Ujambazi daraja la mlalakuwa, dar

ExpertBroker

JF-Expert Member
Jun 1, 2009
454
107


Wadau, hii ni copy and paste kutoka kwa michuzi! Nimeona si mbaya tukipeana habari hii!

Nawasilisha!!


JUZI MAJIRA YA SAA SABA USIKU RAFIKI YANGU ALIKUA ANA RUDI NYUMBANI KWAKE KUPITIA NJIA YA KAWE CHINI. BAADA YA KUVUKA KIDOGO DARAJA LA KAWE (MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA) GHAFLA AKAKUTANA NA MAGOGO YAMEPANGWA BARABARANI KUZIBA NJIA NA ALIPOJARIBU KUPUNGUZA MWENDO ALIWAONA WATU WAKIJA TOKA NYUMA YAKE WAKIIBUKIA VICHAKANI, UAMUZI ALIOUCHUKUA NI KUPARAMIA YALE MAGOGO UKIZINGATIA GARI YAKE SIO KUBWA YALIHARIBU MIGGU YOTE YA MBELE NA BAMBER LAKINI ALIKIMBIZA HADI POLISI KAWE NDIPO ALIPOJIHISI YUPO SALAMA LAKINI GARI MBELE KOTE HAIFAI

CHA KUJIULIZA, HII SIO MARA YA KWANZA KWA UJAMBAZI HUO KUTOKEA MAENEO YALE NA KUNA KIPINDI KULIKUA NA ULINZI WA PAMOJA KATIKA ULTIMATE SECURITY , POLISI NA JKT LAKINI NADHANI ULINZI HUO HAUPO TENA

NAWASHAURI WAKAZI WANAOTUMIA NJIA HIYO NI BORA UZUNGUKE LUGALO NI SALAMA ZAIDI KULIKONI NJIA HIYO HASA WAKATI WA USIKU MKUBWA. NASIKITIKA KWAMBA VITENDO HIVYO VINAFANYIKA MITA CHACHE TOKA MAKAO MAKUU YA JKT???

MDAU, KAWE
 
Du!, sipati picha, japo taarifa yako imesema daraja la Mlalakuwa, hii haiwezekani kwa sababu daraja linalindwa na JKT 24/7, ila eneo la hatari lazima litakuwa pale mbele baada kona ya Msasani beach, ila ujumbe umefika.

Bahati nzuri pia kilichowekwa itakuwa sio magogo, bali ni vigogo tuu, maana kama ni magogo kweli, 4-Wheel haiwezi kupanda, itakuwa Saloon?.

Nadhani hawa watakuwa ni vibaka tuu wa Kawe wakitafuta hela ya gongo na bangi, ila ni angalizo muhimu. Asante.
 
Kambi za jeshi ni maeneo hatari.
magari yanayotekwa Ruvu na Ngerengere inasadikiwa kuwa yanatekwa na wanajeshi wetu.
Je kwanini tusiamini kuwa wahalifu wa Mlalakuwa ni wanajeshi?
 
Back
Top Bottom