Ujambazi staili mpya, waja na defender , waiba mchana kweupe saa sita

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
tukio la kusikitisha limetokea Bunju beach Masaiti, baada ya majambazi kuja na stail mpya, staili waliohitumia ni kuchukua Defender kama ya Police na kuchukua kijana mmoja kujifanya amewekwa chini ya ulinzi nakuelekea kama kwambwa anaweza kuwaonyesha watuhumiwa wengine walipo, baada ya kufika eneo la tukio wakatoka wakiongozana na kijana aliyeshikiliwa kuelekea eneo la tukio, walipofika wakagonga, housgeli akawafungulia, wakamwambia awaonyeshe chumba cha boss wake, wakabomoa mlango na kukomba vitu vyote vya chumbani wakijifanya ni vya ushahidi, wakapanda defender na kutokomea, vijana waliowaona walikimbia hovyo wakizani polisi wanatafuta wavuta bangi.
House g. alipopiga simu na kuweleza bosi, na kubonyeza kitufe cha Ultimate Security walikuta walipishana nao wakidhani ni mapolisi wanasaidiana kutafuta watuhumiwa. Ilikuwa kama sinema. Aliyeibiwa kweli anaonekana anazo sana kwa kuwa eti ni mkurugenzi kampuni ya madini.

Fundisho.
Watu wengi wanapopata vipesa hujifanya kuweka mikwara ya ulinzi, wengi wao hawana ushirikiano na majirani, eneo hili jamaa wengi wanajifanya vibopa, wanasusia ulinzi shirikishi, umoja, uelewano mzuri na majirani. Huyu aliyeibiwa, hatoagi michango ya ulinzi wala ya umoja wa wanabunju, alipopatwa na tatizo ndipo anaaaha kuomba kujiunga. Acheni maringo jenga jamii.
 
Maelezo mengi sana ila ujumbe 2shaupata,unapgia kampeni ulinz shirikshi ndo unaponda wanaoweka walinzi.mi ninao MBWA WATANO sihtaji ushrikiano na mtu yeyote katika ulinzi
 
tukio la kusikitisha limetokea Bunju beach Masaiti, baada ya majambazi kuja na staomoa ili mpya, staili waliohitumia ni kuchukua Defender kama ya Police na kuhukua kijana mmoja kujifanya amewekwa chini ya ulinzi nakuelekea kama kwambwa anaweza kuwaonyesha watuhumiwa wengine walipo, baada ya kufika eneo la tukio wakatoka wakiongozana na kijana aliyeshikiliwa kuelekea eneo la tukio, walipofika wakagonga, housgeli akawafungulia, wakamwambia awaonyeshe chumba cha boss wake, wakabomoa mlango na kukomba vitu vyote vya chumbani wakijifanya ni vya ushahidi, wakapanda defender na kutokomea, vijana waliowaona walikimbia hovyo wakizani polisi wanatafuta wavuta bangi.
House g. alipopiga simu na kuweleza bosi, na kubonyeza kitufe cha Ultimate Security walikuta walipishana nao wakidhani ni mapolisi wanasaidiana kutafuta watuhumiwa. Ilikuwa kama sinema. Aliyeibiwa kweli anaonekana anazo sana kwa kuwa eti ni mkurugenzi kampuni ya madini.

Fundisho.

Watu wengi wanapopata vipesa hujifanya kuweka mikwara ya ulinzi, wengi wao hawana ushirikiano na majirani, eneo hili jamaa wengi wanajifanya vibopa, wanasusia ulinzi shirikishi, umoja, uelewano mzuri na majirani. Huyu aliyeibiwa, hatoagi michango ya ulinzi wala ya umoja wa wanabunju, alipopatwa na tatizo ndipo anaaaha kuomba kujiunga. Acheni maringo jenga jamii.

Kama anajionapa ndio yeye basi na ajilinganishe na hilo lililompata sasa!

Hapo ni Bongo hakuna shamba wala ni kichwa tu!

AJIFUNZE NA YOTOKANAYO!
 
mbwa wenyewe wanapewa viroba wanalewa, au wanadondosha mafuta ya simba mbwa wanajificha wenyewe wanabaki kulia lia, je saa sita utawaachia mbwa wako?
 
Kumbe nia ilikuwa kusuta.....sasa mwenyewe yumo humu apate huu ujumbe au umendika kufurahisha moyo wako?
 
una tabia kama hii nini, nimetoa habari ya ukweli na yanayofanyika ni ya ukweli, hupo hapooo

ndiyo ninayo,lakini kwangu kunalindwa na mitambo maalum na mbwa wakali!!tatizo nyie majirani mlikuwa mnamuombea jamaa njaa ili mpate cha kuongea
 
Kwa kifupi hao waliokuja na defender sio majambazi bali ni mapolisi wanaofanya ujambazi! Wewe wa wapi kama watu wanaweza kutumia bomu,risasi kumuangamiza mtu, ndo washindwe kuja na defender sasa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom