Uhuru wetu hautoki kwa Kikwete au Rais yeyote; Rais hawezi kuwa "Dikteta kidogo"

Unajua nimegundua kuwa watu wengi humu ni vilaza wa kutupwa na huwa wanafuata mkumbo tu. Inashangaza sana kuona kuwa hadi sasa hivi kuna watu hawaelewi mswada uliopitishwa na bunge unahusu nini. Hali ikiwa hivi humu ndani kwa ma-great thinker je itakuwaje huko nje?

vizuri kabisa.. nendeni mkatoe maoni kwenye hiyo tume itakayoundwa; wananchi wengine wasioridhika na mchakato ulivyo wanayo haki ya kukataa. Kama huna tatizo na mchakato na dhana ambayo imeongozwa huu mswada una wajibu mmoja tu kushiriki.
 
Hata kama ningekuwa na tatizo na utaratibu mzima wa mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi, kwa sasa hakuna njia yoyote itakayoweza kutumika kuupinga. Itatulazimu tuukubali mchakato jinsi ulivyo kwasababu ndivyo KATIBA iliyopo inavyotaka uwe. Kinyume cha hapo ni kutaka kuiingiza nchi kwenye machafuko yasiyo ya lazima kitu ambacho watanzania wengi wasingependa kukiona baada ya kushuhudia shida walizopata majirani zao kwa aina hiyohiyo na migongano.
 
Ninaendelea kuonesha makosa ya kimantiki na kifalsafa ya hotuba ya Rais Kikwete jana. Mojawapo ya mambo ambayo aliyadai akikanusha kuwa yeye si Dikteta ni kauli hii ambayo sidhani kama watu waliielewa uzito wake. Rais alidai kitu kingine ambacho nacho pia hana!
Hiyo ni mifano michache tu. Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais kuwa yeye ndiye anatoa uhuru na kuwa anaweza kuuondoa uhuru huo wa kuwa "dikteta kidogo" haina msingi. Uhuru wetu hautoki kwa Rais. Period.
Mkuu labda kabla sijachangia hoja yako kwanza naomba nikuulize je ni kweli JK sio "Dikteta" kama alivyotuhumiwa ama ni dikteta?
 
Unajua nimegundua kuwa watu wengi humu ni vilaza wa kutupwa na huwa wanafuata mkumbo tu. Inashangaza sana kuona kuwa hadi sasa hivi kuna watu hawaelewi mswada uliopitishwa na bunge unahusu nini. Hali ikiwa hivi humu ndani kwa ma-great thinker je itakuwaje huko nje?
Mkuu wangu Ukilaza nadhani unao mwenyewe kwa sababu unataka kushurutisha vitu. Mimi nimesema kwa nini linapokuja swala la Katiba mpya wanazungumziwa JK, Slaa na wengine wakiwasahau wananchi?..

Mimi nazungumzia ktk position waliyokuwepo JK na hao kina Slaa na sio litoke kwao na kuja kwa wananchi. Mkuu wangu hamuelewi kitu gani hapa. Hatua ya kwanza JK anaamua katiba mpya, safi tunamkubali, inayofuata anataka kuchagua tume, Slaa anasema hapana kwa nini?.. well tuseme anataka awe yeye mchaguzi basi...Well, tunachouliza sisi kwa nini isiwe sisi wananchi ndio tuchague ktk hatua hiyo hiyo?..Kwa nini sio sisi tuchague delegates toka sehemu zetu wenyewe waratibu mawazo yetu kisha wayawakilishe iwe bungeni au Ikulu..Kama tunaweza wachagua wabunge, madiwani makatibu kata na kadhalika tutashindwa vipi kuwachagua waratibu wetu kutuwakilisha?..

Kama rais ana madaraka makubwa kiasi hicho mnachodai basi achague hata wabunge madiwani na kadhalika ikiwa swala ni kuwa na mwakilishi...Hii ikiwa na maana amri inatoka huku kwetu wananchi tunawatuma huko kuwakilisha kama wabunge na sio wawakilishi watoke Ikulu kutaka kujua sisi tunataka nini...Hawa watakuwa wawakilishi wa IKULU na sii wawakilishi wa wananchi mnashindwa kuelewa kipi hapa.. Who ever chose a delegate, he represent himself - mtume ni mja wa mtumaji..

Ndio yale sisi tunasema hivi Bakwata hakiwezi kuwa chama cha Waislaam maadam Mufti anachaguliwa na rais..Mufti anatakiwa kuchaguliwa na waislaam ili kuwa represent waislaam kinyume cha hapo anakuwa anamwakilisha rais kwa waislaam. Na ndio maana bakwata hawana sauti kwa serikali kwa sababu Mufti huchaguliwa na rais while wakristu wanachagua viongozi wao wenyewe na serikali inawatambua. Sasa kuna ugumu gani waislaam kuomba wao wamchague Mufti badala ya rais?...
Kigumu kipi hapa kuelewa kama wewe mwenyewe sio kilaza!.
 
Mkuu labda kabla sijachangia hoja yako kwanza naomba nikuulize je ni kweli JK sio "Dikteta" kama alivyotuhumiwa ama ni dikteta?

Binafsi inawezekana JK siyo dikteta ila Tanzania kinamnanamna ni de facto single party dictator state.
 
vizuri kabisa.. nendeni mkatoe maoni kwenye hiyo tume itakayoundwa; wananchi wengine wasioridhika na mchakato ulivyo wanayo haki ya kukataa. Kama huna tatizo na mchakato na dhana ambayo imeongozwa huu mswada una wajibu mmoja tu kushiriki.

Ukitaka usitake hata wewe hapa unatowa maoni na si zaidi ya hayo ingekuwa huridhiki ungekaa kimya au ungejitokeza kuupinga mahakamani, hivi hizi pumba unazomwaga humu siyo maoni yako? Unanchekesha!
 
Mkuu labda kabla sijachangia hoja yako kwanza naomba nikuulize je ni kweli JK sio "Dikteta" kama alivyotuhumiwa ama ni dikteta?

JK alikuwa dikteta na wala si tuhuma ni ukweli, halina ubishi hilo. By JK namaanisha Julius Kambarage.
 
Uhuru wa uhuru wa maoni unatokana na katiba lakini Rais dikteta anaweza ku-tamper na katiba na kuwaondolea watu uhuru wao, ndicho alichokuwa anamaanisha JK. Alikuwa na pointi katika hilo na wala hujamkosoa chochote hapo. Kwani wewe MMM unataka kusema nchi zenye madikteta hazina katiba nzuri? Usitake kukosoa kitu kisichokosolewa hapo ila badala yake mwambie Mbowe ajibu kwanini alimsifia JK bungeni halafu baadaye anaanza kumgeuka kuwa hana haki ya kuunda tume ya katiba.

Haya maneno yako ni baada ya kupona malaria au ilikuwa bado uko hospital? Kama ana uwezo wa kupora haki zisizoporeka ajaribu kama ataweza. Ajaribu kuuwa watu makusudi, ajaribu kutulazimisha wote tuvae suruali fupi kwa wanaume n wanawake wavae kama FF, ajaribu kutufanya wote tuwe mafisadi kama yeye ajaribu uone kama ataweza.

Nina uhakika, hawezi, na akijaribu kabla hajakamilisha hata theluthi ya mpango wake, naye hizo haki zote anazojaribu kuzipora ataporwa.
 
Hata kama ningekuwa na tatizo na utaratibu mzima wa mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi, kwa sasa hakuna njia yoyote itakayoweza kutumika kuupinga. Itatulazimu tuukubali mchakato jinsi ulivyo kwasababu ndivyo KATIBA iliyopo inavyotaka uwe. Kinyume cha hapo ni kutaka kuiingiza nchi kwenye machafuko yasiyo ya lazima kitu ambacho watanzania wengi wasingependa kukiona baada ya kushuhudia shida walizopata majirani zao kwa aina hiyohiyo na migongano.

Ooh ok, nimekupata. Kipengele gani cha Kaitba hii ili huu mjadala ufe kuwa ndivyo kinavyotaka mchakato uwe?
 
The God who gave us life,gave us liberty at the same time the hand of force may destroy but cannot disjoin them. Thomas Jefferson.
 
Ukitaka usitake hata wewe hapa unatowa maoni na si zaidi ya hayo ingekuwa huridhiki ungekaa kimya au ungejitokeza kuupinga mahakamani, hivi hizi pumba unazomwaga humu siyo maoni yako? Unanchekesha!

haya ni MAWAZO ya MMM siyo maoni ya MMM. Kama ni maoni, tueleze nani anayapokea
 
Mkuu labda kabla sijachangia hoja yako kwanza naomba nikuulize je ni kweli JK sio "Dikteta" kama alivyotuhumiwa ama ni dikteta?

Ukisoma maneno yake hayo hapo juu yeye mwenyewe anaamini kuwa ni dikteta mkarimu (Benevolent dictator)... vinginevyo tusingekuwa huru hivi. Tumshukuru kwa kutupa uhuru wetu.
 
Ooh ok, nimekupata. Kipengele gani cha Kaitba hii ili huu mjadala ufe kuwa ndivyo kinavyotaka mchakato uwe?

Sikumbuki kipengele husika lakini katiba inampa mamlaka Rais wa JMT kuunda tume juu ya jambo lolote na kuzunguka kukusanya maoni juu ya jambo husika. Hapo nimekupa mwanga tu jinsi ambavyo katiba inavyompa nguvu Rais.
 
Mkuu labda kabla sijachangia hoja yako kwanza naomba nikuulize je ni kweli JK sio "Dikteta" kama alivyotuhumiwa ama ni dikteta?

...JK ni "Dikteta" japo ataki umma umwone hivyo lakini kama utakumbuka alisha tamka kwa kauli yake mwenyewe ya kwamba(ninamnukuu)..."uraisi wangu hauna HUBIA"....mwisho wa kumnukuu.Kutokuwa na HUBIA na wananchi unao-waongoza ndio sifa kuu ya udikteta,atakalo-amua yeye ndio lifanyike mfano akisema waliokwapua ngawila BOT(EPA) warudishe na wasamehewe hatakiwi mtanzania yeyote kuhoji coz uraisi wake hauna "HUBIA!"...
 
JK alikuwa dikteta na wala si tuhuma ni ukweli, halina ubishi hilo. By JK namaanisha Julius Kambarage.

du! Wewe kweli mnafiki kumbe hapa tupo tunamuongelea jk Nyerere? Atatoka huko aliko kututengenezea katiba? Kama tunamjadili huyo basi tufute tuanze upya kwani wengi hawajailewa thread hii.
 
Sasa hujuwi kama huo mswaada umepitishwa ili wananchi watoe maoni yao? au hayo maoni utayakusanya vipi? kupitia JF? unanchekesha? piga uwa, huwezi kutetea ujinga. Tume ya kuratibu na kukusanya maoni lazima iwepo, halikwepeki na hiyo hiyo katiba (uliyoonesha kifungu bila kukinukuu) ndiyo inampa Rais uwezo wa kuunda tume, kama walivyounda wa kabla yake. Mlitaka apewe Slaa kuunda tume? basi wangepewa CUF walioanzisha mjadala wa Katiba mpya na wakafikia mpaka kuandika katiba yao wanayoona kuwa ndio sahihi au hilo hulijuwi?

Kwa nini basi raisi ang'ang'anie kila kitu:
anaunda tume ya kukusanya maoni
anawapa hadidu za rejea
anaunda secretariate
anaunda bunge la katiba
anapewa maoni yaliyokusanywa
anaamua nini cha kufanya baada ya kupokea maoni

wanachi wanapiga kura kama wanataka katiba:
tume imechaguliwa na raisi

Kwani watu wengine na au vyombo vingine haviwezi kufanya kazi hiyo? Mpaka kazi zote afanye yeye

Anayelipa mpuliza filimbi ndieye anayechagua wimbo, tuna uhakika gani kama Rais hatachagua wimbo anaoutaka katika mazingira yaliyotajwa hapo juu?

Maoni yoyote ya wananchi kwa mfumo wa kulimbikiza kiasi hiki hayawezi kuonekana kuwa ni yao
 
Mkuu wangu Ukilaza nadhani unao mwenyewe kwa sababu unataka kushurutisha vitu. Mimi nimesema kwa nini linapokuja swala la Katiba mpya wanazungumziwa JK, Slaa na wengine wakiwasahau wananchi?..

Mimi nazungumzia ktk position waliyokuwepo JK na hao kina Slaa na sio litoke kwao na kuja kwa wananchi. Mkuu wangu hamuelewi kitu gani hapa. Hatua ya kwanza JK anaamua katiba mpya, safi tunamkubali, inayofuata anataka kuchagua tume, Slaa anasema hapana kwa nini?.. well tuseme anataka awe yeye mchaguzi basi...Well, tunachouliza sisi kwa nini isiwe sisi wananchi ndio tuchague ktk hatua hiyo hiyo?..Kwa nini sio sisi tuchague delegates toka sehemu zetu wenyewe waratibu mawazo yetu kisha wayawakilishe iwe bungeni au Ikulu..Kama tunaweza wachagua wabunge, madiwani makatibu kata na kadhalika tutashindwa vipi kuwachagua waratibu wetu kutuwakilisha?..

Kama rais ana madaraka makubwa kiasi hicho mnachodai basi achague hata wabunge madiwani na kadhalika ikiwa swala ni kuwa na mwakilishi...Hii ikiwa na maana amri inatoka huku kwetu wananchi tunawatuma huko kuwakilisha kama wabunge na sio wawakilishi watoke Ikulu kutaka kujua sisi tunataka nini...Hawa watakuwa wawakilishi wa IKULU na sii wawakilishi wa wananchi mnashindwa kuelewa kipi hapa.. Who ever chose a delegate, he represent himself - mtume ni mja wa mtumaji..

Ndio yale sisi tunasema hivi Bakwata hakiwezi kuwa chama cha Waislaam maadam Mufti anachaguliwa na rais..Mufti anatakiwa kuchaguliwa na waislaam ili kuwa represent waislaam kinyume cha hapo anakuwa anamwakilisha rais kwa waislaam. Na ndio maana bakwata hawana sauti kwa serikali kwa sababu Mufti huchaguliwa na rais while wakristu wanachagua viongozi wao wenyewe na serikali inawatambua. Sasa kuna ugumu gani waislaam kuomba wao wamchague Mufti badala ya rais?...
Kigumu kipi hapa kuelewa kama wewe mwenyewe sio kilaza!.

kinacho msumbua Mwita25, Rejao na FF, inawezekana hawajui nini maana ya katiba, nani wenye katiba na nani bosi. Wakijua hilo, nadhani wataungana na activist wote wanotaka katiba iratibiwe na wananchi na sio serikali ya CCM.

Kifupi ni kwamba, wananchi ndio wenye nchi. Ndiyo msingi wa kila kitu ndani ya nchi. Na kwa mjibu wa katiba iliyopo hewani, vyombo vyote vya dola (SERIKALI, BUNGE NA MAHAKAMA) pamoja na taasisi nyingine za umma, za kiraia zinatakiwa kuwajibika kwa wananchi.

Katiba hii, imeweka wazi masuala haya, lakini kwa hila za viongozi wa CCM, wakabadilisha na kuongeza vingele vinavyowakuza RAIS aonekane ni mhimu kuliko wananchi. Ndio maana wanakiburi ambacho hakuna anayeweza kuwagusa. Haya ni makosa makubwa.

Sikumbuki kipengele husika lakini katiba inampa mamlaka Rais wa JMT kuunda tume juu ya jambo lolote na kuzunguka kukusanya maoni juu ya jambo husika. Hapo nimekupa mwanga tu jinsi ambavyo katiba inavyompa nguvu Rais.

Umesahau kuwa katiba iliyopo ni ya milele? umilele wa katiba hautoi fursa kuundwa nyingine isipokuwa kurekebisha iliyopo. Hivyo basi, ana mamlaka hayo lakini si ya kuunda katiba mpya mpya
 
Back
Top Bottom