Uhusika wa Rais Kikwete katika utapeli wa Richmond...kwa mujibu wa Lowassa ?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,244
HATIMAYE Edward Lowassa ametoka hadharani na kuonyesha kuwa anataka kupimana ubavu na Rais Jakaya Kikwete.

Ameeleza hadharani kuwa Rais Kikwete anahusika kwenye mkataba tata wa Richmond/Dowans; lakini pia, kuwa hafuati taratibu katika kuongoza chama chake.

Lowassa ambaye alikuwa nguzo muhimu katika mbio za urais wa Kikwete mwaka 2005, ameonekana kumgeuka waziwazi swahiba wake huyo kwa kuanika kile wachunguzi wanaita “udhaifu katika uongozi.”

Ndani ya kipindi cha siku nne, Lowassa ametoa kauli tatu nzito zinazoonyesha dhahiri ameamua kufanya mapambano na Kikwete.

Akiwa ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lowassa alinukuliwa akieleza hatua kwa hatua namna kampuni ya kitapeli ya Richmond Development Company (RDC), ilivyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura nchini.

Lowassa alijiuzulu wadhifa wa waziri mkuu mwaka 2008 kufuatia kashfa ya mkataba wa Richmond, kampuni iliyopewa kwa upendeleo zabuni ya kuzalisha umeme wakati haina fedha, haina uzoefu wala fedha za kufanyia kazi hiyo.

Alikiambia kikao cha NEC mjini Dodoma, “Hakuna jambo nililolifanya ambalo wewe Rais Kikwete hukulifahamu au hukunituma” kuhusu Richmond/Dowans.

Alisema, “…Mwenyekiti, natukanwa kwa ufisadi wa Richmond wakati wewe unafahamu yalichosababisha kashfa ya Richmond ni makosa ya watendaji walio chini yangu? Sasa kosa langu ni lipi? Ni kule kukubali kuwajibika kwa ajili ya serikali yangu na chama chetu? Kwa nini nihukumiwe kwa kosa hilo?”

Huku akimtolea macho Kikwete alisema, “Unakumbuka vema jinsi nilivyotaka kuvunja mkataba ule. Nilikupigia simu ukiwa nje ya nchi, lakini ukasema umepata ushauri wa kamati ya makatibu wakuu, ushauri ambao ulisababisha mkataba usivunjwe?”

Lowassa alisema Kikwete anafahamu kila kitu kwa kuwa ni yeye aliyeridhia Rostam Aziz kutafuta mbia baada ya Richmond kushindwa kuleta umeme.

“Uliponitaka ushauri wa mtu wa kutusaidia ili kuondokana na aibu ya Richmond kushindwa kutimiza mkataba wake, nilipokutajia jina la Rostam, haraka ulikubali na kusema, naona hilo ni sawa,” alieleza Lowassa kwa njia ya kumsuta Kikwete.

Hatua ya Lowassa kumuingiza Kikwete kwenye tope la Richmond/Dowans imezima moja kwa moja kauli yake iliyodai, “Siwajui wala siwafahamu wamiliki wa makampuni ya Dowans Tanzania Ltd na Dowans Holdings SA.”

Akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, tarehe 5 Februari 2011, mjini Dodoma, Kikwete alikana kufahamu wamiliki wa kampuni hiyo na kwamba hajawahi kuwaona wamiliki wake.

Alisema, “Nataka kuuhakikishia umma kwamba, sihusiki na kampuni hii. Siifahamu na wala sijawahi kuwaona wamiliki wake…Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi.”

Kauli ya Kikwete ya kutoitambua Dowans wala wamiliki wake, ilikuwa ni mwendelezo wa kauli kama hizo zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wasaidizi wake, zikilenga kumuondoa kwenye kashfa hiyo iliyomlazimu kuvunja baraza lake la mawaziri.

Akizungumzia kwa undani jinsi Richmond ilivyoingia na jinsi yeye na Kikwete walivyokuwa kitu kimoja kuhakikisha mkataba unasainiwa na kutekelezwa, Lowassa alisema, “Hakuna jambo nililolifanya ambalo Rais Kikwete hukulifahamu.”

Akizungumzia kwa undani suala hilo kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu wadhifa wa waziri mkuu, Februari 2008, Lowassa alisema, “Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama, hivi hatukujua kama kuna kamati hizo za maadili?”

Lowassa alikuwa akichangia pendekezo la Kamati Kuu (CC) ya CCM lililotaka kurejeshwa kwa suala la “kujivua gamba” kwenye vikao vya chini vya chama hicho baada ya watuhumiwa, isipokuwa Rostam Aziz, kukataa kuachia uongozi katika chama.

Kikwete alikiambia kikao cha NEC kuwa, uamuzi wa kutaka jambo hilo lirejeshwe kwenye vikao vya chini, umetokana na “taratibu kukosewa.”

Hata hivyo, kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho aliliambia gazeti hili juzi Jumatatu, uamuzi wa Kikwete kulirejesha suala la kujivua gamba kwenye vikao vya chini ulitokana na hofu ya NEC kujaa wajumbe wengi kutoka kwa kundi la Lowassa.

“Unajua mle NEC, Kikwete hana chake. Mle ndani kuna kundi kubwa la Lowassa, ndiyo maana jamaa ameogopa suala hilo la kuvuana magamba lijadiliwe,” ameeleza kiongozi huyo ambaye ni waziri katika serikali ya Rais Kikwete.

Kanuni za CCM zinaeleza kabla ya tuhuma kufikishwa NEC, sharti wale wanaotuhumiwa wapewe haki na fursa ya kujitetea mbele ya vikao vya kamati ya usalama na maadili.

Akifunga mjadala huo kwa angalizo mwanana, Kikwete aliagiza suala hilo lipelekwe kamati ya maadili ambako alitaka kuwasilishwa ushahidi wa vielelezo na siyo hujuma dhidi ya watuhumiwa.

Wakati Lowassa akishusha tuhuma kwa Kikwete, kiongozi huyo wa nchi alionekana kama amepigwa ngazi. Hakukana hata tuhuma moja miongoni mwa yaliyoelezwa na swahiba wake huyo wa zamani.

Kikwete na Lowassa, wamejitambulisha mara kadhaa kuwa ni marafiki, huku mmoja akisisitiza, “Hatukutana barabarani.”

Haijafahamika mahusiano yao yamefikia wapi kwa sasa baada ya Lowassa kumhusisha mwenzake katika kashfa ya Richmond katika kile wachunguzi wanasema amechukua tabia ya “tufe sote au tukose wote.”

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kauli ya Lowassa ambayo ilitolewa mbele ya viongozi wake wakuu, akiwamo rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ililenga kuonyesha udhaifu wa Kikwete ndani ya CCM kwa kuasisi falsafa ya kujivua gamba na kuikimbiza moja kwa moja kwenye CC na NEC, kinyume cha taratibu na kanuni za chama chake.

Kama hiyo haitoshi, juzi Jumapili akiwa mkoani Singida alikokwenda kusimamia harambaee ya kuchangia fedha za ujenzi wa kanisa, Lowassa alinukuliwa akisema, “Kwa vyovyote vile, nitaibuka mshindi dhidi ya vita vya kuvuana magamba.”

Akitiwa moyo na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kati, Ushirika wa Amani, mjini Singida, Eliufoo Sima aliyesema, “suluhu ya mapambano ni kukabiliana nayo,” mwanasiasa huyo alisema, amekuwa akihusishwa na tuhuma ambazo hazina ukweli.

Askofu Sima alisema mapambano katika maisha hayatakwisha na “suluhisho siyo kuyaogopa, isipokuwa kuyatafutia majawabu kwa upole, hekima na utulivu.”

Vita vya magamba viliasisiwa na Kikwete 5 Februari 2011, kabla ya kudakwa na baadhi ya watendaji wa Sekretarieti ya CC ambao kwa miezi saba sasa, wamekuwa wakituhumu Lowassa na wenzake wawili - Rostam Aziz na Andrew Chenge – kuwa mafisadi wanaokidhalilisha chama mbele ya jamii.

Wakati hayo yakiendelea, taarifa kutoka ndani ya CC zinasema kushindwa kwa Rais Kikwete kutekeleza mkakati wake wa kumfukuza Lowassa ndani ya chama chake, kulitokana na upinzani mkali uliotokea kwenye mkutano wa CC.

“Ni kweli kabisa, ndani ya CC, Lowassa alipata uungwaji mkono mkubwa, kiasi ambacho mwenyekiti alilazimika kulipeleka suala hilo NEC. Alipofika NEC na kuona moto umekuwa mkubwa, ndipo alipoamua kuliondoa na kutaka lifanyiwe kazi kwenye vyombo vya chini,” kimeeleza chanzo kimoja cha gazeti hili.

Amesema wajumnbe wa Zanzibar, wakiongozwa na makamu mwenyekiti wa chama hicho visiwani, Amani Abeid Karume, muda wote wa mkutano walisimama imara kuhakikisha Lowassa hafukuzwi kwenye chama.

“Kuna wakati watu kutoka Bara walikuwa wanakaribia kushinda. Lakini baadaye Zanzibar wakapata nguvu pale Karume aliposimama na kusema, shutuma zote hizo hazijafuata taratibu,” ameeleza.
 
LOWASSA ameshatamka kuwa wanaotuhumiwa wote wajiuzuru kama alivyofanya yeye
haya KIKWETE changamkia tenda hiyo ya kujiuzuru
wewe ni GAMBA mkubwa
 
Historia inamuhukumu vibaya huyu mheshimiwa! Tafuteni omo na jik za kutosha
 
Ukweli huwa haufichiki, usipoonekana leo basi huonekana kesho! JK ni tatizo kwa uchumi wa Tanzania,.
Hana uwelewa, hana element hata moja ya uongozi, ni mchumia tumbo anae kubali kila ushauri asiyejua kuchanganua au kujihangaisha hata kidogo kujua yanayojiri!
Anautaalamu wa ku sign tuu
 
Jamaa muuza sura tu,hupenda kuhudhuria vitafrija na matukio mengne madogomadogo,rais mzma anadai hajui kwa nin Tanzania ni maskini!fyoooooooooo
 
Huu urais wa kutafutwa kwa namna hii akiupata kama taifa tutaulipia gharama kubwa sana....kama ambavyo sasa hivi tunalipa kwa makosa tuliyofanya 2005 na baadae 2010!
 
Kweli nachoka sana na ccm, ivi nyie mnaojitapa kuwa wanachama wa ccm, haya matapishi yanayonuka yaliyomakini kuwaongoza hamuhisi ata kichefu chefu?? Au na nyie ni matapishi pia?? Tangu mwenyekiti wa ccm ni muhujumu uchumi kupitia dowans nk, makamu mwenyekiti msekwa muhujumu kupitia wanyama pori, hamuyaoni aya?? Au ndo njaa zanawaweka uko na hamna alternatives?? Ata lowasa umaarufu anaoupata ni kutokana na ela alizoiba serikalini na sasa anazitumia kwa wenye njaa, nawaapieni tukichukua dola cdm hawa viongozi wenu mafisadi tunawapeleka mahakamani na lazima wafungwe, na mtajuta kuwapa nafasi wezi na majambazi kuwaongoza. Mnatuhudhi sana watanzania tunaodhurumiwa rasilimali zetu
 
Huu urais wa kutafutwa kwa namna hii akiupata kama taifa tutaulipia gharama kubwa sana....kama ambavyo sasa hivi tunalipa kwa makosa tuliyofanya 2005 na baadae 2010!
Hawa watu kwa ujulimla hawafai hata kuitwa watnzania tu, hawafai kuongoza hata nyumba kumi tu! Hawa mahali salama kwao ni ahera huko watastarehe na kupata vyeo vyovyote wavitakavyo!

Pambafuuuu zao!
 
Bado nasikitika, hawa wazanzibar njaa inawasumbua sana, ivi wanamjua vizuri lowasa na kuamua kumuunga mkono?? Hapana yawezekana aliwaongezea posho za kikao pia pocket money si ivi ivi!!! Hii njaa itatupeleka pabaya, lowasa ni fisadi hachomoki katika ili uyu, asitambe kuwa alijiuzulu kishujaa, uyu alijiuzulu kwa kashfa za wizi na uhujumu wa uchumi ilo ni doa na washirika wake wajue ni washirika wa mwizi pia muhujumu wa uchumi wala hawatapata la maana kwake wanalolifuta zaidi watanzania tunawachukulia na wao kuwa wasaliti wakubwa
 
Hivi kuwa Rais kuna maslahi gani ya ajabu? mbona unatafutwa kwa gharama kubwa hivi? Lowassa anatafuta urais hivyo ili atufanyie nini? kikwete alifanya hivyohivyo tunaona kinachoendelea. watu wa namna hiyo wasipewe nafasi.
 
Hivi kuwa Rais kuna maslahi gani ya ajabu? mbona unatafutwa kwa gharama kubwa hivi? Lowassa anatafuta urais hivyo ili atufanyie nini? kikwete alifanya hivyohivyo tunaona kinachoendelea. watu wa namna hiyo wasipewe nafasi.

Sasa wewe unataka nani awe rais!
 
Ngeleja alitumia mkutano huo kuwataja wamiliki wa Dowans baada ya kupata taarifa kutoka Brela kwa barua yenye kumb. namba MITM/RC/58550/22 ya Januari 5, mwaka huu ambao ni Dowans Holdings S.A, yenye hisa 81 ya Costa Rica na Portek System and Equipment PTE Limited hisa 54 ya Singapore.

Alisema wakurugenzi wa Dowans wa hapa nchini ni Andrew James Tice (Canadian), Gopalakrishnan Balachandran (Indian), Hon Sung Woo (Singapore), Guy Arthur Picard (Canadian), Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi (Oman),Jakaya Kikwete (Tanzania )na Stanley Munai (Kenyan).

 
Tafakuri Yangu Ya Leo: Ya Kakobe na TANESCO mwogopeni Mungu tujaribu kwa Mafisadi




KAMA kuna jambo linalowakera watanzania basi ni hili la Ufisadi miongoni mwa baadhi ya viongozi wetu. Watanzania wanajiuliza, iweje wao waendelee kuwa masikini ilihali wachache wanazidi kuneemeka huku wakikodi ndege kwenda kutumbuliwa vipele huko Berlin Ujerumani? Sasa mimi nina pendekezo binafsi mkiona linafaa tulifanyie kazi wadau.

Hivi mnakumbuka enzi zile za mgogoro kati ya Askofu Zakaria Kakobe na TANESCO? , Kakobe aliendesha harakati zisizo na umwagaji damu akazipachika jina la "TANESCO Mwogopeni Mungu !!" na fulana za njano alichapa tunazikumbuka, Sasa kwa nini na sisi tusitumie mbinu hii kuwashughulikia Mafisadi?

Na hii iwe Tafakuri yangu ya leo jamani……

Nova Kambota Mwanaharakati
"Kitendawili sio deni ukishindwa nipe mji"
0717-709618 au 0766-730256
novakambota@gmail.com
novadream.blog.com
10 Machi 2011
Njombe , Tanzania.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom