UJambazi Banki ya Biashara ya Africa (CBA)

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Muda mfupi uliopita katika redio Wapo nimesikia ujambazi uliotokea "Commercial Bank of Africa" tawi la Nyerere RD-Jamana House. Majambazi 6 yalitumia vitambulisho vya benki hiyo na kutumia muda wa saa 2-3 na kufanikiwa kuchukuwa mamilioni ya fedha za Ki-Tz bila kutumia silaha. Kamanda Kova akihojiwa amesema wamewakamata watumishi 2 na mlinzi 1 wa Security Grp. Pia ameeleza kuanza kwa upelelezi mkali kwa kutumia Ma-CID kutoka Makao Makuu na Kanda Maalum.

Hakuna madhara mengine ambayo yamesababishwa na uvamizi wa majambazi hayo.

Mwenye taarifa zaidi wadau kwa hapo Dar...
 
Ujinga tu,taarifa zimerushwa redioni wakati majambazi wapo ndani,hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa wakati,
 
Hao sio majambazi, bali ni wasanii wa levo nyingine. Ambao ofcoz huko mtaani watamwagiwa sifa kibao kuwa wao ni wajanja.
 
Back
Top Bottom