Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,505
- 41,011
Katika vipindi mbalimbali nchini mwetu Tanzania, tumeshuhudia vurugu na fujo zenye mwelekeo wa kidini. Kuanzia zile za uvunjaji wa bucha za nguruwe (Tanzania Bara), uchomaji wa baa (Zanzibar), uchomaji wa makanisa (Zanzibar) na uchomaji wa nyumba za kuishi na biashara (Zanzibar). Na hivi sasa uchomaji wa makanisa na vitisho kwa watu wa bara waishio Zanzibar. Japo ndani yake kunaonekana ni chuki dhidi ya watu wa bara lakini ukweli ni kuwa kuna sehemu kubwa ambayo ni chuki dhidi ya Ukristo.
Watu wengi, ikiwemo watu wa kawaida na viongozi, hasa wale walio wakristo, wamekuwa waangalifu sana wa kuchagua maneno katika kuongelea mambo haya, na hasa isije ikaonekana kuwa kwa kuwa wao ni wakristo labda kwa kauli zao wanaubeza au kuudharau uislam.
Kwangu mimi, nadhani ni muhimu sana kwa Waislam wa Tanzania na Dunia nzima, kujiondoa katika kutazamwa kuwa dini yao inapenda kupalilia vurugu au mafundisho yake hayana mkazo wa dhati juu ya kuheshimu haki za watu wengine. Wasio waislam wana maswali mengi juu ya dhamira ya kweli ya Uislam kuyakubali makundi mengine yenye imani tofauti na Uislam kuishi kama jamii moja katika mazingira ya aina moja.
Waislam ni wengi sana Duniani, na kama kila Muislam angekuwa ni mtu wa vurugu basi Dunia isingeweza kukalika. Lakini hao wachache wenye kupenda fujo, mapigano na mauuaji wanaashiria upungufu fulani katika mafundisho ya uislam, maana hao wauaji wote na wapenda vurugu, kwa wakati fulani wamepitia kwenye mafundisho ya dini ya Kiislam, na hata wakati wanapofanya mauaji na mapigano hudai kuwa wanatimiza mafundisho ya Dini ya Kiislam. Huko kwenye mafundisho ya Uislam wanafundishwa nini mpaka wawe watu hayawani kabisa wa kufurahia mauaji au mapigano.
Viongozi wengi Duniani, wanapoongea mbele ya watu hueleza kuwa wanapigana na makundi ya kigaidi na siyo uislam lakini ukweli ni kuwa zaidi ya 90% ya makundi hayo ya kigaidi, wafuasi na viongozi wake ni waislam. Hiyo pekee yake ilitosha kuufanya uongozi wa dini ya Kiislam, kukaa na kujiuliza na kutafakari, kwa nini iwe hivyo, maana kwa vyovyote ni lazima kuna walakini wa mafundisho yanayosisitiza upendo na uvumilivu baina ya binadamu. Hata hapa kwetu, wakati kuna makanisa yamechomwa lakini sijawahi kusikia msikiti umechomwa moto; wakati nimesikia bucha za nguruwe, bar na nyumba za wakristo zikichomwa na Waislam lakini sijawahi kusikia biashara au makazi ya waislam yameshambuliwa na wakristo. Ninaamini utulivu wa nchi yetu umetokana na uvumilivu wa Wakristo, lakini kama na Wakristo wangetaka kulipiza kisasi, hakika Tanzania isingekuwepo.
Hapa kwetu tuna bahati kubwa, Rais wetu ni Muislam, Makamu wa Rais ni Muislam, Jaji Mkuu ni Muislam, Mkuu wa Jeshi la Polisi ni Muislam, Afisa Tawala Mkuu wa JWTZ ni muislam, hivi hawa wote wanajisikiaje katika nafasi zao hizo wanaposhuhudia kunakuwa na vurugu zinazohusishwa na imani yao? Kwa kuwa ni imani yao, nina imani kuwa walikuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kudhibiti na kuwakanya viongozi wa dini yao wanaopandikiza na kushabikia vurugu, kama wangekuwa na dhamira. Kwa kiongozi yeyote mwenye hekima, ni aibu kubwa hata kwako binafsi kama kundi mojawapo ambalo wewe umo linatenda kinyume cha sheria na hekima.
Naheshimu sana utendaji wa Yusuph Makamba alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam juu ya uovu unaosima katika fikra za kidini, hakuwa na simile kwa waleta vurugu wowote wanaosimama nyuma ya kivuli cha uislam. Na kwa maneno yake aliwahi kusema, 'Yeyote anayefanya fujo akikimbilia msikitini tutamfuata na kumtoa, uislam unaujua wewe tu?'. Lakini hawa wa sasa katika maneno wanalaani udini lakini katika matendo wanapalilia.
Sikutaka kuongea kwa kufurahisha nafsi ya mtu yeyote bali yale ninayoamini. Ninaamini huu ni wakati sahihi kwa waislam wote nchini wanaopenda amani (ambao ni wengi), kusimama na kulaani uchafu unaofanywa na makundi ya kidini Zanzibar, na ndani ya taasisi za kuislam lazima uwepo uwezo na taratibu za kuwadhibiti watu hawa maana kwa matendo yao wanaudhalilisha uislam na Waislam, hata ifike mahali iaminike kuwa mafundisho ya dini ya kiislam yanalea na kupalilia fujo na mauaji. Kikwete, Sheni, Mwema, Zito, n.k. mko wapi? Mbona watu wanafanya ouvu nyuma ya imani yenu bila sisi wengine kuona kama kuna jitihada za wazi za kudhibiti hali hiyo. Ninyi mna bahati mnaufahamu uislam na mnafahamu sheria za nchi yetu na sheria za kimatifa, mna uwezo wa kujadiliana na wenzenu katika imani yenu na mna nafasi za Kitaifa katika jamii yetu lakini mbona hatuoni uwezo wenu? Au hata ninyi hamna uwezo juu hao waovu wanaosimama nyuma ya imani yenu?