Ujambazi ,ujambazi tatizo nidhamu/haraka ya maisha bora ya kikwete??

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,050
Majambazi Wateka Basi Kigoma, Wapora Mamilioni
3582226.jpg

Friday, November 20, 2009 9:43 PM
Majambazi wawili wenye silaha za moto wameteka basi la abiria mkoani Kigoma na kupora mamilioni ya pesa na mali zingine mbali mbali.Majambazi wawili wenye silaha za moto aina ya SMG, jana waliteka basi la abiria katikati ya kijiji cha Muyama na Mnyegera wilayani Kasulu mkoani Kigoma na kisha kupora vitu mbali mbali zikiwemo fedha na simu.

Taarifa za jeshi la polisi mkoani Kigoma zimelitaja gari lililotekwa kuwa ni Toyota Costa lenye namba za usajili T 248 AHA mali ya Lojin Msama Zihuye mkazi wa Kasulu mjini lililokuwa likitokea Muyama kwenda Kasulu.

Imebainishwa kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa mbili asubuhi katika mlima Kabuye ambapo dereva wa gari hilo Bw. James Ngirante alilazimishwa kusimamisha gari akitishiwa kupigwa risasi.

Jeshi la polisi limeeleza kuwa katika tukio hilo majambazi wamefanikiwa kupora simu za mkononi zenye thamani ya shilingi laki nne na elfu kumi pamoja na pesa taslimu shilingi milioni 2.4 wakati thamani za mali zingine za watu zilizoibwa shilingi 2.8.

Katika ujambazi huo wahusika wanauhusisha na uwepo wa wakimbizi katika wilaya ya kasulu ambapo majambazi walidaiwa kuongea kwa lafudhi ya Kirundi na hivyo kupelekea kuwepo kwa hisia kuwa raia wa Burundi ndio wanaendesha uhalifu mpakani mwa Tanzania.

Aidha hakuna mtu aliyejeruhiwa, ingawa inatajwa kuwa huenda tukio hilo lilipangwa kutokana na majambazi hao kuwataja baadhi ya abiria kwa majina wakiwataka kutoa fedha.

Hadi sasa hakuna anayeshikiliwa kutokana na ujambazi huo na jeshi la polisi limepeleka kikosi maalumu katika tarafa ya Muyama kufanya uchunguzi utakaowezesha wahusika kukamatwa.
 
m nahisi soon inabidi tuake nao chini tujue tatizo ni nini??aiwezekani kila siku ujambazi kila siku...hawa polisi wanalinda wake zao??lipo tatizo moja kigoma polisi nao ni moja ya matatizo kule wengine unakuta wako dhamu wanaingia porini asbh wanarudisha silaha...je tatizo ni kwa nani???
kazi kwako mwema
 
Back
Top Bottom