Ujambazi

Mahmood

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
7,909
2,477
Kuvizia njiani na kunyang`anya mali za watu kwa nguvu yaani ujambazi ni kati ya madhambi makubwa sabini.

Na yule atakaefanya ujambazi basi ajue kwamba anapigana vita na Mweyezi Mungu S.W.T. na Mtume Wake S.A.W.. Adhabu yake duniani ni kufuatana na kitendo alichokifanya Mfano mmojawapo, jambazi akiuwa ahukumiwe kuuawa. Na adhabu ya Akhera inayomgoja ni kubwa sana. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Maaida aya ya 33,

"Basi malipo ya wale wanaopigana na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (kwa kufanya aliyowakataza) na kufanya uovu katika nchi, ni kuuawa au kusulubiwa au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho; (mkono wa kulia kwa mguu wa kushoto, na mkono wa kushoto kwa mguu wa kulia) au kuhamishwa katika nchi. Hii ndiyo fedheha yao katika dunia; na Akhera watapata adhabu kubwa."

Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu adhabu ya ujambazi hukumu yake ni kama ilivyokuja katika Qur-ani katika Suratil Maaida aya ya 33.

Sheikh Abdallah bin Saleh Al-Farsy ameelezea kuwa akatiwe shauri kwa mujibu wa kitendo alichofanya yule jambazi.

Na hukumu yenyewe ni hii ifuatayo:

1) Ikiwa kauwa tu bila kuchukua mali ya mtu. Hukumu yake ni kuuawa.

2) Ikiwa kauwa na kachukua mali ya mtu. Hukumu yake ni kuuawa na kusulubiwa.

3) Ikiwa kanyang`anya mali tu bila kuuwa mtu. Hukumu yake ni kukatwa kiganja chake cha mkono wa kulia na unyayo wa kushoto au kukatwa kiganja chake cha mkono wa kushoto na unyayo wa kulia.

4) Ikiwa hakuuwa wala hakunyang`anya mali ya mtu, ila kutaabisha watu na kuwatisha. Hukumu yake ni kutolewa nchini na kufungwa nchi nyingine. Au afungwe nchini.
 
Back
Top Bottom