simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,409
- 9,183
Okay sawa Mzee! mamlaka unayo lakini kwenye hili swala la katiba busara lazima itawale.
Ninaendelea kuonesha makosa ya kimantiki na kifalsafa ya hotuba ya Rais Kikwete jana. Mojawapo ya mambo ambayo aliyadai akikanusha kuwa yeye si Dikteta ni kauli hii ambayo sidhani kama watu waliielewa uzito wake. Rais alidai kitu kingine ambacho nacho pia hana!
Rais amedai vitu ambavyo vinahitaji kukataliwa mara moja kwa sababu tukivukubali tu tunampa nguvu ambazo hana.
1. Rais ndiye anayetoa uhuru wa kutembea, vyombo vya habari na hata kuwa (the freedom to be)
2. Rais ndiye anayetoa uhuru kwa watu, vyama vya siasa tena "mkubwa mno"
3. Anaweza kuingilia kati uhuru huo kwa kuwa "dikteta" kidogo.
Ndugu zangu, Uhuru wa Watanzania hautoki kwa Rais - awe Kikwete au yeyote mwingine. Katiba yetu inasema hivi kuhusu uhuru wetu: (Ibara ya 12:1)
Maneno hayo yanaweza kuonekana ni shallow au hollow lakini ni makubwa sana. Yanatueleza kwamba kila Mtu (mimi, wewe, mtoto, mzee, kijana, msomi, mjinga, kichaa, mwenye akili sana, mlevi, mzinzi hata shoga!) huzaliwa 'HURU NA SAWA'! Kwa maneno mengine uhuru wetu hautokani na rais au chama cha siasa unatokana na kuzaliwa kwetu kama BINADAMU. Ndio maana tunasema "binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa".
Kwa hiyo, hoja ya kuwa uhuru wetu unatoka kwa rais au kwamba RAis anafikiria kuwa sisi tuko huru kwa sababu kaamua kutugea uhuru haina msingi, ni ya kukataliwa na kwa mara nyingine haina msingi wa Kikatiba (lacks constitutional basis whatoever).
NI kutoka katika kutambua kuwa sote tunazaliwa huru ndipo Katiba sasa inatambua uhuru huo na kuuhakikisha (the constitution recognizes and guarantee that freedom). Kumbe wananchi wanazaliwa wakiwa huru na kwa kutumia katiba yao wanajihakikishia uhuru huo - Rais hatoi wala kuhakikisha uhuru huo bali anasimamia kuwa uhuru huo hauondolewo - iwe na maadui wa ndani au wa nje - na hii ina maanisha hata na yeye mwenyewe!
Je ni uhuru gani tunazaliwa nao ambao hauwezi kuondolewa kiholela kama Rais alivyoashiria? Nitataja tu kama Katiba inavyoanisha sasa:
Uhuru wa kuwa hai (rais hawezi kuja na kumwambia polisi 'mpige huru risasi' halafu mtu akapigwa risasi kwa vile 'rais kasema'). Ili kuhakikisha hili Katiba imeweka wazi kuwa "itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake". Kwa maneno mengine ni kuwa kauli ya Rais anaweza kuwa dikteta kidogo na kuzuia uhuru wawatu haina msingi ni ya kuikataa kwani hana madaraka wala uwezo huo (nililisema hili siku ile aliposema Bungeni kuwa angeweza kuagiza Dr. Slaa akamatwe na akakamatwa)!
Uhuru wa mawazo na maoni - kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati. Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna mtu anayeweza kumlazimisha mtu mwingine kufikiri au kuwa na maoni anayoyataka yeye! Kiila mtu anahaki ya kufikiri na kujenga maoni ayapendayo yeye bila kulazimishwa. Hii ina maana kuwa uhuru huu hautoki kwa Rais. Rais hawezi kutuambia kuwa sote tunatakiwa kufikiria hivi au vile na tukifikiri tofauti basi ni makosa!
Uhuru wa imani - Katiba inatambua kuwa kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutoamini dini yoyote. Na katiba yetu inaenda mbali zaidi na kusema kuwa mtu anayo haki ya kubadilisha imani yake. Kwa maneno mengine mtoto aliyezaliwa katika familia ya kikristu akiamua kuwa Muislamu serikali au mtu yeyote hawezi kwenda na kumlazimisha abadili. Wanaweza kumshawishi au kumuonesha makosa lakini mwisho wa siku uamuzi ni wake. Na mtu akiamua kutoamini Mungu au akiamini minazi hakuna mtu wa kumlazimisha kuwa abadili imani! Rais hawezi kulazimisha watu waamini vyovyote apendavyo yeye.
Hiyo ni mifano michache tu. Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais kuwa yeye ndiye anatoa uhuru na kuwa anaweza kuuondoa uhuru huo wa kuwa "dikteta kidogo" haina msingi. Uhuru wetu hautoki kwa Rais. Period.
Ukisoma maneno yake hayo hapo juu yeye mwenyewe anaamini kuwa ni dikteta mkarimu (Benevolent dictator)... vinginevyo tusingekuwa huru hivi. Tumshukuru kwa kutupa uhuru wetu.
Tatizo la Kikwete ni mjinga.
Sasa wewe unaetaliwa na Kikwete tukuiteje? mjanja?
Aaaaaaghrrr!
We bb umekuja kwa usafırı ganı tena?
Kumbe mods wanahongeka ee!
Umewapa nn wakakutoa kıfungonı sı ulıkataa dhamana?!
haya ni MAWAZO ya MMM siyo maoni ya MMM. Kama ni maoni, tueleze nani anayapokea
Ooh ok, nimekupata. Kipengele gani cha Kaitba hii ili huu mjadala ufe kuwa ndivyo kinavyotaka mchakato uwe?
Udikteta tumeuacha zamani, wakati unarundikwa ndani bila hata kujuwa lini utatoka, mpaka apende Nyerere.
Udikteta tumeuacha wakati gazeti ni Daily news na la chama.
Hivi ni nani anaopinga kuwa zama za Udikteta tumeshaondokana nazo huko, chama kilikuwa kimoja, magazeti anayotaka nyerere tu. Radio anazotaka nyerere tu. TV hakuna. Jela unafungwa kwa amri tu ya Nyerere, au unapotezwa na hujulikani umeenda wapi? Nani asiojuwa kisa cha kuadhiriwa Hanga uwanjani na Nyerere na hajaonekana tena baada ya hapo> kama si udikteta ni nini ule?
Acha kulia lia mama.Tafadhali sana wacha kuchakachuwa jina langu kwenye post yako. Hayo uliyoyabandikia jina langu si maneno yangu naomba post # ngapi kama u mkweli.
Tafadhali moderators, mtu anafikia kuchakachuwa maneno ya watu na kubandika jina kwenye post ambayo si yangu na bado mnamuwachia. Nini hii? Tazameni huyu ntamaholo alivyochakachuwa post #103 na kuya "quote" hayo maandiko na kuyawekea jina langu. Tafadhali naomba haki itendeke.
Huu ni ukosefu wa ustaarabu wa hali ya juu na nnatumai moderators mtachukuwa hatua kali kwa watu kama hawa.
Huyu mzee hapa ndo kiboko yako tu!!
Huyu ndo alitawala bana..........alaaa!!Sasa wewe unaetawaliwa na Kikwete tukuiteje? mjanja?
I'm not being rude. You're just insignificant.Wanasheria wote waliomo JF basi nisimjuwe hata mmoja? unanchekesha!
Sasa wewe unaetawaliwa na Kikwete tukuiteje? mjanja?
Act No.15 of 1984, section 3.Ooh ok, nimekupata. Kipengele gani cha Kaitba hii ili huu mjadala ufe kuwa ndivyo kinavyotaka mchakato uwe?