Uhusiano uliopo baina ya kukohoa na vinywaji baridi

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,829
1,296
Wadau,

Kuna hii knowledge ya kwamba ukiwa na kikohozi ama kikohozi na mafua vinasababishwa na mtu hasa kwa watoto kutumia vinywaji ama vimiminika baridi!

Na ikiwa wa mtoto anakohoa asitumie kabisa hivi vitu....................ni kweli ama ni elimu ya mitaani?

Naseama hivi nikiwa nafuatilia tatizo la mwanangu amekuwa akikoho kwa wiki ya tatu sasa na mara zote hospitali wamekuwa wakimwandikia syrup ya mucolyn mpaka nilipolalamiaka leo na wakambadilishia cifalexin (antibiotic)

Lakini nikawaambia kuwa tatizo kubwa kuwa nimeruhusu aendelee kutumia vitu kama juice nk vya baridi............kitu ambacho nachelea kukiamini
 
Kwa Mgonjwa wa kifua haswa watoto wadogo haifai kuwapa vinywaji vya baridi inachangia huo ubaridi asiweze kupona haraka hicho kifua chake. Nakuashauri kama una mtoto ana ugonjwa wa kifua usipe vinywaji baridi mpaka akimaliza kupona huo ndio ushauri wangu sijuwi kwa wenzangu wanaojuwa zaidi watupe maelezo yao zaidi.
 
ushauri mzuri - ila naongezea - hakikisha mtoto wako juice anazokunywa ni "fresh juice" - sio za makopo/chupa/boxes - zenye artificial flavours, food colouring etc. Pia atumie mafuta ya samaki (godliver oil) kwa muda mrefu -

Mpe pole mtoto wako
 
Back
Top Bottom