Uhusiano wa ajira za ualimu Vyuo Vikuu, TCU na GPA za SUA

matunge

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
442
426
Wanajamii !!
1. Naomba msaada wenu kuhusu namna GPA za SUA zinavyopatikana. Kwa uwezo wangu mdogo wa hesabu nimekuja kugundua kuwa ukokotoaji wa GPA katika SUA uko tofauti kabisa na vyuo vikuu vingine hapa nchini. Kwani hutumia mfumo wa raw marks:
GPA calculation as per SUA is:

Y= 0.024X + 2.6 for (A; 75-100 marks; 4.4 to 5.0 GPA): Y=0.08X - 1.6 for (B+;70-74.9 marks; 4.0 to 4.39 GPA): Y=0.1X-3 for (B;60-69.9 marks; 3.0 to 3.99 GPA): Y=0.1X-3 for (C; 50-59.9 marks; 2.0 to 2.99 GPA): Y=0.1X-3 for (D; 40-49.9 marks; 1.0 to 1.99 GPA) and Y=0.025X for (E; 0-39.9 marks; 0.0 to 0.99 GPA).

All ranging from Excellent, Very Good, Good, Satisfactory, Marginal Fail and Absolute Fail respectively. Where: Y= Grade point and X=Raw marks (%).

Wakati vyuo vingine kwa mfano A ni A tu hata kama ni 100 ama 80, wote hawa wako katika kundi moja. Hivyo basi ukichukua matokeo ya mwanafunzi wa SUA na kukokotoa kwa mifumo hii miwili unapata GPA tofauti kabisa, yaani wa vyuo vingine mfano UDSM atapata GPA kubwa zaidi. Jamani TCU sijui wanalijua hili, maana limekuwa likiwaathiri wanafunzi wengi wa SUA katika soko la ajira hasa ya kufundisha vyuo vikuu na taasisi za utafiti maana huhitaji GPA zaidi ya 3.8, jamani naomba kuwasilisha kama kuna mtu anaweza kufafanua vizuri itatusaidia sana.

2. Kuhusu ajira za ualimu kwa Tutorial Assistants kuwataka kuwa na GPA ya kuanzia 3.8 ni kuwanyima fursa wale wote wenye 3.5 na kuendelea ili hali nao pia wapo katika kundi la pili la ufaulu, na wana uwezo mkubwa wa kufundisha.

Ninawafahamu rafiki zangu wengi tu ambao wana GPA 3.5 lakini uwezo wao hauna mfano hata hao wenye GPA za juu hawawafikii. Nawaomba TCU waliangalie hili, maana si kila wakati GPA kubwa ndo inatoa picha ya candidate bora.

Ukichunguza sana vyuo vingi bora barani afrika hata ulaya wanataka tu first class ama upper second, ije hapa tanzania ambapo kuna GPA nyingi tu kubwa wamepewa wanafunzi isivyo halali nawasilisha
 
Nimemaliza SUA mwaka huu na hiyo system ya GPA wana argue kwamba watu hawawezi kufanana mpaka useme A ni A bila kuangalia raw marks! So hapo ndio panapotubana lakini pia ukikutana na watu wanaojua system ya GPA za SUA katika swala la kazi hauna tabu kuchukuliwa koz unaeza ukawa na 3.5 ya SUA na mwingine ana 4.0 ya mzumbe lakini kindani we wa 3.5 ya SUA uko juu zaidi!!
Dats wat av experienced in my tym at SUA
 
Sifa ya kufundisha chuo kikuu inayotambulika na TCU ni 3.5 and above na si 3.8 kama wadau wanavyodai kwa hiyo mwenye GPA hiyo anaweza pata kazi chuo kikuu ya kufundisha but tunapokuja kwenye competition ndiyo unaweza kukuta hawakuchukui kwa vile wapo watu wenye first class.Lakini kuna vyuo ambavyo wamejiwekea utaratibu wao wa kuchukua GPA ya 3.8 kama UDSM,SUA,OPEN na baadhi ya private.Sasa hapo unaweza kukuta mtu una first class mwenzio ana 3.5 mkaomba kazi wakati mmoja wewe ukaachwa 3.5 akachukuliwa usiulize kwa nini maana nae ana sifa hamna atakayewauliza (TANZANIA YETU).Nawashauri wale wote wenye GPA 3.5 kama wana uwezo wapige masters hasa Sayansi opportunities zipo kibao first degree zina compettion sana na vyuo vimekuwa vingi vinavyotoa degree.Na si lazima ufundishe chuo kikuu tu kuna vyuo ambavyo vipo chini ya NACTE navyo mishahara ni ileile kama ya vyuo vikuu vyuo hivyo ni kama DIT,Arusha tech,Veta,vyuo vya ardhi kama Morogoro,Tabora na vinginevyo.Kwa hiyo kama una GPA hiyo ya 3.5 bado una nafasi ya kufikia ndoto yako.Nawasilisha.
 
Nimemaliza SUA mwaka huu na hiyo system ya GPA wana argue kwamba watu hawawezi kufanana mpaka useme A ni A bila kuangalia raw marks! So hapo ndio panapotubana lakini pia ukikutana na watu wanaojua system ya GPA za SUA katika swala la kazi hauna tabu kuchukuliwa koz unaeza ukawa na 3.5 ya SUA na mwingine ana 4.0 ya mzumbe lakini kindani we wa 3.5 ya SUA uko juu zaidi!!
Dats wat av experienced in my tym at SUA

mkuu unajua GPA za Mzumbe Universty zinavyokuwa calculated?pia naomba kujua kozi zinazotolewa Mzumbe ambazo na SUA wanatoa,otherwise nadiriki kusema umekurupuka kupost au SUA wamewafundisha kuongea bila kufanya research.
 
Tatizo let watanzania ni kulalamikia kila jambo pasi kuchukua hatua! Kila chuo kina maamuzi yake when it comes to academics, na chombo kikubwa kabisa kinachamua mifumo ya academics katika respective colleges ni senete ambayo wanafunzi wana uwakilishi. Kama kuna mapungufu yeyote na tuna hoja za msingi kabisa, kwa nini tusitumie vyombo hivi? Nimepata bahati ya kuwa mwakilishi wa wanafunzi huko nyuma nikiwa chuo na mambo kama haya yanajadilika na yanaweza kupata ufumbuzi. Suala la kudai vyuo visiangalie GPA vinapotafuta walimu ni jambo lisilowezekana kwani ndo kipimo pekee cha kisayansi kinachoweza kutofautisha uwezo wa watu ingawa pia ni kweli wenye uwezo mkubwa zaidi wanaweza kwa sababu hii na ile wasipate alama za juu zaidi ya wengine. Jambo jingine, tunapaswa kua na malengo. Kama unataka kufundisha na unajua wanahitaji high grades, go for it, get the 1st class! yeah, why not.
 
Hakuna anayelalamika kaka nimeweka mada hii kwa ajili ya kupata maoni tu.
 
mkuu unajua GPA za Mzumbe Universty zinavyokuwa calculated?pia naomba kujua kozi zinazotolewa Mzumbe ambazo na SUA wanatoa,otherwise nadiriki kusema umekurupuka kupost au SUA wamewafundisha kuongea bila kufanya research.

Mkuu utakuwa umesoma Mzumbe na unahisi umedharauliwa.Mdau katoa mfano tu hakuwa na maana ya kuattack Mzumbe na kaeleza wazi jinsi GPA calculation ya SUA inavyotofautiana na Institutions nyingine including hiyo Mzumbe yako.Inferiority complex inatutesa sana watanzania.Soma posts zote vizuri kama kuna walakini weka post ya kile unachofikiri kipo sahihi.Note,yule mleta mada katolea mfano UDSM watu wakaenda moja kwa moja kwenye hoja ya msingi siyo kumshambulia kwa nini kataja UDSM...jiamini mkuu
 
hahaha,mkuu tusaidie calculation ya GPA ya mzumbe
 
Ushindani wa ajira ndyo zinafanya hizo GPA kubadilika,maximum 3.5,so kujiweka sehemu nzuri katka ajira pata above it.
 
Duh kumbe GPA deal wakuu.Kwanini vyuo vya Tz sanasana public universities hawadahili watu wenye lower second kama 3.4,3.3 etc lakini vyuo kama Makerere,Nairobi,Kenyatta wanapokea watu hao?
 
Gpa ya mzumbe wanatumia the same formula wanayotumia SUA, aliileta DVC ACADEMIC mwaka 2007 baada ya kuamia mzumbe kutoka SUA i mean
mchango wa A ya 80 na A ya 90 ni tofauti kwenye GPA, mfano mtu akipata C ya 50 is equal to 2.0 GPA while akipata C ya 59 is equal to 2.9 GPA
kwa hiyo wakuu hata kama hamuipendi mzumbe but msidanganye kuhusu mzumbe, i was there for BAF from 2007-2010 and now i enjoy MU fruits at KPMG,,, there is no place like home go go Mzumbe japokuwa haters wana chuki na wewe
 
Mi nadhani pamoja na mawazo na maoni ya hapo juu,pia ubora wa chuo unatofautiana.Halafu wakubwa mbona Mzmbe now days siisikii kabisa nini shida,Marketing au? Ninapozungumzia ubora namaanisha field,Laboratories na Competent lecturers ktk muktadha wa PROFESSIONALISM!
 
Your name says it all,hope hapo kpmg huendelezi hako kamchezo
Gpa ya mzumbe wanatumia the same formula wanayotumia SUA, aliileta DVC ACADEMIC mwaka 2007 baada ya kuamia mzumbe kutoka SUA i mean
mchango wa A ya 80 na A ya 90 ni tofauti kwenye GPA, mfano mtu akipata C ya 50 is equal to 2.0 GPA while akipata C ya 59 is equal to 2.9 GPA
kwa hiyo wakuu hata kama hamuipendi mzumbe but msidanganye kuhusu mzumbe, i was there for BAF from 2007-2010 and now i enjoy MU fruits at KPMG,,, there is no place like home go go Mzumbe japokuwa haters wana chuki na wewe
 
Mkuu utakuwa umesoma Mzumbe na unahisi umedharauliwa.Mdau katoa mfano tu hakuwa na maana ya kuattack Mzumbe na kaeleza wazi jinsi GPA calculation ya SUA inavyotofautiana na Institutions nyingine including hiyo Mzumbe yako.Inferiority complex inatutesa sana watanzania.Soma posts zote vizuri kama kuna walakini weka post ya kile unachofikiri kipo sahihi.Note,yule mleta mada katolea mfano UDSM watu wakaenda moja kwa moja kwenye hoja ya msingi siyo kumshambulia kwa nini kataja UDSM...jiamini mkuu

kumbe mkuu na wewe unaongea bila kufanya research, na siamini kama SUA mmefundishwa hivyo!nilichotaka kukuonesha ni kwamba calculation ya GPA inayotumika SUA na Mzumbe Chuo Kikuu ni hiyohiyo kwa kukusadia tafuta prospectus ya Mzumbe University(kama unaitaka nipm nikupe) hvyo basi mfano alioutoa hauendani na malengo ya muanzishaji thread kwa sababu GPA zote kwa SUA na Mzumbe zinafanana jinsi zinavyokuwa calculated.MIMI NA JIAMINI KWA SABABU NATIMIZA MSEMO WA NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK.Tukirudi kwenye mada nadhani hiyo sxstem inasaidia watu wasome na vilevile pindi unapopeleka gamba lako kama una 3.5 unaonekana upo makini.NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK,TUACHE MALUMBANO TUJENGE TANZANIA ILIYO IMARA. .
 
wewe kama umeenda chuoni na unataka first class dawa ni kusoma kwa bidiii bila kujali ni chuo gani. Lazima ufikie kiwango cha chuo ulichosajiliwa. sasa wewe kama umeenda SUA kujirusha tu shauri yakoSM , kwanini ukuapply huko tangu mwanzo. Wewe kama ulikuwa usomi shauri lako usituchanganye hapa. Ukilialia hapa hatuna msaada kwani majibu yapo kwenye cheti tayari. cha msingi songa mbele nayo tafuta kazi yoyote. Kwani maisha ni kuwa lecturer?? TAFAKARI
 
Gpa ya mzumbe wanatumia the same formula wanayotumia SUA, aliileta DVC ACADEMIC mwaka 2007 baada ya kuamia mzumbe kutoka SUA i mean
mchango wa A ya 80 na A ya 90 ni tofauti kwenye GPA, mfano mtu akipata C ya 50 is equal to 2.0 GPA while akipata C ya 59 is equal to 2.9 GPA
kwa hiyo wakuu hata kama hamuipendi mzumbe but msidanganye kuhusu mzumbe, i was there for BAF from 2007-2010 and now i enjoy MU fruits at KPMG,,, there is no place like home go go Mzumbe japokuwa haters wana chuki na wewe

Hivi kale kamchezo ka "KUKATA KIU" bado kanaendelea kule MU?
 
Back
Top Bottom