto wanaendelea vema kielimu.




CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom