Uhusiano unapovunjika nani hasa mwenye hasara?

aaaaaaah kama mimi kwangu hakuna hata hasara nimekubwaga/umenibwaga najua soon replacement ipo na maisha yanaendelea
 
anayeumia ni yule aliyeinvest sana.kuweni makini hasa wanaume katika hili.
Wanawake wa sasa hawapendi kirahisi
 
Salaam wanajamvi. Kama kawaida yangu nikitingwa na jambo nakimbilia Great Thinkers!
Nimekuwa nikisoma malalamiko mengi humu jamvini kuhusu kuvunjika kwa mahusiano baina ya wapenzi au wanandowa. Nami nimekuwa nikijiuliza hivyo mwanamme analalamika nini iwapo mwanamke kwa hiari yake anaamuwa kuvunja uhusiano? Pengine mtizamo wangu sio sahihi hivyo naomba mawanzo ya jamvi kuhusu hili.Uhusiano unapovunjika nani hasa mwenye hasara zaidi?

Hasara ipo kwa wote, maana wote wameinvest muda wao na resource zao kwa muda mrefu na hivyo kuvunjika kwa mahusiano, ni lazima viwaguse wote. Ila kwa yule aliyependa zaidi na kunufaika zaidi na uhusiano huo, yeye ndiye atakeyesuffer zaidi kwa kipindi fulani mpaka moyo wake utakapokubali matokeo.
 
Binafsi ninaamini hakuna wa kumlaumu pindi mahusiano yanapovunjika...ila ingekuwa ni ndoa sawa!
Mahusiano siku zote ni daraja la kuelekea kwenye hatma ya wawili wapendanao.
Ni kama vile umepanda basi unaenda mkoa, katikati ya safari unagundua gari halina breki...hilo si ni jambo jema kuliko ingetokea ajali halafu mnagundua chanzo ni ukosefu wa breki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom